Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Chapeni kazi acheni kulia lia, kuna vyama vingi sana vya upinzani viliingia madarakan katika bara la Afrika ukianzia, kenya, burundi, zambia, nigeria, algeria,ghana,n.k lakin maisha ni yale yale , hiko chama chenu kina kitu gan so special kias kwamba kikiingia kitatofautiana na vyama vingine vilivowah kushika dola. Punguzen kulalamika pigen mzigo mbona wengi tu tumeyatoa maisha ndan ya tawala hii hii, mzee ndesa, mbowe na kina mtei mbona wamefanikiwa chin ya sera hizi hizi za CCM!

Kwa mantiki ya maelezo yako haya basi hakuna haja ya kuwa na serikali!
 
Waziri wa fedha ametangaza jedwali jipya la PAYE kwa punguzo la 1%. Naomba aliyefanikiwa kuliona jedwali hilo anisaidie kuliweka hapa. tafadhari sana.
 
15% to 14%! Jk, this is very unfair. Ili sisi wafanyakazi tuone impact ya reduction it should have been reduced to less than 10% hii governance style inatunyonga wengine ili wengine waishi kama wako peponi. Mungu atusaidie hii situation isidumu katika miaka 2 inayokuja
 
Hiyo 1% ni kubwa sana upande wa serikali. Hapo serikali inapoteza mabilioni ambayo inabidi ikayatafute kwenye vyanzo vingine. Ni kweli kuwa hii PAYE sisiw afanyakazi hatuipendi lakini ukiangalia kwa picha kubwa bora wangeongeza hata Kidogo hii PAYE na kupandisha juu kiwango cha msamaha ili serikali ipate uwezo zaidi wa kutuhudumia vizuri .
Absolutly ----! Please be informed kuwa kwa kila Transactions anazozifanya Mfanyakazi wa nchi hii huwa analipa kodi mbali na P.A.Y.E... Mfumuko wa bei unawaumiza sana wafanyakazi, suala la elimu ambalo serikali ilipaswa iligharamie ili watoto wetu wapate elimu bora na si bora elimu linawaumiza sana wafanyakazi ambao wengi wao wanajua umuhimu wa elimu hivyo kulazimika kuwapeleka watoto wao kwenye shule ambazo angalau zinajitahidi kutoa elimu bora lakini kwa gharama kubwa sana...
Badala ya kuendelea kuwaangamiza wasioweza kulipa kodi na kuwaneesha wenye uwe wa kulipa kodi ambao pia ndiyo wakwepa kodi; Serikali sikivu kwa wawekezaji inatakiwa itanue wigo wa kukusanya kodi kwenye meli zinazovua kwenye:-
1. bahari yetu
2. Machimbo ya Dhahabu
3. Machimbo ya Almasi
4. Machimbo ya Nickel
5. Machimbo ya Uranium
6. Udhibiti wa mapato Mt Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Selou, Mikumi nk.
7. Udhibiti wa mapato kwenye Bandari zetu
8. Udhibiti wa mapato kwenye vivuko
9. Udhibiti wa mapato kwenye viwanja vya mipira
10. Kukusanya kodi kikamilifu kwenye hotel za kitalii hususan zile zinazomiliki viwanja vya ndege

.... Tunajua kuwa Bajeti hii inatekeleza matakwa ya IMF, WB na nchi wanazojiita wahisani! Hawa siku zote huwa wanalinda maslahi yao, Ifike mahali CCM wajue kuwa wanatufanyia dhulma kubwa sana sisi WATANZANIA...
 
Inasikitisha na kuuzunisha serekali hii kutotambua vyanzo vipya vya kodi ili kunusuru wafanyakazi na mzigo huu mzito.Utajiuliza ni wananchi wangapi wanaishi nyumba za kupanga na wangapi wanaishi kwenye nyumba zao? Je, kodi za upangaji kwenye makazi yanalipiwa kodi?Madalali wanauza nyumba na kupangisha nyumba wanalipa kodi?Tuishike mikono kwa kuinyima kura kwani haioni na ikiendelea kuongoza bila macho itaangamiza nchi hii
 
Chapeni kazi acheni kulia lia, kuna vyama vingi sana vya upinzani viliingia madarakan katika bara la Afrika ukianzia, kenya, burundi, zambia, nigeria, algeria,ghana,n.k lakin maisha ni yale yale , hiko chama chenu kina kitu gan so special kias kwamba kikiingia kitatofautiana na vyama vingine vilivowah kushika dola. Punguzen kulalamika pigen mzigo mbona wengi tu tumeyatoa maisha ndan ya tawala hii hii, mzee ndesa, mbowe na kina mtei mbona wamefanikiwa chin ya sera hizi hizi za CCM!

kati ya nchi ulizozitaja ni ipi iliyochini ya uchumi wa tanzania!?
 
Kulikuwa na matarajio makubwa kuwa PAYE ingepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu ilikuwa ni ahadi ya Mh Rais mwenyewe aliyoitoa kule Mbeya. Kwa punguzo hili sidhani hata kama kulikuwa na sababu ya kuwatangazia wafanyakazi kuwa PAYE itapungua.
Angalia jedwali hapa chini (mapato ni kwa Mwaka).
Viwango vya Sasa
Viwango vya sasa Jumla ya Mapato
Kiwango cha Kodi
Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi 2,040,000/=
Asilimia sifuri (0%)
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 2,040,000 lakini hayazidi shilingi 4,320,000/=
14% ya kiasi kinachozidi Shilingi 2,040,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 4,320,000/= lakini hayazidi shilingi 6,480,000/=
Shilingi 319,200/= + 20% ya kiasi kinachozidi Shilingi 4,320,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 6,480,000/= lakini hayazidi shilingi 8,640,000/=
Shilingi 751,200/= + 25% ya kiasi kinachozidi Shilingi 6,480,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 8,640,000/=
Shilingi 1,291,200/= + 30% ya kiasi kinachozidi Shilingi 8,640,000/=
Viwango vinavyopendekezwa
Jumla ya Mapato
Kiwango cha Kodi
Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi 2,040,000/=
Asilimia sifuri (0%)
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 2,040,000 lakini hayazidi shilingi 4,320,000/=
13% ya kiasi kinachozidi Shilingi 2,040,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 4,320,000/= lakini hayazidi shilingi 6,480,000/=
Shilingi 296,400/= + 20% ya kiasi kinachozidi Shilingi 4,320,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 6,480,000/= lakini hayazidi shilingi 8,640,000/=
Shilingi 728,400/= + 25% ya kiasi kinachozidi Shilingi 6,480,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 8,640,000/=
Shilingi 1,268,400/= + 30% ya kiasi kinachozidi Shilingi 8,640,000/=
Hapo kwenye bold, ukifanya mahesabu punguzo la kodi ni 0.20%, sawa na 0.002 fraction. Yaani kwa mfano kama kabla ya punguzo ulikuwa unakatwa PAYE ambayo kiwango chake kilikuwa tuseme TShs 1,000,000/=, (million moja, let's say a Professor) kwa mwezi, kwa punguzo hili PAYE hiyo hiyo itapungua kwa 0.002*1,000,000/= ambayo ni sawa na TShs 2,000/= kwa mwezi. Kwa hiyo aliyekuwa analipa PAYE ya shillingi million moja kwa mwezi kwa punguzo hili sasa hivi ataweza kulipa PAYE ya TShs 998,000/=, kwa mwezi, pungufu ya 2,000/= kwa ile PAYE ya mwanzo kabla ya punguzo.
 
Huu ni uhananga wa CCM, asilimia 1, hii ni dhihaka kabisa, wafanyakazi tumevunjika mioyo kabisa na sijui km kuna mtumishi atayefanya kazi kwa moyo, pumbavu zaooooo.
 
Serikali hii eti inajiita "SIKIVU"
Wakati haina macho,masikio maanaimeshindwa
kuona vyanzo vya maana kwenye kodi isipokuwa
Wafanyakazi tu.
 
Each year the main focus for revenue boosting is beer and cigarettes..public servants have being conned during May Day celebrations that PAYE will be cut only to hear 1% cut. Moreover what amaze me was to hear cheering and applause from magamba side when it was mention that no duty will be imposed on bodaboda as they believe they will win hearts and minds of the unemployed youth.
Aftter row most of those bodaboda belongs to them,so they were clapping knowing that they are not going to pay and they will exploit more people.
 
Mkuu..serikali zote duniani zinatoza PAYE.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado Paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa

Mkuu,

Hakuna mtu humu ndani akabisha kuwa serikali zote duniani hazitozi PAYE tatizo la nchi yenu haina mbinu mbadara ya kukusanya kodi na kodi ambayo ni tegemezi kwa kuiendesha serikali hii ni PAYE. sasa unapunguza PAYE 1% huku unaongeza kodi kwenye vitu vingine sasa hapo umefanya nini then Natural resource zote za nchi hatuoni kodi zake kwa manufaa ya Taifa hili hapo huoni ni upuuzi na siasa hizo? Tabaka la kati ndio mimi na wewe twaiongoza nchi hii










 
Baada ya kusikia Hotuba ya Bajeti, nilipatwa na mshituko mkubwa pale waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Fedha Dk William Mgimwa alipotangaza kushuka kwa PAYE kawa asilimia moja kwa mtu ambaye anakipato cha chini ya milioni mbili.

Ndugu yenu nilidhani ni kwa mwezi nikajua ooh tumeula, ila baada ya kutafakari zaidi nikasema hii haiwezekani kabisa serikali hii hii iondoe kodi ya mapato kwa watu wenye kipato chini ya milion mbili? Kumbe ni mwaka.

Kwa utaalamu wangu wa hesabu za darasa la saba na excel nimejaribu kutafuta ni kiasi gani kilichopunguzwa kwa mwezi katika pato la mwezi baada ya hii 1%. Asante sana mwalimu wangu wa darasa la saba ulionifundisha hesabu za Mlinganyo hapa nimetafuta X. Asante sana Mwalimu Onesmo Misanga.

Pia bila hiyana niishukuru kampuni ya microsoft kwa kunisaidia kujumlisha na kutoa bila ya kutumia calculator na ubongo wangu.

Kwa viwango vya sasa na vinavyopendekezwa



VIWANGO CHA SASA
VIWANGO VINAVYOPENDEKEZWA


Jumla ya Mapato kwa mwaka
Kiwango cha Kodi kwa mwaka
Kiwango cha Kodi kwa mwaka
Punguzo kwa mwaka
Punguzo kwa mwezi
Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi 2,040,000/=
Asilimia sifuri (0%)
Asilimia sifuri (0%)


Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 2,040,000 lakini hayazidi shilingi 4,320,000/=
14% ya kiasi kinachozidi Shilingi 2,040,000/=
13% ya kiasi kinachozidi Shilingi 2,040,000/=
max 22,800
max 1,900
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 4,320,000/= lakini hayazidi shilingi 6,480,000/=
Shilingi 319,200/= + 20% ya kiasi kinachozidi Shilingi 4,320,000/=
Shilingi 296,400/= + 20% ya kiasi kinachozidi Shilingi 4,320,000/=
max 22,800.00
max 1,425.00
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 6,480,000/= lakini hayazidi shilingi 8,640,000/=
Shilingi 751,200/= + 25% ya kiasi kinachozidi Shilingi 6,480,000/=
Shilingi 728,400/= + 25% ya kiasi kinachozidi Shilingi 6,480,000/=
15,960.00
1,330.00
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 8,640,000/=
Shilingi 1,291,200/= + 30% ya kiasi kinachozidi Shilingi 8,640,000/=
Shilingi 1,268,400/= + 30% ya kiasi kinachozidi Shilingi 8,640,000/=
15,960.00
1,330.00


Kwa hiyo baada ya mchanganuo hapo juu hebu tuangalie mshahara wa mtu mwenye kipato zaidi ya 8,640,000/=


EXAMPLE
OLD RATES
NEW RATES
assume: mapato kwa mwaka
20,000,000.00
20,000,000.00
less fixed amount
1,291,200.00
1,268,400.00
30% of the remaining
5,612,640.00
5,619,480.00
total tax
6,903,840.00
6,887,880.00
Punguzo kwa mwaka

15,960.00
Punguzo kwa mwezi

1,330.00



Haya sasa kwa wale wa group ya 3

Calculation Grade 3
OLD RATES
NEW RATES
assume: mapato kwa mwaka
4,320,000.00
4,320,000.00
less fixed amount
751,200.00
728,400.00
25% of the remaining
892,200.00
897,900.00
total tax
1,643,400.00
1,626,300.00
Punguzo kwa mwaka

17,100.00
Punguzo kwa mwezi

1,425.00
Calculation Grade 4
OLD RATES
NEW RATES
assume: mapato kwa mwaka
8,640,000.00
8,640,000.00
less fixed amount
1,291,200.00
1,268,400.00
30% of the remaining
2,204,640.00
2,211,480.00
total tax
3,495,840.00
3,479,880.00
Punguzo kwa mwaka

15,960.00
Punguzo kwa mwezi

1,330.00


Kwa hiyo KIMSINGI KWA MWEZI UTAKUWA UNAPATA PUNGUZO LA SH 1330 TU, hata nauli ya siku ya daladala kwenda kazini na kurudi haitoshi



 
Kuitoa CCM pekee haitoshi, lipeni kodi kama inavyotakiwa katika biashara zenu zingine mnazofanya.

Tatizo kubwa lililopo ni serikali (TRA) kushindwa kubuni vyanzo vya kodi na hii nadhani inatokana na watanzania kutokuwa na national IDs. Vitambulisho ni muhimu sana kutrack raia na income zao.

Viwango vya kodi vya Tanzania viko juu, kwa Kenya na Uganda minimum income tax band iko 10pc.
 
Naomba wabunge wetu watusaidie sisi wafanyakazi, kilio chetu sio hiyo asilimia 15% au 14% - la asha ni ile 30% ya kodi wanayokata kwenye mshahara unaozidi 720,000. Asilimia 30% jumulisha hiyo PAYE ni kuua watu. Mbona kuna wafanyabishara wanaopata zaidi ya milioni 2 kwa mwezi lakini hawakatwi kodi ya asilimia 30% ya mshahara? kwanini wafanyakazi wa Tanzania tunaonewa hivyo?
 
Punguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.

Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo.

Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezeta—amkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari.

Tafakari, chukua hatua!

-------
Mwananchi (Juni 14)

Mhm, acha tu
 
Kwa nini misamaha ya kodi ni kwa wawekezaji tu?

cartoons_0225_005.jpg
 
Hivi kweli kwa kuongeza bei ya fuel ndiyo maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa rahisi? Infact kila kitu kitapanda bei. Sasa hizi rasilimali ni za nini kama wananchi hawazifaidi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Kwa maneno mengine, ni afadhali wasingepunguza hiyo P.A Y. E, kuliko kuipunguza na kuongeza kodi lukuki hasa kodi katika mafuta/petrol ambayo itasababisha vitu vyote kupanda. Wametoa pipi kwa mkono mmoja na kuichukua kwa mkono wa pili. Shame on them!
 
Back
Top Bottom