Pwani: Kiongozi mwingine wa CCM auawa kinyama Ikwiriri

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mjumbe wa shina la CCM Ikwiriri eneo la Darajatatu ameuawa jana na watu wasiojulikana.

=====

Wingu la mauaji limezidi kutanda katika Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani. Taarifa zinasaema kiongozi mwingine wa CCM ambaye ni mjumbe wa shina, ameuawa katika kijiji cha Ikwiriri na watu wasiojulikana na mwili wake kutelekezwa eneo la Daraja tatu Wilayani humo.

Akizungumza na Mtanzania jana Ndugu wa Marehemu, Isaka Hamis alimtaja ndugu yake aliyeua kuwa ni Masunga Mayuka.

Nlipokea taarifa za tukio hilo leo(jana) asubuhi wakati huo nikiwa nyumbani kwangu. Mdogo wangu ambaye anaishi Ikwiririndiye wa kwanza kunijulisha juu ya tukio hilo, alinipigia simu, alisema Isaka.

Alisema kwa mjibu wa Maelezo ya mdogo wake huyo, ndugu yao aliuawa akiwa njiani kwenda Msikitini kufanya ibada.

" Mdogo wangu alinieleza, inadaiwa Mayuka alikutana na wauaji njiani ambao walimpiga Risasi na baada ya kitendo hicho walitokomea kusikojulikana" alisema.

Alisema saa chache baada ya kupokea simu ya mdogo wake huyo, alipokea tena simu ya ndugu yake mwingine ambaye naye alimjulisha jambo hilo hilo la kusikitisha.

"Nlielezwa kwamba ndugu yangu aliuawa huku akiwa anajitetea mbele ya watu hao Wasimdhuru, Sasa tupo msibani tunajiandaa kwa maziko" alisema Isaka.

Akizungumza na Mtanzania Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga, alise,a hajapokea taarifa hizo na kuahidi kuzifanyia kazi. "Sina hizo taarifa, sijazipokea labda na mimi nizifuatilie hivi sasa". alisema.

Tangu mauaji hayo yatokee, inadaiwa watu takriban 38 wamekwisha kuuawa.

Chanzo: Mtanzania
 
Hali inaogopesha sasa tutafanyaje Tayari IGP ameshaongea na wazee wa Kule basi waandike barua za Madai yao kama Alquida au Alshabab tujue wanataka nini?

Ni Ngumu Kukisia wauaji wa Kibiti/Ikwiriri wanataka nini? Ukizingatia serikali huwa haiendi kwa Waganga wa Kienyeji.

Toeni Mikanda ya Video mtueleze mnataka nini?
IMG_20170612_084849.jpg
 
Hali inaogopesha sasa tutafanyaje Tayari IGP ameshaongea na wazee wa Kule basi waandike barua za Madai yao kama Alquida au Alshabab tujue wanataka nini?

Ni Ngumu Kukisia wauaji wa Kibiti/Ikwiriri wanataka nini? Ukizingatia serikali huwa haiendi kwa Waganga wa Kienyeji.

Toeni Mikanda ya Video mtueleze mnataka nini?

siyo kwamba mlishasema ni upinzani
 
"Nilielezwa kwamba ndugu yangu aliuawa huku akiwa anajitetea mbele ya watu hao Wasimdhuru, Sasa tupo msibani tunajiandaa kwa maziko" alisema Isaka.
Kama kuna watu waliona akijitetea ina maana hawakumtambua muuaji hata mmoja, haya mambo ni ya kufikirisha sana.
 
Back
Top Bottom