Pwani: Mume, nduguze wawili mbaroni kwa kuua mke baada ya fumanizi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Chacha Machangu (27) mkazi wa Kibindu kata ya Kibindu Tarafa ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, kwa tuhuma ya kumuua mke wake kwa kumkatakata kwa panga kisha kumfukia kwenye shimo.

Aidha linawashikilia ndugu zake wawili kwa kushiriki tukio hilo la kumuua mke ambapo baada ya mauaji hayo walichimba shimo na kuufukia mwili wake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa alisema lilitokea Machi 10 saa 8 mchana Kibindu.

Nyigesa alisema baada ya mtuhumiwa kumfumania mkewe alimshambulia kwa kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha yaliyosababisha kifo usiku wa tukio hilo.

“Baada ya kumuua mtuhumiwa akishirikiana na ndugu zake, Emmanuel Machangu (19) na Hamis Machangu (22) wote wakazi wa Kibindu, walichimba shimo kwenye shamba la mahindi na kumfukia marehemu,” alisema Nyigesa.

Alisema walipata taarifa na kufuatilia na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote watatu Machi 19 na kwa ridhaa yao wenyewe walionesha shimo lilipo.

“Ilibidi Polisi wafukue na kuukuta mwili wa ambapo ulifanyiwa uchunguzi na daktari na kufanyiwa maziko na ndugu zake kwa heshima zote tofauti na walivyofanya watuhumiwa kuuzika bila ya taratibu,” alisema Nyigesa.

Chanzo: HabariLeo
 
Swali la kishuwa; Alimfumania akijifanyisha kibaharia au? Mbona huyo mmbaba hajakatwa katwa ila mmama ndiye kakatwa katwa? Mfumo dume haujaanza leo. Mafarisayo wakamletea Yesu mwanamke aliyefumaniwa. Kumbuka Yesu alivyo wajibu waliofumania.
 
"na kwa ridhaa yao wenyewe walionesha shimo lilipo."
 
Ulitaka wamfanyeje mwanaume? Kwanza amekosea Nini? Mwanamke kutongozwa lazima ila kukubali ilhali anajua ana mume wake ni kosa lake. Pamoja na hayo kitendo walichokifanya hawa maharamia siyo sahihi na inapaswa wapate haki yao
Swali la kishuwa; Alimfumania akijifanyisha kibaharia au?? Mbona huyo mmbaba hajakatwa katwa ila mmama ndiye kakatwa katwa?? Mfumo dume haujaanza leo. Mafarisayo wakamletea Yesu mwanamke aliyefumaniwa. Kumbuka Yesu aivyo wajibu waliofumania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora huyu mjomba baada ya kumpiga mapanga mkewe angeenda kujisalimishwa police kuwa ame ua bila kukusudia...sasa ameenda mpaka kufukia kabisa huyo ataonekana alikusudia kabisa.
 
Ulitaka wamfanyeje mwanaume? Kwanza amekosea Nini? Mwanamke kutongozwa lazima ila kukubali ilhali anajua ana mume wake ni kosa lake. Pamoja na hayo kitendo walichokifanya hawa maharamia siyo sahihi na inapaswa wapate haki yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Marehemu hawezi jitetea na kusema yaliyo tokea. Kama alifumaniwa lazima aliyekuwa akifanya naye awepo hapo ndo fumanizi hutimia. Kumbuka; kama amemchukia mkewe aweza tengeneza hilo lipicha tu na kumfyekelea mbali
 
Life is not fair huyo mwanamke alihitaji kuiburudisha nafsi yake ila kaishia kuuwawa, watuhumiwa umri 19, 22 bado wana ndoto nyingi za kutimiza ila ndio basi tena, wazazi wa watumiwa na marehemu wote walikua wanawategemea vijana wao ila ndio basi tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote aya wanaume tunajitakia kwa kupenda mwanamke. Wee gegeda tu mambo yakisema oh huyu ni wangu tuu nikujiletea matatizo kama haya siku ukija kujua watu waigegeda papuchi ya mkeo.
 
Back
Top Bottom