Mkutano wa viongozi wa CCM kutangaza uzuri wa bajeti ulienda vizuri kwenye viwanja vya Mwembetogwa kuanzia saa kumi jioni hadi ilipotimu saa kumi na mbili jioni pale kada wa zamani wa Chadema aliyehamia CCM Bwana Shaibu Akwilombe alipotoa tuhuma kuwa Chadema inaondeshwa kindugu huku akitaja orodha ya majina katika kupeana vyeo kindugu. Ndipo hapo kada wa Chadema aliyesimama mbali mkutanoni alipotamka kwa sauti; " Mbona humtaji mtoto wa Mwinyi, Husein Mwinyi! Mbona humtaji mtoto wa Karume Zanzibar!". Ndipo hapo purukushani zikaanza mara ile makada wa CCM walipomwendea kada wa Chadema kutaka kumshughulikia kwa kuvuruga mkutano wao. Angalia picha za tukio hilo katika; http://mjengwa.blogspot.com