tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,810
- 18,241
Punguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.
Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo.
Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezeta-amkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari.
Tafakari, chukua hatua!
-------
Mwananchi (Juni 14)

Punguzo la kodi kwa wafanyakazi kiini macho
Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/14 inaonyesha kuwa wafanyakazi wamepunguziwa kodi katika mishahara yao ingawa punguzo lenyewe linaonekana kama kiini macho.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha, William Mgimwa alisema Serikali imependekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato ili kupunguza kodi hiyo.
Waziri Mgimwa alisema Serikali imepunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 14 hadi 13... "Hatua hii inalenga katika kutoa nafuu ya kodi kwa mfanyakazi."
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, viwango vinavyopendekezwa ni ikiwa mfanyakazi anapata jumla ya mapato yasiyozidi Sh2,040,000 kwa mwaka ambayo ni sawa na Sh170,000 kwa mwezi, kiwango cha kodi ni asilimia 0, kwa maana kwamba hatalipa kodi.
Kwa wafanyakazi wenye mapato ya jumla yanayozidi Sh2,040,000 lakini hayazidi Sh4,320,000 sawa na Sh360,000 kwa mwezi kiwango cha kodi atakachokatwa ni asilimia 13 baada ya malipo ya Mfuko wa Jamii ambayo ni nafuu ya isiyozidi Sh1,540.
Kwa wafanyakazi wenye mapato yanayozidi Sh361,000 kuendelea watapata nafuu ya Sh1,900.
Dk Mgimwa hakuzungumzia suala lolote kuhusu kupandishwa kwa mishahara tofauti na kilio cha Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), ambalo katika sherehe za Mei Mosi, mwaka huu zilizofanyika kitaifa mkoani Mbeya, lilipendekeza kima cha chini cha mshahara kiwe Sh740,000 kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.