Punguzo la kodi ya ongezeko la thamani toka 20% kuwa 18% walajali tumenufaika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Punguzo la kodi ya ongezeko la thamani toka 20% kuwa 18% walajali tumenufaika?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ndachuwa, Jun 9, 2010.

 1. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Katika makadirio ya serikali ya mwaka 2009/2010 serikali ilishusha kiwango cha kodi ya ongezeko la thamani toka 20% hadi 18%.

  Mimi binafsi sehemu niliyopanga mkataba wa upangishaji unasema kodi ya ofisi inajumuisha kodi ya ongezeko la thamani hivyo pamoja na kiwango cha kodi kupungua, kodi yangu ya mwezi haikupungua.

  Swali, kuna bidhaa yoyote iliyopunguzwa bei kutokana na kiwango cha kodi ya ongezeko la thamani kupunguzwa na serikali?
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ni jambo ambalo nimekuwa nikiliwaza hata mie; mathalani tunahusianishaje punguzo hilo na bei za vitu madukanai na tunapimaje impact ya punguzo kwa hizo bidhaa? bei zinadi kupanda na binafsi sioni kama mtu wa kawaida ananufaika.
   
Loading...