Punda ambwaga bosi wake na kumvunja mguu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Punda ambwaga bosi wake na kumvunja mguu

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jul 16, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  15th July 2009  Mkulima mmoja wa kijiji cha Mapango Wilayani Kondoa, amejeruhiwa vibaya baada ya punda wake kumbwaga chini.
  Sasa mtu huyo aitwaye Ramia Husseni, 29, amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili, MOI.
  Akiongea akiwa wodini, Bw. Ramia amesema tukio hilo alikumbana nalo wiki iliyopita wakati akitoka shambani kwake kuvuna mahindi.
  Akasema siku hiyo baada ya kuvuna mahindi mengi shambani kwake, alimchukua punda wake aliyefungiwa mkokoteni kwa ajili ya kusafirisha mahindi hayo hadi kijijini kwake.
  Akasema baada ya kuhakikisha mahindi yote yamepakiwa kwenye mkokoteni huo, alimpanda punda wake na kumwamrisha kuondoka eneo hilo.
  "Kutokana na kijiji ninachoishi kuwa mbali na shambani, nilimuongoza punda kukimbia kwa kasi ili giza lisiingie nikiwa huko, lakini nikiwa katika mwendo huo, ghafla alinibwaga chini’’ akasema Bw. Ramia.
  Anasema pamoja na kuanguka chini, punda huyo aliendelea kukimbia kwa kasi hiyo hiyo huku akimburuza chini na kusababisha avunjike mguu wake wa kushoto.
  "Punda aliniburuza kwa muda mrefu kwani hapakuwa na mtu wa kumsimamisha, lakini baadaye punda alisimama baada ya kukosa mtu wa kumuongoza," akasema .
  Afisa Uhusiano wa MOI, Bw. Almas Jumaa amesema mgonjwa huyo alifikishwa hapo jana akitokea Hosptali ya Mkoa wa Dodoma.
  Amesema tayari madaktari wameanza kumpatia matibabu ya kunyoosha mguu wake kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha mfupa uliovunjika.
  :: IPPMEDIA
   
 2. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Inabidi tuwe makini sana na mifugo yetu
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  TAtizo kubwa ni hao madaktari wetu ,wasije wakamfanyia operesheni ya kichwa ,nakumbuka zamani ukivunjika mguu ,unakuta unavalishwa POP na mambo na watu wanapoa ,sasa siku hizi ukivunjika basi ujue kinachofuata ni operesheni ,hata hivyo naona serikali ya Tanzania imeangushwa chini ila wananchi wanakwenda mbio sasa ikifika siku wakasimama ,sijui itakuwaje ?
   
 4. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35

  Hili nalo ni tangazo au!
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  shukrani za punda...!
   
Loading...