Pwani: Askari Wawili wa Usalama Barabarani wauawa kwa kupigwa risasi Kibiti

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Muda mfupi uliopita askari polisi wawili wa kikosi cha usalama Barabarani Bungu, Kibiti wamepigwa risasi na kufa papo hapo wakiwa kazini eneo kati ya Bungu na Jaribu! Walikuwa watatu, mmoja wa kike kasalimika!

=========

UPDATES:

Watu wasiojulikana wamemuua askari wa Usalama Barabarani katika Kijiji cha Bungu B wilayani Kibiti, mchana huu.

Taarifa za kuaminika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa gari la askari hao pia limechomwa moto na kwa sasa vikosi vya ulinzi na usalama vinaelekea eneo la tukio.

Tutaendelea kukujuza jina la askari huyo na namna mauaji hayo yalivyotokea hivi punde.

Chanzo: Mwananchi

UPDATES 2:

Rufiji. Askari Polisi wawili wa kikosi cha usalama wa barabarani wilayani Kibiti ambao majina yao bado hayajatambulika wapigwa risasi na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Msafiri,Kata ya Bungu wakiwa kazini.

Mbali na kupigwa risasi, pia watu hao wamechoma moto gari moja na pikipiki moja za askari hao kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema anafuatilia.

Tukio hilo limetokea kilomita chache kutoka eneo ambalo waliuawa askari polisi wanane kwa kupigwa risasi katika eneo la Mkengeni walipokuwa wakitoka doria katika Kijiji cha Jaribu.
Risasi.jpg
 
Aisee, hawaogopi mkulu yuko mkoa wa pwani?

Nilisikia jeshi la wanachi limehamia huko?

Hili sio tatizo la kutuma jeshi kule maana jeshi liko trained kwa visible enemy, sasa hawa hawajulikani jeshi litafanyaje?

Kuna haja ya kufikiria upya jinsi ya kukabiliana na hao watu huko, nguvu kubwa bado sio suluhisho.
 
Back
Top Bottom