Pwani: Baada ya Rais kung'aka, gari la wagonjwa lakarabatiwa, vyoo vya soko vinaendelea kujengwa na mgogoro wa wakulima na wafugaji kutatuliwa

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
875
545
Lile Sakata la Kaimu DED Rufiji aliyewekwa ndani kwa kudaiwa kuwa amemdanganya mkuu wa nchi leo limechukua sura mpya baada ya TEMESA kukiri kuwa Gari lilikuwa bovu na kuwa wameshalitengeneza. Nisiwachoshe karibu msikie wenyewe.

MAAGIZO YA MH RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI YAANZA KUTEKELEZWA PWANI

==========

Mtakumbuka kwamba tarehe 30/07/2020 tulikuwa na ziara ya Mh. Rais alipita katika mkoa wa Pwani na alipita katika wilaya zetu tatu kwa maana ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti. Katika wilaya hizo aliongea na wananchi na kutoa maelekezo mbalimbali.

Alipokuwa wilaya ya Rufiji alitengua uteuzi wa DC. Njuayo na Kumteua Ruteni Kanali Patrick Sawala ambae sisi kama mkoa tulimuapisha tarehe 31/ 07/ 2020.

GARI LA KUBEBA WAGONJWA
Na akiwa pale Rufiji kulikuwa na changamoto ya gari la wagonjwa "Ambulance" taarifa ambazo zilitolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rufiji ni kuwa gari lile la wagonjwa lilikuwa bovu, na Rais akatoa maelekezo kuwa ndani ya siku tano gari hilo litarabatiwe na liwe limetengenezwa.

Na leo nafurahi kuwaonesha kwamba maelekezo ya Rais yametekelezwa gari hilo limetengenezwa na TEMESA na nitalikabidhi kwa mganga mkuu wa mkoa na dereva wake yupo hivyo litakwenda Rufiji kuanza kazi.

UJENZI WA CHOO
Na alipokuwa Kibiti alitoa maelekezo kwa almashauri ya wilaya ya Kibiti ukamilishe mara moja ujenzi wa vyoo vya soko la pale Kibiti.

Nafurahi kuwataarifu kuwa kwa taarifa ambazo nimepewa asubuhi hii na wataalam wetu wa regional secretairiete baada ya kuwa wametembelea eneo lenyewe na pia nimeongea na mkuu wa wilaya na mkurugenzi wamesema kuwa matundu tisa na ifikapoJumamosi inayokuja yaani kwamba mabafu mawili na vyoo saba vitakuwa tayari vimekamilika.

MGOGORO WA ARDHI
Alipokuwa pale Mkuranga pamoja na mambo mengine mengi limeibuka sUala la mgogoro wa ardhi yenye takribani ukubwa wa hekari 1750 na akatoa maagizo kwamba Mkuu wa wilaya, mbunge na mkurugenzi wafanyie kazi utatuzi wa mgogoro huo na kwa taarifa nilizozipata leo asubuhi ni kwamba tayari wizara ya imeshawaita wahusika wote wa ardhi ile tayari juzi wameshafanya mazungumzo na katibu mkuu na kamishna wa pale wizara ya ardhi na leo tumepokea taarifa kuwa kesho tarehe nne na tano Waziri wa ardhi atakuwa na ziara wilaya ya Mkuranga pamoja na mabo mengine atakwenda kushughulikia suala la mgogoro wa ardhi hekari 1750 kulingana na maelekezo ya Rais.

Sasa niwaombe sana wananchi wa wilaya ya Mkuranga hasa eneo lile lenye mgogoro wa ardhi maana kwa taarifa ambazo nimepewa na vyombo vyetu vinasema baada ya Rais wananchi walikwenda kuvamia shamba lile na kugawana wakidhani rais amewapa shamba lile, hapana rais hakuwaagiza muende kuvamia shamba lile haikuwa hivyo maelekezo yalikuwa kwa wizara na serikali ya wilaya ya Mkuranga walitolee utatuzi suala hilo, kwa hiyo wananchi walivamia shamba lile maelekezo hayakuwa hivyo.

Kwa hiyo niwaombe sana waganga wakuu wa hospitali magari haya ya wagonjwa kuwa ni muhimu sana tusisubiri wananchi wamlalamikie kiongozi mkuu wa kitaifa wakati sisi tupo, Tuhakikishe magari haya yanakuwa salama na kama gari lina natatizo ni jukumu lenu kulitengeneza. Basi tuyashughulikie sio mpaka Rais aje na hata matatizo mengine ya wananchi sio hadi rais aje atukumbushe kutatua mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu ni aibu kabisa.

UPDATE

Mh JPM amemsamehe kaimu DED kwa kosa la kusema uongo kuwa gari la wagonjwa “ Ambulance “ kuwa ni mbovu , Ilhali Gari ni zima .
 
Hii nchi kila kitu kinawezekana kukiwa na usimamizi madhubuti.
Hivi kweli hii nayo ni kazi ya Mkuu wa nchi kweli??
Ndio maana kila mteule wa Rais hawezi kusema nime fanya au wizara ime fanya. Instead kila kitu JOM kafanya.
Basi hamfai kuwepo kwenye hizo position..
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tanzania na watanzania ni wagumu sana.

Naanza kuamini hii nchi kupata maendeleo ni ngumu sana.

Kuanzia mwananchi mpaka viongozi wake ni shida tupu.

Rais awe Magufuli, Tundu lissu lipumba au yeyote yule bado hamna kitakacholeta mabadiliko makubwa ya kusema kweli hapa tumepiga hatua ya kutoka kwenye 1 kwenda 80 au 90.

Ni watu wachache sana wanaojali maslahi ya taifa hili, narudia tena wachache sanaa.

Kuanzia mwananchi wa chini mpaka viongozi wa juu woote ni wabinafsii, sijui ndio asili ya mtu mweusi.

Kila mtu akipata mwanya anataka kupiga, baadae huyo huyo analalamikia huduma mbovu hospitalini, barabara mbovu, shule hamna madawati, elimu mbovu.

Mtu huyo huyo mpigaji anataka apewe madaraka ya kuongoza wananchi, na atapewa na wananchi na viongozi walewale wapigaji, maono yake ni upigaji.

Itoshe kusema tunasafari ndefu sana.

Vizazi vitakavyoweka mbele maslahi ya taifa hili ndio wenye nafasi ya kuibalisha nchi hii kuwa ya asali.

Kuna watu watasema taasisi imara ndio msingi, taasisi tunazo imara ila watu sio imara, taasisi imara ni watu imara, hamna watu imara hamna taasisi.
 
Mara nyingi TEMESA wanakataa kutengeneza magari ya serikali kwa sababu wanawadai sana. Kutokulipwa kwa wakati na wateja wao kunaifanya TEMESA wadaiwe na wenye kuuza vifaa vya magari ambao nao wameacha kuwakopesha.Inawezekana kabisa kuwa kawakulitengeneza hilo gari la wagonjwa kutokana na madeni ya Halmashauri.

Amandla...
 
Tanzania na watanzania ni wagumu sana.

Naanza kuamini hii nchi kupata maendeleo ni ngumu sana.

Kuanzia mwananchi mpaka viongozi wake ni shida tupu.

Rais awe Magufuli, Tundu lissu lipumba au yeyote yule bado hamna kitakacholeta mabadiliko makubwa ya kusema kweli hapa tumepiga hatua ya kutoka kwenye 1 kwenda 80 au 90.

Ni watu wachache sana wanaojali maslahi ya taifa hili, narudia tena wachache sanaa.

Kuanzia mwananchi wa chini mpaka viongozi wa juu woote ni wabinafsii, sijui ndio asili ya mtu mweusi.

Kila mtu akipata mwanya anataka kupiga, baadae huyo huyo analalamikia huduma mbovu hospitalini, barabara mbovu, shule hamna madawati, elimu mbovu.

Mtu huyo huyo mpigaji anataka apewe madaraka ya kuongoza wananchi, na atapewa na wananchi na viongozi walewale wapigaji, maono yake ni upigaji.

Itoshe kusema tunasafari ndefu sana.

Vizazi vitakavyoweka mbele maslahi ya taifa hili ndio wenye nafasi ya kuibalisha nchi hii kuwa ya asali.

Kuna watu watasema taasisi imara ndio msingi, taasisi tunazo imara ila watu sio imara, taasisi imara ni watu imara, hamna watu imara hamna taasisi.

kweli kabisa.
 
Kwahio kwa mawazo yake mkuu wa nchi, Tanzania nzima shida kama hizo hazipo ila zipo hapo tu alipotatua ? Hence kuanzia sasa magari ya wagonjwa na vyoo masokoni ni Swafi bin Safi... ?
 
Back
Top Bottom