Putin asisitiza kuendelezwa mashirikiano ya pamoja kati ya Russia na China

jollyman91

Member
Sep 21, 2021
69
29
Rais Vladimir Putin wa Russia amesisitiza kuendelezwa mashirikiano ya pamoja baina ya nchi yake na China.

Putin ametoa sisitizo hilo katika salamu alizomtumia Rais Xi Jinping wa China kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 72 wa kuasisiwa Jamhuri ya Watu wa China.

Katika salamu zake hizo, Rais wa Russia amesema ana uhakika ushirikiano baina ya nchi mbili katika nyanja tofauti utazidi kuimarishwa kwa kila namna itakayowezekana.

Putin amesisitiza kuwa, kuendelea kustawishwa ushirkiano kati ya Russia na China ni kwa manufaa kamili ya nchi mbili na kunaendana na juhudi za kudhamini usalama na uthabiti wa kikanda na ulimwengu mzima.

4bmy73daf75936siu0_800C450.jpg
Rais Vladimir Putin wa Russia (kulia) na Rais Xi Jinping wa China
Rais wa Russia amebainisha kuwa, kwa mtazamo wa uhusiano wa pande mbili, Moscow na Beijing zinafuatilia ushirikishaji wa pande zote na maelewano ya kistratejia.

Baada ya kumalizika enzi za Vita Baridi, kiwango cha uhusiano wa kiuchumi, kisiasa, kijeshi na wa mauzo ya silaha baina ya Russia na China kimezidi kuongezeka na nchi hizo mbili zimekuwa zikifuatilia majimui ya malengo kadhaa kikanda na kimataifa sambamba na kuzingatia masuala ya kisiasa ya kila upande.

Kwa sasa mashirikiano kati ya Russia na China hususan katika nyuga za uchumi na nishati yamefikia kiwango cha juu.../
 
Back
Top Bottom