PWANI: Majambazi 4 wameuawa katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Kikosi kazi cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kimeua watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika majibizano ya silaha huko katika kijiji cha Mtambani kata ya Tambani wilayani Mkuranga mkoani Pwani na kufanikiwa kukamata silaha aina ya Shortgun Pump Action ikiwa na risasi Tano ndani ya Magazini na nyingine 6 za Shortigun zikiwa ndani ya mfuko wa rambo pamoja na risasi nane za Pistol.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Temeke Kamishna Msadidizi Mwandamizi Gilles Mroto akizungumzia tukio hilo amesema mnamo tarehe 21 mwezi wa kumi mwaka huu majira ya saa 5:30 kikozi kazi kilifanya ufuatiliaji na kubaini majambazi hayo katika nyumba ambayo hiajaisha imezungushiwa uzito na mlango wake muda mwingi ukiwa umefungwa na walipofika eneo la tukio waligonga mlango wakiomba waliopo ndani wajisalimishe ndipo ghafla milio ya risasi ilianza kutoka ndani ya nyumba hiyo na kufanya askari kujipnga katika medani ya kivita ili kujibu mashambulizi .

Kwa mujibu wa kamishna Mroto amesema katika mpambano huo majambazi wengine walitoroka na watatu walifariki wakati wakikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na risasi na msako uliendelea kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mtambani na mnamo majira ya saa 3 asubuhi jambazi mmoja alipatikana akiwa mahututi na jeraha lake na akiwa njiani kukimbizwa hospitalini alifariki dunia huku askari wao mmoja akijeruhiwa katika bega lake la kushoto na kulazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisubiri kufanyiwa upasuaji.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Mroto ametoa wito kwa wananchi mkoa wa kipolisi Temeke Pwani na mikoa yote ya kipolisi kanda maalum kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo katika kufichua uhalifu ili maeneo yote yawe na utulivu na amani.

Chanzo: ITV
 
Safi sana, hao waliotoroka nao watafutwe na kupokonywa silaha haraka hata kama watafariki wakati wanapelekwa hospitali.

Tumechoka na majambazi.

Pole askari wetu uliyeumia, tunakuombea kwa Mungu upone haraka.
 
Lakini Ni majambazi kweli?,kuwaamini Polisi wetu yataka moyo Sana...na Kama kweli hongera kwao.
 
Hongera jeshi letu la police, na endeleeni kuwatusuwa wanasumbuwa sana, halafu pwani kuna nini why majambazi wanakimbilia sana kujificha huko? Km ni mapori hata tabora yapo au kuna nini cha ziada, naomba nijulishwe wanajamvi.
 
Back
Top Bottom