Pwani: Mwalimu wa shule ya msingi Mwendapole anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumshambulia Mwanafunziwa miaka 12 kwa fimbo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
JESHI la polisi mkoani Pwani, linamshikilia mwalimu Evata Mboya,wa shule ya msingi Mwendapole,Kibaha, kwa kosa linalodaiwa ni kumshambulia kwa fimbo mwanafunzi na kumsababishia maumivu makali ya kichwa.

Mwanafunzi huyo wa darasa la tano ,miaka 12 ,walipewa adhabu ya kuchapwa fimbo na wenzake ambao walikuwa wakipiga kelele darasani.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alithibitisha kuhusu tukio hilo na kusema ,mwalimu huyo alitoa adhabu kwa wanafunzi 15 waliokuwa wanapiga makelele darasani ambapo walipigwa fimbo tatu kila mmoja.

Alieleza,baada ya muda walimu wakiwa ofisini walishangaa kuona wanafunzi wengine wakiwa wamembeba mtoto huyo huku akilalamika maumivu makali ya kichwa ,hali iliyosababisha kumpeleka hospital ya Tumbi na hali ilizidi kuwa mbaya ambapo mtoto huyo alihamishiwa hospital ya Mloganzila kwa matibabu zaidi .

Wankyo alifafanua ,mtoto anaendelea na matibabu na mwalimu Evata anaendelea kushikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea kufanyika na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Wakati huo huo,
Jeshi la polisi likiwa doria eneo la Ruvu JKT ,Mlandizi,lilifanikiwa kumkamata dereva Alfajiri Kibonda (33)wa USA River ,Arusha akiwa na gari yenye namba za usajili T.173 CMK aina ya Toyota Chaser,ambayo inadhaniwa ni gari la wizi .

Wankyo alibainisha,dereva huyo hana nyaraka halali hivyo amewataka wananchi kama yupo aliyeibiwa gari tajwa na akiwa na nyaraka halali afike katika jeshi hilo .

Katika hatua nyingine Shaban Salum (70)mkazi wa Mkange ,Chalinze na Ally Hussein (79) mkazi wa Bwilingu wamekamatwa na polisi kwa kosa la kumiliki silaha aina ya gobore ambazo hazina vibali vya umiliki .

Wankyo aliiasa jamii kutoa ushirikiano wa taarifa ya wahalifu wowote , kwa jeshi hilo ili kupambana na uhalifu mkoani humo .
 
Seeikali sio ya kutegemea kabisaaa,majuzi kati Ndalichakoo akasema wanafunzi wapigwe wasiachwe wakaendelea lufanya makosa lakini likikukuta kila mmoja anakuruka.Daaa ualim jamani shughuli.
 
Physical assault ni kosa la jinai,,mwalimu apewe adhabu kali,ili iwe fundisho kwa wengine
Unafurahia mikasa ya wenzako au siyo Mkuu, Nakuombea heri hili pepo la roho ya Kichawi litoke Moyoni mwako mkuu. Hapo ulipo ni Mchawi kamili uliyekosa vifaa.
 
Serikali ingetoa tamko juu ya adhabu ya viboko, either iwepo au isiwepo na kama ikiwepo basi serikali ijicommite kwa hawa walimu yanapotokea mambo kama haya..

Huyu kijana amechapwa na wenzie kadhaa fimbo tatu tatu lakini ni yeye pekee ameonyesha tatizo hapa inaonyesha huyu kijana ni mgonjwa tokea nyumbani na matatizo haya inaonekana si wazazi au walimu anayefahamu bali ghafla ndio yamejulikana kwa hali kama hii tunawaweka walimu kwenye risk sana...
 
Jamii imebadirika sana na hali ya binadamu kiafya imebadirika sana, ni vyema hii adhabu ya viboko ikaangaliwa namna ya kutekeleza na sheria ikawepo ikieleza nini kifanyike wakati wa kutoa adhabu hii kwa wanafunzi... Kuendelea kuacha hali hii ni kuwaweka walimu wetu kwenye risk zisizo na maana..
 
Back
Top Bottom