Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,487
17,682
Punguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.

Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo.

Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezeta-amkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari.

Tafakari, chukua hatua!

-------
Mwananchi (Juni 14)
Punguzo la kodi kwa wafanyakazi kiini macho

Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/14 inaonyesha kuwa wafanyakazi wamepunguziwa kodi katika mishahara yao ingawa punguzo lenyewe linaonekana kama kiini macho.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha, William Mgimwa alisema Serikali imependekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato ili kupunguza kodi hiyo.

Waziri Mgimwa alisema Serikali imepunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 14 hadi 13... "Hatua hii inalenga katika kutoa nafuu ya kodi kwa mfanyakazi."

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, viwango vinavyopendekezwa ni ikiwa mfanyakazi anapata jumla ya mapato yasiyozidi Sh2,040,000 kwa mwaka ambayo ni sawa na Sh170,000 kwa mwezi, kiwango cha kodi ni asilimia 0, kwa maana kwamba hatalipa kodi.

Kwa wafanyakazi wenye mapato ya jumla yanayozidi Sh2,040,000 lakini hayazidi Sh4,320,000 sawa na Sh360,000 kwa mwezi kiwango cha kodi atakachokatwa ni asilimia 13 baada ya malipo ya Mfuko wa Jamii ambayo ni nafuu ya isiyozidi Sh1,540.

Kwa wafanyakazi wenye mapato yanayozidi Sh361,000 kuendelea watapata nafuu ya Sh1,900.

Dk Mgimwa hakuzungumzia suala lolote kuhusu kupandishwa kwa mishahara tofauti na kilio cha Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), ambalo katika sherehe za Mei Mosi, mwaka huu zilizofanyika kitaifa mkoani Mbeya, lilipendekeza kima cha chini cha mshahara kiwe Sh740,000 kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
 
Hivi kweli kwa kuongeza bei ya fuel ndiyo maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa rahisi? Infact kila kitu kitapanda bei. Sasa hizi rasilimali ni za nini kama wananchi hawazifaidi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ni dhihaka hasa.

Nafikiri hatuna haja ya kusubiri kubamizwa marungu kama mabwege wa Mtwara iliyokuwa inaitwa NGOME YA CCM ndio tuamke. Asiyepiga kura 2015 ni ndugu yake na shetani

Mkuu..serikali zote duniani zinatoza PAYE.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado Paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa
 
Chapeni kazi acheni kulia lia, kuna vyama vingi sana vya upinzani viliingia madarakan katika bara la Afrika ukianzia, kenya, burundi, zambia, nigeria, algeria,ghana,n.k lakin maisha ni yale yale , hiko chama chenu kina kitu gan so special kias kwamba kikiingia kitatofautiana na vyama vingine vilivowah kushika dola. Punguzen kulalamika pigen mzigo mbona wengi tu tumeyatoa maisha ndan ya tawala hii hii, mzee ndesa, mbowe na kina mtei mbona wamefanikiwa chin ya sera hizi hizi za CCM!
 
serukamba you
 
Nina wasiswasi na IQ yako huenda inamchanganyiko wa vitu vya ajabu sana
 
Wameshindwa kutanua mianya ya kodi na watz wengi wanahela chafu zisizotokana na kipato halali. Ndo maana hawastuki wakiongezewa kodi za magari, vinywaji n.k. MoF wanafikiri kuongeza kodi ndo kukusanya zaidi wakati watz ndo wanaongeza mbinu za kukwepa kodi.
 
Chapeni kazi acheni kulia lia, kuna vyama vingi sana vya upinzani viliingia madarakan katika bara la Afrika ukianzia, kenya, burundi, zambia, nigeria, algeria,ghana,n.k lakin maisha ni yale yale , hiko chama chenu kina kitu gan so special kias kwamba kikiingia kitatofautiana na vyama vingine vilivowah kushika dola. Punguzen kulalamika pigen mzigo mbona wengi tu tumeyatoa maisha ndan ya tawala hii hii, mzee ndesa, mbowe na kina mtei mbona wamefanikiwa chin ya sera hizi hizi za CCM!

Akili ni mali ya mtu, akiitumia vibaya kwa makusudi au kwa bahati mbaya, basi hana tofauti na dumuzi ambao huharibu mazao ya binadamu ili kujipatia chakula chao kwa umaskini wao.NYERERE ALISOMA NA KUFANIKIWA AKIWA CHINI YA WAKOLONI, KAMA MAWAZO YAKE YANGEKUWA KAMA YA KWAKO, BASI LEO HII SOTE TUNGEKUWA BADO TUANATOBOLEWA MIGUU NA KUFUNGWA MINYORORO NA MABWENYENYE YALE. Tumia akili yako kijana, wizi, utapeli na uzandiki vina mwisho, lakini ukweli na siha njema ni hazina kwa avitumiaye. "You can fool some people sometimes but you can't fool all people all the time" kumbuka hii. “If a man hasn‛t discovered something that he will die for, he isn‛t fit to live.”
Martin Luther King, Jr., Detroit Michigan. June 23,
1963.
 
mkuu..serikali zote duniani zinatoza paye.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa

kwa asiyemfanya kazi kaMa wewe kutoa kauli kama hii ni kawaida...wafanya kazi hawalalamikii kutozwa p.a.y.e bali kiwango kinachotozwa,... unaposema kila nchi inatoza kwa kiwango cha kulalamikiwa mi nilidhani ungekuja na data za jinsi gani nchi zipi zinatoza paye inayolalamikiwa na ambayo ni ndogo au kubwa zaidi ya tanzania....kwa wafanyakazi wa tz tunalipa kodi zaidi ya paye kwani kua vat kwa kila tunacho nunua....kwanini tukamuliwe....?

MAFUTA WAMEONGEZA BEI MFANYA KAZI HUYUHUYU ATAKUWA ANANUNUA MAFUTA HAYO HAYO...HATUJAENDA KWENYE MAGARI...
HOJA YA KUONGEZA BEI KWENYE MAFUTA SERIKALI HAIJATATUA TATIZO BALI LIMEKUWA KWANI VYAKULA NA BIDHAA NYINGINE ZINASAFIRISHWA KWA MAJI...?

HAPA TUTEGEMEE GHARAMNA ZA USAFIRISHAJI KUONGEZEKA HASA VYAKULA NA MWISHI WA SIKU MFUMUKO WA BEI KILA KONA...!!
Think of it before u comment tafadhari.....!!
 
Each year the main focus for revenue boosting is beer and cigarettes..public servants have being conned during May Day celebrations that PAYE will be cut only to hear 1% cut. Moreover what amaze me was to hear cheering and applause from magamba side when it was mention that no duty will be imposed on bodaboda as they believe they will win hearts and minds of the unemployed youth.
 
That's true mkuu,katika budget yote sijaona plans za kupambana na unemployment tofauti na wenzetu ambao youth employment ni sensitive issue

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Chapeni kazi acheni kulia lia, kuna vyama vingi sana vya upinzani viliingia madarakan katika bara la Afrika ukianzia, kenya, burundi, zambia, nigeria, algeria,ghana,n.k lakin maisha ni yale yale , hiko chama chenu kina kitu gan so special kias kwamba kikiingia kitatofautiana na vyama vingine vilivowah kushika dola. Punguzen kulalamika pigen mzigo mbona wengi tu tumeyatoa maisha ndan ya tawala hii hii, mzee ndesa, mbowe na kina mtei mbona wamefanikiwa chin ya sera hizi hizi za CCM!

kwa nini mimi nisistahili msamaha wa kodi? Kwa nini nifanyiwe dhihaka?
1%?
 
Mkuu..serikali zote duniani zinatoza PAYE.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado Paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa

kwa nini wanifanyie dhihaka?
1%? Kweli?
Watoze PAYE sawa sikatai, lakini mbona sioni dhati yoyote ya kupunguza mfumuko wa bei ili niyamudu maishi? Unadhani mfumuko wa bei ungedhibiwa ningelalamika kuwa PAYE ipunguzwe?
 
Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom