Pwani kajifunzeni Detroit ubaya wa viwanda vingi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,232
12,506
Mapinduzi ya viwanda duniani yalitokea Marekani kwenye mji wa Detroit Jimbo la Michigan.

Mji huo sasa hivi yamebaki magofu ya viwanda hivyo kutokana na madhara makubwa yaliyotokana uchafuzi wa mazingira.

Hewa, maji na viumbe viliathiriwa sana na uchafu kutoka viwandani na kusababisha magonjwa ya saratani na mfumo wa hewa na vifo vingi vilivyosababisha wafanyakazi migomo mikubwa wakidai fidia kubwa na mishahara mikubwa.

Hali hii ilipandisha gharama za uzalishaji viwandani Marekani na ndiyo iliyosababisha viwanda vya mji huo vihamishiwe Asia ili kupata unafuu wa uzalishaji. Lakini wamehamishia tatizo la uchafuzi wa mazingira kwenye mataifa mengine.

Wakati mkoa wa Pwani mkishangilia viwanda vingi kumbukeni hatima ya wajukuu wenu pia kiafya na kimazingira.
 
Usifananishe viwanda vya nyuklia na vya katani chief.
Pale Detroit vikubwa vilikuwa ni vya kuunda magari kama General Motors, chevlorent nk, meli na vingine kama vilivyoko Pwani. Kitu cha msingi hapo ni wastes zitakazoweza kuchafua maisha ya maji, ardhi, mimea na viumbe hai vingine wakiwemo wakwere na wazaramo.
 
Kuna vitu vingine lazima vifanyike hata km vina athari kwa namna flan,ni sehem gn hakuna mimea na viumbe hai wengine ili viwanda vikajengwe huko na pwani ipone.
 
Kuna vitu vingine lazima vifanyike hata km vina athari kwa namna flan,ni sehem gn hakuna mimea na viumbe hai wengine ili viwanda vikajengwe huko na pwani ipone.
Mipango na technolojia sahihi ni muhimu
 
Suala la pwani kujenga viwanja vingi limetokea automatically-viwanja bei rahisi na iko karibu sana na Dar ambako kuna soko kubwa sana la mahitaji mbalimbali. Nilishangaa sana rais alipowamwagia sifa viongozi wa mkoa wa pwani kana kwamba kuna jitihada ya msingi wameifanya-tofauti na viongozi wa mikoa mingine.

Hivyo suala la Pwani kujengw viwanda vingi limekuja lenyewe kutokana na kuwa strategic location kwa malighafi na soko. Hakuna kitu watu wa pwani wanaweza kufanya kuzuia viwanja.
 
Lazima waseme sasa ni viwanda vingapi na vya aina gani vijengwe wapi. Wawe na habari kamili juu ya faida na hasara ya hiwanda hivyo kiuchumi, kijamii na kiafya.
 
Lazima waseme sasa ni viwanda vingapi na vya aina gani vijengwe wapi. Wawe na habari kamili juu ya faida na hasara ya hiwanda hivyo kiuchumi, kijamii na kiafya.
Sioni kama kuna mtu atawasikiliza, hasa ukizingatia uchafuzi wa mazingira kwa kutumia viwanda uko chini sana kwa nchi zetu masikin. Mambo ya viwanda yana siasa nyingi sana hata ktk nchi zilizoendelea, ndo maana USA akajitoa ktk Paris Agreement.
 
Mkuu hivyo viwanda vyenyewe vya pwani umeviona lakini?Vingi ni vya yeboyebo,rasta,matunda na mikoba.Ni small scale industrial area.
 
Ni uboya kufananisha Detroit ya mwaka 1710 na Tanzania ya mwaka 2017 aisee..
 
Ni uboya kufananisha Detroit ya mwaka 1710 na Tanzania ya mwaka 2017 aisee..
Kwanin,heb nyumbua tukuelewe,..maana kiwanda ni kiwanda tuu,hata kama small scale,waste za malighafi ni zile zile though kwa wenzetu zilizid sabab wanatumia energy ya nuclear..maana idad ya viwanda vilivyopo pwan inaelekea kua kubwa sana,labda kama hujatembea pwan au si mdau,ila sis wadau tunaelewa idada iliyoko huko,..mfano tuu kuna viwanda vy cement huku vingi,njia ya mkuranga na hata kule visiga madafu,na vya gypsum,na chuma etc
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom