Pwani: Askari Polisi agoma kusema CCM oyee. Afukuzwa kwenye mkutano na kiongozi wa CCM, aambiwa atakiona

Mkuu kwa akili zako ili askari awepo kazini lazima awe amevaa sare...or awe yupo kituoni????...askari yupo kazini muda wote na kikawaida hata wewe hapo mtaani kwenu mnaweza mkawa na mkutano wa mtaa na mnaruhusiwa kumuomba askari yoyote aje kwenye mkutano wenu kama kuna jambo mnahitaji lipate ufafanuzi kutoka kwenye vyombo vya usalama
Tatizo liko wapo grand father?
 
Mtu akitaka Kujua Mwisho wa CCM umekaribia Asome Tu comments za Kwenye Hii Thread..iDs Very Genuine na Mawazo Yanaeleweka ni TakaTaka Chache Tu Zimejaribu Kuvamia Uzi Lakini Zimechezea Ngumi za Pua.
 
Yaani CCM wanataka kutuaminisha tunaishi kwa fadhila zao?
Wana CCM wengi ni vilaza wao huamini hata ujenzi wa reli viwanja vya ndege kununua ndege ni Fadhila hawajuia kuwa zile ni pesa za walipa kodi wote nchini ambao idadi kubwa siyo wanachama wa CCM
 
very sorry !
CCM hata sheria walizotunga wenyewe hawaziheshimu..
Code of Ethics and conduct zimeweka wazi umarufuku wa askari kuwa mwanachama wa chama chochote..
Lakini serikali ya CCM hupokea kodi kutoka kwa wapinzani na kwa Ccm wachache, kwa nini askari wasiwajibike kwa wapinzani kwa mantiki hiyo..
Wanaolipa mishahara ni wananchi kupitia kodi zao, CCM ni wajanja tu wanaoishi kwa kodi hizo..
Sasa kuna haja ya kupitisha sheria ili askari wawajibike kwa vyama vya siasa vyote kwani vyote vinalipa kodi zinazotumika kulipa mishahara..
eg ivi pombe hela ya kula anapata wapi nje ya kodi zetu ?
 
Dah...nimejisikia vibaya sana kwa udharirishaji aliofanyiwa huyu askari.
Live bila chenga nauona mwanzo wa mwisho wa hili genge ccm, na kwa vile hawana uzoefu wa kufanya siasa bila mbeleko ya vyombo vya dola basi ndiyo itakuwa kaburi la genge hili hatari kwa ustawi na umoja wa Taifa letu.
Hawa ndiyo watu wanahitajika ktk jamii watu wanaosimama ktk ukweli pasipo kuyumbishwa na yoyote

Huyo MNEC ana tatizo eti huyo nani, ana cheo gani, limeisha hilo anafanya intimidation za kipuuzi lkn ashukuriwe huyo koplo kwa kutoogopa kusimamia anachokiamini
Aiseee ukisikia top down effect ndiyo hii.

Kinachofanyika juu kinashuka na kuigwa chini, WE ARE DOOMED, it is just a matter of time TUNAENDA KUSAMBARATIKA KABISA,

Angalia hii video kwa makini ujionee na usikie mwenyewe,sitashangaa kusikia huyo askari katoweshwa au kachukuliwa hatua kali kwa maelekezo fulani.


View attachment 1181707

Safi pot.. unyanyembe sio miaka hii
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amempongeza askari polisi mkoani Pwani aliyegoma kutumia salamu za chama hicho tawala nchini kwa maelezo kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yake #MwananchiUpdates https://t.co/K6wbfhRBod
 
Polisi munaona mnaowabeba jinsi wanavyo wadharau?
IGP unaitwa majina ya hovyo kwa vile umeruhusu hali hii ishike kasi bila kuikemea.
Zamani nilikuwa nafikiri IGP Mangu ndio alikuwa lainilaini kumbe nilikosea wewe wa sasa sio tuu ni lainilaini bali hawa tuviongozi wa ccm wanakuona mdebwedo kabisa.
Kitendo cha RPC wa Arusha (yule msindikiza dhahabu wa Mwanza) kujikomba kwenye mkutano wa CCM nilijuwa lazima kitaleta madhara makubwa, ona Leo kimekuwa reference ya nini polisi afanye kwa wanasiasa wachovu.
Kama IGP hatoi tamko kwenye hili kweli atakuwa mdebwedo hasa
Watu dizaini ya igp huyu wanaishiaga kubaya sana baada ya utawala kubadilika
 
Hapa chini ni video ikimuonyesha askari wa jeshi la polisi akikataa kusurutishwa kukubali utumwa kutoka kwa viongozi wa ccm.

Amejieleza vya kutosha na akasimamia maadili ya kazi yake na hakuogopa hata pale alipo tishwa na viongozi wa ccm.

Hawa ndiyo aina ya askari taifa linawahitaji ktk kusimamia haki.
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom