Pwani: Askari Polisi agoma kusema CCM oyee. Afukuzwa kwenye mkutano na kiongozi wa CCM, aambiwa atakiona

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Aiseee ukisikia top down effect ndiyo hii.

Kinachofanyika juu kinashuka na kuigwa chini, WE ARE DOOMED, it is just a matter of time TUNAENDA KUSAMBARATIKA KABISA,

Angalia hii video kwa makini ujionee na usikie mwenyewe,sitashangaa kusikia huyo askari katoweshwa au kachukuliwa hatua kali kwa maelekezo fulani.



=====

Bashiru ampongeza polisi aliyegoma kusema ‘kidumu Chama cha Mapinduzi’​

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amempongeza askari polisi wa mkoani Pwani ambaye siku za hivi karibuni aligoma kutumia salamu ya ‘Kidumu Chama cha Mapinduzi’ inayotumiwa na chama hicho tawala nchini Tanzania.

Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Dk Bashiru Ally amempongeza askari polisi wa mkoani Pwani ambaye siku za hivi karibuni aligoma kutumia salamu ya ‘Kidumu Chama cha Mapinduzi’ inayotumiwa na chama hicho tawala nchini Tanzania.

Askari huyo aliombwa kutoa salamu hiyo na mjumbe wa halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho, Haji Jumaa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Vianzi wilayani Mkuranga, kabla ya kueleza kero za kufungwa kituo cha polisi muda wa kazi.

Hata hivyo, askari huyo aligoma akisema maadili ya kazi yake hayaruhusu kutoa salamu hiyo, akidai ni kosa kimaadili.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 27, 2019 katika mkutano wa wanachama wa CCM wilaya ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya ziara yake iliyoanza leo ya kukagua uhai wa chama, miradi ya maendeleo na kuzindua mashina.

Akitoa mfano wa tukio hilo, Dk Bashiru amesema CCM haiwezi kuwa chombo cha nidhamu kwa watumishi wa umma.

"Nampongeza yule askari aliyegoma kufuata maelekezo nataka nimjue hata IGP nilimpigia simu kuhusu tukio hilo.”

"Polisi hapokei maelekezo ya chama chochote cha siasa iwe CCM au CUF. Kama una jambo usibwatuke tu, sitaki kusikia amri au maelekezo yoyote, tukiendelea na tabia hiyo tutakuwa tunajenga nchi isiyofuata sheria,” amesema Dk Bashiru.

Amebainisha kuwa watumishi wa umma wana vyombo vyao vya kuwajibishana na wakati mwingine hupeana adhabu.


 
ASKARI POLISI Agoma Kusema CCM Oyee | Afukuzwa Mkutanoni na Kiongozi wa CCM

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
Na wa aina hii wapo wengi tu, ila hawajui njia ya kujinasua bila madhara kuwapata.

Nadhani kunahitajika pawe na mkakati wa kuwapa aina fulani ya 'support' hata kama ni ya chini chini ili wasidhurike.

Wakishapatikana wengi wa kutosha kuonyesha ujasiri kama huo hadharani, hapo CCM itakuwa imekwisha.
 
Ni mwanzo mzuri kwa jeshi letu kuanza kutambua wajibu wao, yeye kajitoa mhanga ingawa inaweza kumgharimu lkn kesho na keshokutwa wataongezeka walio na ujasiri kama yeye.

IMG_20190815_054654.jpg
 
Polisi munaona mnaowabeba jinsi wanavyo wadharau?
IGP unaitwa majina ya hovyo kwa vile umeruhusu hali hii ishike kasi bila kuikemea.
Zamani nilikuwa nafikiri IGP Mangu ndio alikuwa lainilaini kumbe nilikosea wewe wa sasa sio tuu ni lainilaini bali hawa tuviongozi wa ccm wanakuona mdebwedo kabisa.
Kitendo cha RPC wa Arusha (yule msindikiza dhahabu wa Mwanza) kujikomba kwenye mkutano wa CCM nilijuwa lazima kitaleta madhara makubwa, ona Leo kimekuwa reference ya nini polisi afanye kwa wanasiasa wachovu.
Kama IGP hatoi tamko kwenye hili kweli atakuwa mdebwedo hasa
 
Back
Top Bottom