Pwani Kenya wanataka kujitenga

arigold

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
600
341
Natazama KTN hapa. Naona waafrica washaanza kuamka

haya mambo ya kulazimishana kuwa pamoja watu washachoka kila mmoja anataka kwenda kivyake
 
Mkuu Znzbar hawataki kujitenga bali wanataka kuchukua nchi yao, na nitofauti na Mombasa sio nchi ila ilikuwa sehemu ya Znzbar hao ndio wanataka kujitenga kutoka Kenya.
 
Kuna mpango wa kuitenga pwani ya afrika mashariki na kuvunja muungano ili pwani ya Afrika Mashariki iungane na Zanzibar na kurudi enzi za utawala wa kisultani. MRC ya Mbombasa ni sawa na Uamusho huko Zanzibar.
 
zamani nilikuwa na ujinga wa muungano na umoja wa kitaifa...siku hizi huniambii kitu au mshasahau kama Nyerere aliunga mkono Boafra kujitenga?

kisha tuaona East Timor, then Somaliland, Kosovo na juzi serikali yetu imeunga mkono south sudan kujitenga sasa sioni sababu ya watu kukaaa pamoja kama wengine hawataki

watu lazima wawe huru kujiamulia wanakotaka kwenda
 
Kuna mpango wa kuitenga pwani ya afrika mashariki na kuvunja muungano ili pwani ya Afrika Mashariki iungane na Zanzibar na kurudi enzi za utawala wa kisultani. MRC ya Mbombasa ni sawa na Uamusho huko Zanzibar.

wafanye watakavyo

lakini enzi za kulazimishana kwenye umoja wa kitaifa huku wengine ndio wanafaidia halikubalini hata kidogo
 
Back
Top Bottom