Pwani: 16 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhujumu SGR

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mwenyekiti wa kamati ya Usalama mkoa wa Pwani,Abubakari Kunenge ameeleza watu 16 waliohujumu miundombinu ya mradi wa reli ya kisasa (SGR) pamoja na wengine kuiba saruji katika mradi mkubwa wa umeme Stigo Rufiji wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Aidha ameagiza watendaji waliopo katika maeneo ya mradi wa SGR kutoa taarifa haraka pale watakapobaini wabadhilifu.

Aliweka bayana hayo wakati alipoambatana na kamati ya Usalama mkoa,wakuu wa wilaya ,maDAS kutembelea daraja la kisasa (WAMI ) na karakana na stesheni ya kupokea mizigo kituo Cha Pugu(SGR) ambapo Kunenge ,alitaka ulinzi uimarishwe kwenye maeneo yote ya miradi ya kitaifa iiliyopo Pwani.

Alitaja waliohujumu kanda ya kipolisi Rufiji wapo 11 na Pwani wapo watano.

Kunenge aliwaelekeza wakuu wa Wilaya mradi wa SGR unapopita kuitengeneza kuwa miji na mazingira bora iweze kuendana na mradi huo.

"SGR mradi mkubwa na muhimu yapaswa kulindwa na kuongeza mradi huu unakwenda kuondoa msongamano wa magari na kupunguza ajali barabara kuu ya Morogoro-Pwani-Dar es salaam".

"Matarajio yetu treni hii ya umeme kuanza kazi mwezi wa kumi na moja ili kunufaisha wananchi kwa kurahisisha usafiri na kufika kwa muda mfupi "Na kuomba jamii isaidie kulinda miundombinu ya Mradi.

Nae mhandisi Tadei Kamu alifafanua,mradi huo umefikia asilimia 93 ,kipande cha DaresSalaam-Morogoro Trilioni 2.7.

Wakati huo huo,akiwa mradi wa Daraja WAMI Kunenge alimuelekeza mkandarasi kukamilisha wakati alioomba kuongezwa Tena kwa wakati.

Alisema ,daraja la WAMI la zamani lilijengwa 1959 na ni kiungo kutoka Chalinze kwenda mikoa ya Kaskazini mwa nchi yetu na nchi jirani .

"Daraja hilo halikidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa kuwa lilijengwa miaka mingi iliyopita na ni jembamba lenye njia moja, barabara zinazounganisha daraja hili ziko kwenye miinuko mikali na kona mbaya ambapo ajali mbaya na vifo vimekuwa vikitokea mara kwa mara ,"

"Nimekuja na nyie wote kwakuwa ni timu moja ya mkoa ninayofanya nanyi kazi muone yanayofanyika chini ya serikali yetu ya Rais Samia,na kauli mbiu yetu ni PWANI YA SAMIA TIMU MOJA KAZI IENDELEE"

Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete alisema mradi huo umetengeneza ajira 500 ,za vijana aliishukuru serikali na Rais Samia Suluhu kwa juhudi zake.

Alisema, Daraja jipya likikamilika litakuwa kubwa urefu wa mita 510 na upana wa mita 11.85 linajengwa umbali wa mita 670 pembeni mwa daraja la zamani .

Ridhiwani alieleza ,daraja hili litakuwa na uwezo mkubwa katika usafirishaji na kufungua milango ya kimaendeleo na kukuza uchumi Chalinze na nchi yetu kijumla.

Awali akitoa taarifa ya mradi ,meneja wa TANROADS Pwani ,Andrea Kasamwa ,alisema mradi umefikia asilimia 64 .

Alieleza , Mkandarasi alianza kazi ya Ujenzi 22,octoba 2018 na kutakiwa kukamilisha mradi September 2021 miezi 35 lakini Mkandarasi amewasilisha sababu za kimkataba nyongeza ya muda wa ujenzi kufika 2022.

Kasamwa alieleza, hivi karibuni Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi ,Pro.Makame Mbarawa alimuagiza Mkandarasi Power Construction Corporation Ltd kutoka China.

Alisema ,tayari mkandarasi huyo ameongeza kasi ya kufanya kazi ikiwa ni agizo la waziri huyo kwa kuongeza raslimali watu watumishi kutoka 230 hadi 520 na kasi ya mtambo mara mbili na mafundi wa zamu mchana na usiku .
 
Wanakamatwa baada ya VP kusema? Wahalifu wanaweza kuwa na choice kama tunasubiri orders za wakubwa tu ndio tuchukue hatua
 
Chadema ni janga kwa nchi yetu wanahujumu miradi huku wakiombea wahisani wainyime misaada Tanzania
 
Back
Top Bottom