Pwani: Ajali yaua watu watatu, Mungu atunusuru

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,231
35,151
Kwa mwendelezo huu ambao kusafiri usiku kumekuwa heri mno kuwapisha wale jamaa na kero zao, tutegemee matukio mengi tu ya Aina hii. Eeh mola wetu ni Dua zetu kwako utunusuru na haya ambayo common sense tumechagua kuzipuuza huku tukishindana u ninja na kuwa mawe.

Ajali yaua watatu Pwani

Kwa double standard zetu, sisi yakitupata dereva wetu alijitahidi sana. Wao yakiwakuta mwendokasi na tena warejee shule!

Ole wetu sisi maana kwake yeye kila nafsi itarejea na huko ndiko kuliko haki, siyo huku ambako waungwana walipaita ni tambara bovu.

======

Kibaha. Watu watatu wamefariki dunia mkoani Pwani, wawili kati yao katika ajali ya basi iliyojeruhi wengine wanane.

Basi hilo mali ya kampuni ya Modern Coach lililokuwa likitokea Nairobi kwenda Dar es Salaam, liliacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo imetokea jana Ijumaa Agosti 3, 2018 saa 5.45 usiku katika Kijiji cha Kimange kwenye barabara ya Segera - Chalinze.

Akizungumza leo Jumamosi Agosti 4, 2018, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Blasius Chatanda amewataja waliofariki dunia kuwa ni Aliakimu Mkiganda (41) mfanyabiashara ambaye ni raia wa Rwanda na Emmanuel Indimuli (3) raia wa Kenya. Miili yao imehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Amesema majeruhi katika ajali hiyo ni Penina Wango (33), Aliasgher Morbiwalia (18), Adrian Flovick (19), Mohamed Idris (18) Mita Naidhukum (54), Adrin Maula (16), Erick Muthon (30) na Hemik Muthon (49) wote raia wa Kenya.

Amesema majeruhi wote walipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Amesema dereva wa basi hilo amekimbia na juhudi za kumsaka zinaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Katika tukio jingine, amesema mwendesha pikipiki Idd Bakar (20), amefariki dunia baada ya kugongana na basi mali ya kampuni ya ABC lililokuwa linatokea Dar esalaam kwenda Mailimoja, Kibaha.
 
Ajali zinatokea kila siku, hazisikiki kwakua Sinai’s na kujeruhi wapiga kura tu. Hii mmeisikia kwakua imemhusu mpigiwa kura.
 
Yaa Rabb, Mola ulieumba mbingu na Ardhi na yote yaliyomo.

Mola wa Ibrahim, Ismael na Is'haka, wa Yaaqub na wanawe 12. Mola mlezi na mwendesha huu ulimwengu kwa haki.

Mola uliemtuma Mussa, Issa na Muhammad kuwa rehema kwa huu Umma.

Tuangazie viumbe vyako na utulinde dhidi ya hizi ajali.

Wape moyo wa ihsani viongozi wa mataifa yetu watutengenezee barabara zetu tunazozilipia kodi.

Na wape mioyo ya utulivu madereva wetu waendeshe kwa uangalifu, upole na dhamira ya kufikisha roho za waja wako waliowabeba kiusalama.

Tujaalie madereva wote kiujumla tusiwe na papara na tusiwe na ile mentality ya kushindana barabarani. Kwani kwa hakika, lengo la vyombo hivi si kipi kinakimbia kwa kasi zaidi. Bali ni Nyenzo ya kututoa sehemu A kwenda B kwa uharaka ulio salama.

Wape moyo wa imani matrafiki wafanye kazi kwa weledi. Wasiwe wakusanya ushuru zaidi, bali walinda usalama barabarani. Watoe mafunzo na wasimamie haki

Wasamehe ndugu zetu waliotangulia ktk haki kupitia ajali hizi. Wape moyo wa subra na uvumilivu ndugu wa marehemu na ndugu wa majeruhi.

Waponyeshe majeruhi wa ajali hizi, kwani kwa hakika hakuna awezaye kuwezesha kupona kwao ila wewe Mola wetu mwingi wa uponyeshaji.

Wape ustahamilivu madaktari kuvumilia kazi hizi za ziada na utambuzi wa tiba muafaka ya kuwapa majeruhi wetu. Wajaalie pia madaktari wetu hawa ambao wanakuwa overworked wapate ile salary increase wanayoisubiria kwa mwaka wa tatu sasa

Ameen Yaa Rabbal A'alamin
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom