Punguzo la faini kwa bodaboda na bajaji: Serikali imejiridhisha kuwa halitaongeza vurugu na ajali barabarani?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Mwanzo mwanzoni nikiri kuwa nimefuatilia na bado naendelea kuchambua Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kuna jambo, lakini, nimeliona kwa haraka. Ni kuhusu pendekezo la kupunguzwa kwa adhabu kwa makosa ya barabarani kwa waendesha pikipiki almaarufu kama bodaboda na bajaji. Imependekezwa na Waziri wa Fedha jana Bungeni kuwa adhabu kwa kosa moja ipunguzwe kutoka shilingi elfu 30 za sasa hadi shilingi elfu 10.

Pendekezo hili, hakika, lilishangiliwa pakubwa na Wabunge na hata Spika alimtaka Waziri wa Fedha kurudia pendekezo hili na kushangilia kukatamalaki tena Bungeni. Adhabu za barabarani ni sehemu ya kuwarekebisha wamiliki na watumiaji wa vyombo vya usafiri. Ingawa elimu na maonyo hayatumiki sana na askari wa usalama barabarani, adhabu za faini zimekuwa zikitumika zaidi na zimeonyesha mafanikio ya angalau 'kuwatisha' wahusika.

Katika uga wa kisheria, 'kutisha' hutumika kama njia ya kurekebisha na kuzuia wengine kutenda kosa. Ndiyo maana imekuwa kawaida kusikia mahakama ikitamka kuwa 'adhabu hii iwe fundisho kwa wengine...'. Hapo ameadhibiwa mkosaji na kutishwa yeyote anayeelekea kukosa. Kimsingi, adhabu za faini barabarani ingawa wakati mwingine zinatumika vibaya zimepunguza kwa kiasi kikubwa makosa ya barabarani kupitia kutisha kwake.

Je, kupunguzwa kwa faini hizo/ 'vitisho hivyo' kwa watumiaji wa pikipiki na bajaji, hakutachochea makosa ya usalama barabarani na kuleta usumbufu kwa watumiaji wengine wa barababara wakiwemo wenye magari na watembea kwa miguu? Serikali imejiridhisha vya kutosha juu ya jambo hili kabla ya kuja na pendekezo la punguzo hilo la jana ambalo kwa mazingira ya Bungeni linakwenda kupitishwa?
 
Fine za barabarani kwa Tanzania zina lengo la kukusanya mapato hata kama hawasemi hivyo.

Unapompiga mtu fine kwasababu ya ubovu wa gari halafu unaliacha hilo gari barabarani ili likutafutie hiyo fine ya Tsh 30,000 hiyo ni biashara kama biashara nyingine.

Tena fine yenyewe imewekewa Riba, kwamba usipolipa ndani ya siku 7 unawekewa riba, hii ni typical business.

Kama fine ingekuwa ni kwaajili ya usalama barabarani, zuia magari yote mabovu barabarani mpaka pale yatakaporekebishwa.
 
Katika uga wa kisheria, 'kutisha' hutumika kama njia ya kurekebisha na kuzuia wengine kutenda kosa. Ndiyo maana imekuwa kawaida kusikia mahakama ikitamka kuwa 'adhabu hii iwe fundisho kwa wengine...'. Hapo ameadhibiwa mkosaji na kutishwa yeyote anayeelekea kukosa. Kimsingi, adhabu za faini barabarani ingawa wakati mwingine zinatumika vibaya zimepunguza kwa kiasi kikubwa makosa ya barabarani kupitia kutisha kwake.
Nina uhakika Lisu angelikuwepo angetafakari zaidi kabla ya kushangilia. Line yako ya reasoning ni sahihi kabisa.."kutisha" kunasaidia ku deter others from committing the same mistake
 
hili la kushusha adhabu ni msaada kwa wale wanaokosea kwa bahati mbaya, ila hili la kushusha adhabu ni tatizo jingine maana itafika mahala watu wataona ka ni kawaida na hawataogopa tena adhabu maana kiakili itakuwa imejengeka kama ni adhabu ndogo tu, pili swala la kuwaelimisha ambalo linasisitizwa mie naona tunakosea sana na kama tunapendekeza elimu basi tufute hivyo vyuo vinavyowafundisha na badala yake vyombo vya dola na sheria vifanye jukumu hilo. yani mtu akishajua kuendesha tuu aende TRA apate leseni na wasimamizi wa sheria waanze kuwapa hiyo elimu ambayo ilikuwa inatolewaa na vyuo hapo awalii.
Kiufupi hili ni tatizo jingine tunatengenezaa , watu inapaswa kutii sheria kwa kutaka ama pasipo kutaka ili kupunguza hatari zinazotokea ambazo zinatengeneza matatizo mengi kwa watumiaji wa barabara na watumiaji wa vyombo hivyo, pia inachangia uharibifu wa miundombinu ya serikali
 
Fine za barabarani kwa Tanzania zina lengo la kukusanya mapato hata kama hawasemi hivyo.

Unapompiga mtu fine kwasababu ya ubovu wa gari halafu unaliacha hilo gari barabarani ili likutafutie hiyo fine ya Tsh 30,000 hiyo ni biashara kama biashara nyingine.

Tena fine yenyewe imewekewa Riba, kwamba usipolipa ndani ya siku 7 unawekewa riba hiyi ni typical business.

Kama fine ingekuwa ni kwaajili ya usalama barabarani, zuia magari yote mabovu barabarani mpaka pale yatakaporekebishwa.
mkuu usemayo ni sahihi ila niliwahi fuatilia kidogo adhabu za barabarani kwa baadhi ya nchi nyingine, yani ukipigwa faini moja lazima ikuume maana inakuwa kubwa na swala la kuzuia gari kuingia njiani haiwezekani kwa magari yote. ila natumai tutafika tuu
 
Mwanzo mwanzoni nikiri kuwa nimefuatilia na bado naendelea kuchambua Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kuna jambo, lakini, nimeliona kwa haraka. Ni kuhusu pendekezo la kupunguzwa kwa adhabu kwa makosa ya barabarani kwa waendesha pikipiki almaarufu kama bodaboda na bajaji. Imependekezwa na Waziri wa Fedha jana Bungeni kuwa adhabu kwa kosa moja ipunguzwe kutoka shilingi elfu 30 za sasa hadi shilingi elfu 10.

Pendekezo hili, hakika, lilishangiliwa pakubwa na Wabunge na hata Spika alimtaka Waziri wa Fedha kurudia pendekezo hili na kushangilia kukatamalaki tena Bungeni. Adhabu za barabarani ni sehemu ya kuwarekebisha wamiliki na watumiaji wa vyombo vya usafiri. Ingawa elimu na maonyo hayatumiki sana na askari wa usalama barabarani, adhabu za faini zimekuwa zikitumika zaidi na zimeonyesha mafanikio ya angalau 'kuwatisha' wahusika.

Katika uga wa kisheria, 'kutisha' hutumika kama njia ya kurekebisha na kuzuia wengine kutenda kosa. Ndiyo maana imekuwa kawaida kusikia mahakama ikitamka kuwa 'adhabu hii iwe fundisho kwa wengine...'. Hapo ameadhibiwa mkosaji na kutishwa yeyote anayeelekea kukosa. Kimsingi, adhabu za faini barabarani ingawa wakati mwingine zinatumika vibaya zimepunguza kwa kiasi kikubwa makosa ya barabarani kupitia kutisha kwake.

Je, kupunguzwa kwa faini hizo/ 'vitisho hivyo' kwa watumiaji wa pikipiki na bajaji, hakutachochea makosa ya usalama barabarani na kuleta usumbufu kwa watumiaji wengine wa barababara wakiwemo wenye magari na watembea kwa miguu? Serikali imejiridhisha vya kutosha juu ya jambo hili kabla ya kuja na pendekezo la punguzo hilo la jana ambalo kwa mazingira ya Bungeni 0linakwenda kupitishwa?

Itakuwa ni nadharia zaidi kudhani faini barabarani zinapunguza ajali hasa hapa kwetu.

Faini sisi ni mapato ya serikali ambapo si ajabu kusikia askari huwekewa malengo ya idadi ya makosa ya kutoza faini kwa siku. Polisi wenyewe nao wana mgao wao kwa kila kosa ili kuwahamasisha kukusanya zaidi na zaidi. Nia ya kupambana na ajali itoke wapi kwa mitazamo hii?

Haipo nia ya kupambana na ajali bali pana nia ya wazi ya kuvuka malengo ya ukusanyaji.

Mkuu hujawahi kujikuta kwenye kadhia kama hizi:

Hadi pale bajeti ya serikali itakapoacha kuunganishwa na faini zozote kama chanzo cha mapato na pale polisi watakapoondolewa kwenye huu udalali katika faini tungali na Safari ndefu.
 
Back
Top Bottom