Putin asema nchi za Magharibi zikiondoa vikwazo Urusi itauza nje chakula na mbolea

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
Rais Putin jana alisema Urusi inapanga kuuza nje chakula na mbolea ili kutoa mchango katika kukabiliana na msukosuko wa chakula duniani, lakini sharti lake ni kuwa nchi za magharibi zitaondoa vikwazo vilivyowekwa kutokana na madhumuni ya kisiasa.

Habari kutoka tovuti ya Ikulu ya Urusi imesema Putin ameongea kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Italia Bw. Mario Draghi, na kujadiliana masuala ya hali ya Ukraine na usalama wa chakula duniani. Putin amesema hakuna msingi wowote katika kuishutumu Urusi juu ya suala la utoaji wa mazao ya kilimo kwenye soko la dunia.

Changamoto ya sasa inahusiana na kutokuwepo utaratibu kwenye sekta mbalimbali na mnyororo wa ugavi duniani, pamoja na sera za fedha za nchi za magharibi kwenye kipindi cha janga la Corona.

Putin ameongeza kuwa Urusi imechukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha usalama wa usafiri baharini, lakini kazi hizo zinazuiliwa na upande wa Ukraine.
 
WanaJf wanaokataa kuumizwa kwa Russia kwa vikwazo wanasema rongo,ila this time si yeye aliyeomba atolewe na sijawahi sikia akiomba viondolewe ila yanakuja hayo kama masharti majinga majinga ya NATO wakienda lia lia kutaka saidiwa shida zao,this time ametoa ayo maneno after kupigiwa simu na PM wa Italy.

Viva Russia, viva Put-in
 

Attachments

  • Screenshot_20220527-070134.png
    Screenshot_20220527-070134.png
    42.6 KB · Views: 29
Warussi wa JF wanasema vikwazo havimtishi Putin,sasa kama ni hivyo kwa nini analia lia wamuondolee? Akae na chakula chake ikiwezekana alishe hadi kunguni wa nyumbani kwake, vikwazo viko pale pale.
Tatizo sio vikwazo vinaiumiza Russia! Tatizo ni vikwazo vinaiumiza dunia na walio viweka! Unamnyima mwenye chakula asiuze wakati wewe huna hicho chakula!
 
Warussi wa JF wanasema vikwazo havimtishi Putin,sasa kama ni hivyo kwa nini analia lia wamuondolee? Akae na chakula chake ikiwezekana alishe hadi kunguni wa nyumbani kwake,vikwazo viko pale pale.
Hahaha, hakuna aliyesema kwamba vikwazo havimuumizi Putin,yeye mwenyewe alisema vinamuumizi Ila Hana jinsi ila kuingua vitani. Pia akasema kwamba,vikwazo vinawaumiza EU kuliko Urusi na kwamba walikuwa wamejiandaa,ndio maana unaona Rubles 🇷🇺 inapaa Sana hata kabla ya vita
 
Warusi wa JF wanasema vikwazo havimtishi Putin, sasa kama ni hivyo kwa nini analia lia wamuondolee? Akae na chakula chake ikiwezekana alishe hadi kunguni wa nyumbani kwake,vikwazo viko pale pale.
Sasa nawewe,Dunia inamlilia naye anawakumbusha mbona Dunia imemtenga?Akimaanisha watatue shida iliyopo kati ya pande hizi mbili sio waone sindano Kwa wengine tamu,ila kwao chungu🤔
 
Tatizo sio vikwazo vinaiumiza Russia! Tatizo ni vikwazo vinaiumiza dunia na walio viweka! Unamnyima mwenye chakula asiuze wakati wewe huna hicho chakula!
Sasa kwanini aanze kulia kuondolewa vikwazo,si atulie ili hao 'wanaoumia na vikwazo' wateseke.Yani huumizwi na vikwazo na hapo hapo unataka vitolewe,vikwazo viko pale pale
 
Hahaha, hakuna aliyesema kwamba vikwazo havimuumizi Putin,yeye mwenyewe alisema vinamuumizi Ila Hana jinsi ila kuingua vitani. Pia akasema kwamba,vikwazo vinawaumiza EU kuliko Urusi na kwamba walikuwa wamejiandaa,ndio maana unaona Rubles inapaa Sana hata kabla ya vita
Vikwazo vinamuumiza Russia ndiyo maana unaona sasa hivi hadi wameamua kutengeneza Azam Cola na Mo Cola.

Rubles inapaa kwenye makaratasi,impact ya Rubles kupaa wewe unaifeel vipi? Nenda Bank ukanunue hizo Rubles utunze kwakuwa zinapaa ndiyo nitajua kweli ina impact kwako.Lakini kama inapaa kwa maneno matupu na wewe huthubutu hata kuinunua ina faida gani sasa. Pesa haivuki mipaka ya Russia ni kama madafu tu ya Mama Samia hapa.
 
Sasa nawewe,Dunia inamlilia naye anawakumbusha mbona Dunia imemtenga?Akimaanisha watatue shida iliyopo kati ya pande hizi mbili sio waone sindano Kwa wengine tamu,ila kwao chungu
Eti Dunia inamlilia au unamaanisha Dunia ya JF
 
Hahaha, hakuna aliyesema kwamba vikwazo havimuumizi Putin,yeye mwenyewe alisema vinamuumizi Ila Hana jinsi ila kuingua vitani. Pia akasema kwamba,vikwazo vinawaumiza EU kuliko Urusi na kwamba walikuwa wamejiandaa,ndio maana unaona Rubles 🇷🇺 inapaa Sana hata kabla ya vita
Embu tafuta Ruble tukanunue madafu hapo Ukonga tule.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom