Pundamilia apokelewa kwa shangwe kijijini Mara, anapewa heshima kama Mungu

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,211
5,936
Majira ya saa tatu asubuhi, Agosti 2, 2019, katika kijiji cha Rung’abure wilaya ya Serengeti mkoani Mara zilisikika kelele za shangwe mithili ya mapokezi ya kiongozi wa kitaifa.

Hata hivyo yalikuwa ni mapokezi ya mnyama, pundamilia anayesadikiwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati anaingia katika kijiji hicho cha kabila la Wakurya koo ya Nyabhasi (Inchage) inayomaanisha Pundamilia ambaye baadhi yao humpa hadhi kama ya ‘mungu’.

Mnyama huyo au mwingine yeyote wa porini si kawaida kuingia katika makazi ya watu, na kwa pundamilia anafahamika kwa kuwa machachari kwa upigaji mateke lakini aligeuka kuwa mpole baada ya kupewa unga, kuimbiwa nyimbo, kusemewa maneno maalum kwa misingi ya mila yao.

Mwishowe pundamilia huyo akatulia na baadhi ya watu kupiga naye picha na wengine kudiriki kumkalia mgongoni. Ilikuwa kama vile pundamilia huyo alikuwa amefika kwa ndugu zake. Tukio hilo liliwashangaza wahifadhi ambao pamoja na kusomea tabia za wanyama, hawana uwezo wa kumfanya pundamilia kukubali kushikwa mpaka kupandwa juu yake bila kuleta madhara, hata anapofanyiwa matibabu ni mpaka apigwe risasi ya ganzi.

Makorere Maitarya (66) mmoja wa wazee mashuhuri wa kijiji cha Rung’abure alisema punda huyo likuwa anatimiza utabiri wa wazee wa mila wa mwaka 2018 kuhusu ujio wa mgeni mwenye baraka na maendeleo kwa jamii.

Wakati Moses Moroga (69) mkazi wa kijiji cha Nyamirama kata ya Rung’abure akichunga mifugo, ghafla aliona watu wenye mbwa wanaosadikika kutoka kijiji cha Nyamakendo ambao ni koo nyingine wakimfukuza pundamilia ambaye alikimbilia kwenye mifugo yake.

“Aliwaambia wamwache kwa kuwa amefika kwa ndugu zake, kwa kuwa wanajua misingi ya koo zetu, wao wanaabudu tembo (Inchugu) waliondoka huku yeye akimkaribisha kwa maneno mazuri na akitaka kuondoka aelekee mlima wa Kwa Nina, atapokelewa huko,”alisema Moroga.

Moroga ambaye amewahi kuwa katibu wa wazee wa mila aliapiza baadhi ya maneno kwa mnyama huyo, hata hivyo baada ya kukaa kwa muda eneo hilo aliondoka na kuekelea kwenye kilima hicho cha Kwa nina.

Kwa Nina, ni jina la mlima na kitongoji pia, mlima huo wenye msitu mkubwa ambao haukatwi miti, hutumiwa na wazee wa mila wa koo ya Inchage (Pundamilia) kufanyia vikao vya maamuzi mbalimbali yanayohusu jamii yao.

Asili ya msitu huo ulio juu ya mlima ni agizo la hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1975 wakati anapita alishangaa kuona kijiji kizima miti imekatwa na kutaka ufafanuzi wa hali hiyo na maana ya jina Rung’abure akaambiwa uwazi, akaagiza kuanzia siku hiyo wautunze mlima na wasikate miti na kukabidhi wazee wa mila usimamizi, nao walianza kufanyia vikao humo ili kuifanya jamii isipaharibu tena.

Alisema Pundamilia alienda hadi eneo la Nyamemba wanakojenga shule, akasimama na waliomwona ni watoto kama ambavyo ilikuwa imetabiriwa wakatoa taarifa kwa wazazi wao na kuamsha shangwe na nderemo kutoka kwa wanawake.

“Akina mama walifika na unga wakishangilia wakiimba nyimbo zenye ujumbe maalum, huku wazee wakimkaribisha ‘Mungu wao’, ameleta habari njema za amani, maendeleo na umoja na uchaguzi utakuwa wa amani na shule hiyo itakuja kuwa kubwa sana na utabiri wao wa mwaka jana umetimia,”alifafanua.

Alisema kwa kuwa mwaka 2020 ni mwaka unaogawanyika kwa mbili kutakuwa na tohara na ukeketaji. “Tohara ya mwaka kesho itakuwa nzuri maana utabiri umetimia,”alisema huku akisita kuelezea zaidi kuhusu ukeketaji ambao kampeni za kuupiga vita zimeshika kasi kutokana na madhara yake.

Miaka ya 2000 alifika pundamilia dume akakaa kwa muda kijijini hapo, ilikuwa zamu ya jike kama ilivyowahi kutabiriwa na wazee wa mila.

Alisema kwamba hilo ni tukio la sita likiwemo la mwaka 1980, kabla pundamilia hawajafika, wazee wa mila walitabiri na kuonyesha mapokezi yake na walifika nyumbani kwao wanne, madume wawili na majike wawili na wakapokelewa na mama yake.

“Aliwakaribisha ndani akawapa unga baada ya muda akawapeleka kwa mzee wa mila jirani yetu, akawamwagia maziwa na kueleza maneno ya kuwaribisha na kuwashukuru kwa kufika kuwapa ujumbe muhimu, mama alipewa mbuzi na wazee akachinja na kufanya sherehe, baadaye waliondoka na kurudi hifadhini,”alisema.

Mwaka 2013 pundamilia mmoja aliingia Mugumu mjini akiwa amejeruhiwa na watu waliokuwa wakimfukuza ili wamuue, hata hivyo jamii inayotoka koo ya Inchage ilimkingia kifua na kufanikiwa kumpeleka kituo cha Polisi Mugumu na wahifadhi wakamrudisha hifadhini.

Mnanka Nyageko (63) mkazi wa kijiji hicho alisema, “suala hili lina uhusiano mkubwa wa mila na desturi maana sisi ni koo ya pundamilia (Inchage) ambaye babu zao walimtumia kama njia ya kumuomba mambo mbalimbali yaweze kufanikiwa,” alisema.

Nyangeko mmoja wa wazee maarufu kijijini hapo alisema kama angeonyesha tabia tofauti na hizo za upole na upendo ingewapa wakati mgumu wazee wa mila kutafakari tukio hilo na kutafuta namna ya kuepusha.

Alisema ni marufuku kula nyama ya pundamilia huyo hata kumuua, anayebainika kufanya hivyo hutozwa faini ya ng’ombe watano na wazee wa mila na watalazimika kufanya tambiko pasitokee balaa kwake na jamii yake.

Kwa mjibu wa sheria pundamilia ana thamani ya Sh2.6 Milioni, kumuua bila kibali ni kwenda kinyume na Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009 ikisomwa pamoja na marekebisho ya mabadiliko ya sheria Namba 2 ya mwaka 2016 kifungu cha chini ni miaka 20 cha juu miaka 35.

Moses Nyanswi (65) mzee wa mila kutoka kijiji cha Nyamirama alisema alichaguliwa mnyama huyo kutokana na asili yake ya amani, “tunamuita Inchage Kemang’ore (Pundamilia mwenye mistari) ambayo inaashiria amani na upendo,”alisema.

Joseph Meng’anyi alisema pundamilia aliwahi kukaa nyumbani kwao Rung’abure, “Baba alikuwa mhifadhi, alipokaribia kuja likizo ghafla mnyama huyo alikuja nyumbani akawa anaenda kuchunga anarudi, likizo ilipokaribia kwisha naye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.

Eneo hilo palikuwa na nyumba za ovyo ovyo baada ya tukio hilo kumejengwa majumba ya kifahari hiyo ikitokana na maelezo ya wazee wa mila kuwa kila anapopita na kutulia lazima maendeleo yatakuwa makubwa.

Vicent Abely, ofisa wanyamapori alisema pamoja na elimu yake chuoni na kukaa kazini miaka minne hajawahi kuona pundamilia anaimbiwa anatulia kisha anaingizwa ndani ya gari bila vurugu.

“Shukrani ya punda ni mateke, huu msemo umekuwa kinyume kwa wananchi hawa, nilipopigiwa simu kuwa ameingia kijijini niliwaza tutamkamataje ili tumrudishe hifadhini, kwenye gari ataingiaje, lakini nilipofika kwanza nilishangaa alikuwa ametulia wakimpanda mgongoni,”alisema.

Alisema pamoja na kuwa Ngorongoro wanyama wanaishi pamoja na watu hawana uwezo kama ulioonyeshwa na wananchi hao.

Alisema baada ya wananchi kuridhika kukaa naye, walimfunga miguu akiwa ametulia wakampakia ndani ya gari huku wakimuaga kwa shangwe na vifijo na kumrudisha katika Pori la Akiba la Ikorongo.

Chanzo: Mwananchi
 
Inasikitisha nini sasa hapo? Kuwa pundamilia alipofika kwa ndugu zake akatulia? Au unataka hao Wakurya wawe kama Wakenya ambao walimwabudi yule mtu mweupe aliyewadanganya kwamba yeye ni
Yesu?
Imani zetu za kale ni murua kuliko imani za hawa wakoloni/mabeberu.
Alipofika kwa ndugu zake akatulia. Hahahahaaaa.
 
Baadhi ya wakurya wenzangu sijui mpoje yaani bado mnawaondolea watoto wenu utamu
 
Nyerere alikuta mlima umehifadhiwa kimila na miti haikatwi eti na yeye akatoa amri miti isikatwe!!?

Hamziamini akili zenu???
Huu nao ni ujinga uliopitiliza.
 
pic+punda.jpg
 
Inasikitisha nini sasa hapo? Kuwa pundamilia alipofika kwa ndugu zake akatulia? Au unataka hao Wakurya wawe kama Wakenya ambao walimwabudi yule mtu mweupe aliyewadanganya kwamba yeye ni
Yesu?
Imani zetu za kale ni murua kuliko imani za hawa wakoloni/mabeberu.
Imani za kale huku mmevaa jins na suti? Mnatakiwa mfanye hayo maigizo yenu mkiwa uchi
 
Back
Top Bottom