Pwani: Askari Polisi agoma kusema CCM oyee. Afukuzwa kwenye mkutano na kiongozi wa CCM, aambiwa atakiona

Kinachonishangazaga kuliko yote ukisoma comment moja moja ni lazima kuna fala mmoja wa ccm atakuja kutetea hapa na vijustification vya uongo na ukweli, mimi sipo chama chochote ila nashangaaga sana anapofanya blunder mtu wa ccm, ccm huwa kama hawapo yan wanakuwa kama mazezeta na wao ndio wameishika nchi, Tutachelewa sana kufika tukiendelea na unafki wa watu wa ccm na crew yao,
 
CCM wamejipa mamlaka ya kujimilikisha kodi za watanzania kuwa mali yao. Hii nchi sasa kila kitu ni fadhila za chama hata mshahara uliowekwa kwa mujibu wa sheria na vigezo vya kazi ni hisani ya chama.
Haya ni mawazo yako wewe
 
Hili ni tukio la pili baada ya lile la daktari wa Arusha ingawa naye huyo daktari sababu ya kutokuwa kazini ilikuwa ni upuuzi tu! Ni suala la heshima iliyozidi ambayo binadamu wa uwezo wa chini akipewa, huilawiti. Mambo haya hayako CCM tu, hata vyama vingine. Namkumbuka Cheyo akimfukuza Jidulamabambasi (RIP), ".....OUT!". Ktk serikali pia awamu zote ambazo pesa iliangukia mikononi mwa watu wasio na ubora, wakailawiti na kuwaona wa-TZ wengine kama kalunguyeye.

Ufumbuzi wa matatizo ya aina hii ni kwa CCM na vyama vyote kuingiza watu wenye uwezo mkubwa ktk nafasi kubwa kama hizo. NEC na CC ya chama kikubwa kama CCM si sehemu ya kuungwa mkono tu, ni ubora wa akili!
 
Polisi, wanajeshi, wafanyakazi wa umma inabidi wawe neutral ili kuiweka nchi pamoja. Hawa sio wanasiasa.

Hajakosea, amekosewa inabidi aombwe msamaha, Dar dharau?
Huyu jamaa anatafuta ugomvi .! Ni kada na hana cha kutetea hapa, anachokitafuta ni mtu wa kubishana nae .!
 
huyo MNEC ameistaajabisha jamii.... kuna watu wa ccm wamejichekesha kinafiki hapo lakini nashukuru hawakupiga yale makofi ya kinafiki...... ASKARI AMEONDOKA KIABE HAKIKA.
Ccm wangekuwa wanapenda haki na taifa letu walipaswa kupeana semina za ndani nin jukumu la jeshi la polis kwa jamii.polis wanapaswa kuwa impartial wao hawachangamani na chama chochote cha siasa, pia wafanyakazi wa umma na polis wakiwemo hawalipwi na chama chochote Bali kodi za watanzania wote.
 
Polisi munaona mnaowabeba jinsi wanavyo wadharau?
IGP unaitwa majina ya hovyo kwa vile umeruhusu hali hii ishike kasi bila kuikemea.
Zamani nilikuwa nafikiri IGP Mangu ndio alikuwa lainilaini kumbe nilikosea wewe wa sasa sio tuu ni lainilaini bali hawa tuviongozi wa ccm wanakuona mdebwedo kabisa.
Kitendo cha RPC wa Arusha (yule msindikiza dhahabu wa Mwanza) kujikomba kwenye mkutano wa CCM nilijuwa lazima kitaleta madhara makubwa, ona Leo kimekuwa reference ya nini polisi afanye kwa wanasiasa wachovu.
Kama IGP hatoi tamko kwenye hili kweli atakuwa mdebwedo hasa

Utaratibu wa kistaarabu hapa Jeshi la Police lilitakiwa kutoa tamko elekezi lakini kwa ustaarabu wa hivi sasa sidhani kama itakuwa hivyo
 
Huyu jamaa anatafuta ugomvi .! Ni kada na hana cha kutetea hapa, anachokitafuta ni mtu wa kubishana nae .!

Amemkosea huyu polisi Mr Said, Amuombe msamaha.Kitu kidogo sana.

Muhimu kutomuonea Mtanzania yoyote. Hasa akiwa kazini ili kudumisha amani, mshikano na usalama wa Taifa , hawa ndio wanaotulinda wote
 
Back
Top Bottom