Pumzika kwa amani shujaa wetu Philbert Kajuna

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
273b85a8-8fa0-4c94-a8d3-e658a143a40e.jpg

KAJUNA'S SHORT HISTORY

Bwana Yesu asifiwe sana wana!

Natumaini mko poa sana,

Najua kuna mtu atasaidika, na hata kama sio leo, bhasi kwa wakati ujao...

Nipende kuwashirikisha mambo machache kama Bwana atakavyoniwezesha, kuhusu maisha yangu binafsi kama sehemu ya ratiba yetu ya leo.. *stadi za maisha*

*MAISHA YA DAR!*

HISTORIA:

Nilizaliwa mwaka 1994, Bukoba, nikakulia huko mpaka 2012 nilipomaliza f.4 nikahamia mwanza wakati nikisubiri matokeo, kisha nikaja dar 2013 kuja kuanza chuo... diploma.

Baba yangu alishafariki tangu 2000 na hivyo sijafanikiwa kulelewa na baba wala mama kwani nimekulia kwa shangazi. *Shangazi alinifundisha kufanya kazi na kuishi maisha ya kijamaa*

Nilipomaliza kidato cha nne nilipelekwa Mwanza ambako ilibidi nianze maisha ya kujitegemea kwa kufanya kazi za kusaidia mafundi ujenzi, hapa ndipo nilianza kukutana na joto la maisha..

Nilifika dar mwaka 2013 ili kuanza chuo DIT, nilikuwa sponsored na serikali (kwa kutoka moja kwa moja skuli kuja kuanza)... Namshukuru Mungu sikuwa natakiwa kulipa hela nyingi sana so Familia ikawa inachanga changa kulipia Ada, na hela kidogo ya matumizi, walau 10k kwa wiki 2.. Baada ya hapo hali ikaanza kubadilika na hivyo nikawa napatiwa ada tu mengine ntajua mwenyewe.

Mwaka mmoja wa kufanya kazi kama kibarua kusaidia mafundi ndio ulinifanya niwaze kujichanganya nikawa naona aibu kuomba hela nyumbani zaidi ya Ada. So likizo ya kwanza kabisa nilikataa kurudi nyumbani na hawakujua niko wapi.. nikawa nimeenda kujenga nipate hela na nisilishwe tena nyumbani...

Personally, Kulingana na maisha niliyopitia...,
1. Nilianza kuchukia maisha ya utegemezi, kulishwa, n.k... kuna namna yana shidazake hasa kama familia yako sio ya kishua sana.. na hata kama ni ya kishua bado sio nzuri saaana.
2. Niliazimia kupambana hata kama mambo ni magumu, hamna kurudi nyuma.
3. Nilikusudia kuoa mwaka huu, 2019..

Naendelea...

KATIKATI HAPO KATIKA KUJICHANGANYA MJINI NIKAJIKUTA NIMEINGIA KWENYE MAHUSIANO!, ... Sio mbaya kuwa kwenye mahusiano, ila hakikisha umejipanga *kiuchumi*. Hata mimi nilikuwa naamini mapenzi yanaweza kuwepo bila hata hela, ila kwa sasa naweza kusema, *Kwa sisi wanaume, Pesa ni muhimu sana katika haya mambo... hata kama atakwambia anakupenda ulivyo..*

Baadae niliondoka chuo nikawa naishi kanisani CCC-Upanga ambapo niliishi kwa kipindi cha miaka miwili, nilikuwa naishi *store* tu baada ya kusema *nyumbani sirudi lazima nitoboe hapa mjini.* Ndugu nilikuwa nao ambao wangeweza kuniweka ila sikwenda, na hata kwa marafiki sikwenda, nilikaa tu pale na hapo kila siku nilikuwa naamka nawaza naishije nakulaje, then natafuta kazi nafanya nakula.
- Nilifagia, nilihamishia watu vitu, na kazi nyingine nyingi ndogo ndogo sana ili mradi nisiombe hela kwa mtu.... kwa kweli maisha yalikuwa ya chini ila yalinipa wakati mzuri sana wa kuona mbele

*Mke wangu alinikuta naishi STORE kanisani, ila nlikuwa najilisha, najivalisha, nmenunua godoro na jiko.. hahaha.. nafanya huduma na mengine mengi.* hata kama sikuwa nimeajiriwa ila ile kukosa hela ndo kulikuwa kunanifanya niwaze nafanya nini niishi..

Wakati huu nilikuwa chuo mwaka wa tatu..

SITASAHAU HILI,

Kanisani huwa kinapikwa chakula ili washirika wote wale, so nlikuwa kila jumapili naweka chakula cha jioni na cha kesho asubuhi..
Siku hiyo nilichelewa kuchukua nikakuta umebaki ukoko, so kwa sababu nlikuwa sijala nikasema lazima nichukue tu.. So wakati nimefuata chombo nije kuchukua chakula niliporudi nikakuta mtoto mmoja katumwa na mzazi wake abebe ukoko kwa ajili ya nguruwe. Nlipofika akaniambia nililia pembeni, nikasema sitakula tena ukoko. Nikamwambia Mungu, imetosha sasa maisha haya., kesho yake mtu akaniletea hela nikaenda kununua vyakula vyote city mall nianze kula vizuri.

Nilimaliza chuo mwezi wa saba, nikawa najitolea kusaidiana na mafundi wa AC DIT, mpaka mwezi wa kumi ambapo nilipata kazi ya kwanza. Na siku natoka kusaini mkataba wa kwanza nikakuta agizo kwa walinzi kwamba sitakiwi kuonekana tena pale.,

Kuna mdada mmoja hivi, huwa namuita Mama. Alifanya muamala fulani hivi, nikajua ni Bwana kamsukuma.. maana si mara nyingi nilikuwa nikiwaambia watu hali yangu..

huyu ni mke wa Gwamaka kwa sasa, wakati huo walikuwa katika uchumba

Kwa mimi,
Nilikutana na mke wangu, mwaka 2016 mwishoni ambapo tulikutana tu sehemu.. hatukuwa na mawasiliano kabla zaidi ya kuona posts facebook.. then mwaka 2017 february tukakutana tena mahali, tukawa tunawasiliana kidogo kidogo.. mwezi wa nne tukakutana vizuri sasa. Mwezi wa tano tukawa tumeanza mahusiano tu na mwezi huo huo nikawa nishampanga kwamba nitamuoa mwaka huu, 2019 mwezi wa 10.. so tumeangukia Dec..,

Alinikuta naishi store, alikuwa anajua na aliwahi kuja pale kama mara 2 alipokuwa akifika CCC...

SIJAWEZA KUSEMA YOTE, ILA KI UFUPI NIPENDE KUSEMA MAMBO KADHAA MUHIMU,

1. Tangu nimefika dar, nimetulia sehemu moja, CCC- Upanga na hapo ndipo niliposema patakuwa nyumbani. Mwanzoni hakuwa ananifahamu mtu na ilikuwa changamoto sana. Kwa wale ambao wamewahi kuja CCC na kujikuta yatima, kwa kweli haijaanza leo ila itaisha. Nikaamua kuji establish hapa dar, so na maombi yangu yalikuwa niendelee kuwepo, na hata kwenye kutafuta kazi nlikuwa natafuta hapa hapa. .. *Kuna faida ya kuwa sehemu moja ukaeleweka*

2. Nilipata ugumu kupata marafiki hasa kwa kipindi kile ambacho hali yangu ilikuwa ya chini hata sieleweki, ila kupitia *kutumika* nimepata watu wengi, na hata wale ambao pengine wanaonekana hawafikiki. Kama ni kujipendekeza kuna kipindi nilijipendekeza, kwa watu ambao sasa hivi ndio wamekuwa wazazi wangu, familia yangu n.k

Dr. Charles Sokile aliniambia, sio rahisi kuvunja circles za watu hasa kama hawakujui, so lazima ujitoe kufanya kitu ili kujenga mahusiano. *Ukifika mahali kwenye watu wengi ukajikuta hamna watu hata wanakusogelea, kama ni mahali ambapo umeamua kuwa, bhasi jichanganye na watu, usisubiri wakufuate, nenda wewe.*

3. KUFANYA KAZI.

Jamani, fursa huwa zinawakuta wanaojichangamsha kufanya kazi. Halafu fursa ziko kwa watu.

Kuna kipindi hata mimi mwenyewe nilikuwa najiona navyodharaulika.. Kuna watu walikuwa wakini dharau hata kipindi ambacho nilikuwa kwenye mahusiano na mpenzi wangu alikuwa akichukia sana. Nilimwambia kwamba, *"Heshima hailazimishwi. Unaweza kumfanya mtu akuogope ila asikuheshimu. Unaweza kumfanya mtu akawa mnafiki kwako ila asikuheshimu; ila kadiri mtu anavyozidi kuelewa wewe ni nani, umebeba nini.. Heshima huwa inakuja tu, halafu unaona mtu anaanza kubadilika mwenyewe taratibu."* #Majira

4. Kuumia katika maisha kupo, ila kuna wakati yataisha.. Kuna vipindi vya kuumia ila kuna wakati huwa vinaisha tusikate tamaa jamani.

KAMA UKO MAHALI UNAFANYA KITU NA UNAONA KAMA HAWAKIONI, HUONEKANI, WANAKUCHUKULIA POA.. Endelea, kuna wakati utaona mabadiliko. Sio kukimbia kimbia

*5. TUSIPENDE MAISHA YA KUIGA GUYS!*

Sikatai kwamba tunatakiwa kuonekana vizuri, kuvaa vizuri, kukaa nyumba kali, na vitu vingine kama hivyo.. ila wengi huwa tunafanya kutokana na marafiki na watu wanaotuzunguka.

Kuna mama mmoja kanisani kwetu nilienda kumtembelea yeye na mumewe akawa ananiambia...

"Mwanangu, ngoja nikupe siri ya maisha, mimi na mume wangu tulioana tukiwa tumepanga chumba kimoja.. ila sasa tuna nyumba 14 hapa mjini(sio vyumba NI NYUMBA14) Ila ukituona huwezi kujua kama ndo iko hivyo kwa sababu huwa tunaishi tunavyotaka na sio watu wanavyotaka.."

Kwanza nilitiwa moyo kwamba hata kama mwanzo ni mdogo ila kutoboa kupo...
Ila pili kuishi maisha ya kawaida ili ufanye vitu vya msingi na kutimiza malengo yako ni kitu cha kawaida sana.

Moja kati ya vitu ambavyo sijabadilika tangu nimekuja mjini nahisi ni katika kutumia pesa. Sifanyagi vitu ili nionekane, ila navitumia vichache nilivyo navyo kama mwenye akili.

Nimekuwa halisi sana katika eneo hili na mpenzi wangu tunaelewana hapa, so tunaenda njia moja na ananisaidia zaidi kuwa na bajeti nzuri zaidi.

HATA KAMA UNA MPENZI WAKO HUKO, MZOESHE KUISHI KWA BAJETI. KUWA HALISI. SIO MTOKO MNA SPEND LAKI HALAFU UNATOKA UMEBAKI MANYOYA UNAENDA KUNYWA MAJI ULALE

Tumia hela vizuri katika nguo, kula, safari n.k

Siku moja nikawa najiuliza... mtu analipwa 400k tena hana familia analia weee, wakati kuna mtu analipwa 100k ana watoto na maisha yanaenda

KUMBUKA, *Kwa mtu asiye na mipango hakuna kinachotosha, kila kitu ni kichache, ila kama una mipango yako, kidogo kinatosha kabisa kuanzia.*

Be real,

*Kama una kidogo kitumie vizuri, wakati unatafuta kingi.*

Penda kujifunza

Wengine wang'ang'anie tu watakupa vitu

Kuwa karibu na watu ujifunze

MTUMIKIE MUNGU KWA NGUVU ZAKO ZOTE, MOYO WAKO WOTE NA AKILI ZAKO ZOTE...

Naomba niishie hapo..
Kama una swali utauliza. Baadae kidogo nitajibu...,

Kubali kufundishika

Majibu:

*Kufika kwenye ndoa bila kuonja onja inawezekana na ni muhimu sana!*

Hata kama unahisi uko kiroho zaidi ya Roho mwenyewe, usijiweke katika mazingira ya hatari ukihisi utakuwa salama...

Don't entertain anything in your mind ambacho hutaki kukifanya nje

Unaweza kukwepa mimba, ukakwepa ugonjwa, usikamatwe, ILA UTUKUFU WA MUNGU UTAONDOKA TU

Kuna vitu vingine ni vya kawaida, unaweza kudhani hata havina shida... mkaanza romance romance ukihisi wewe uko kiroho sana na imara kama "Chapa Simba" ila UHARIBIFU HUWA UNAKUJA TARATIBU SAANA NA HUTAJUA NI LINI UMEKUMALIZA

Kitu nilichogundua, mwili unaweza kunidhamishwa/Dicplened ... ila ukiuacha utazingua sana

Wewe ni mwanaume tu kwenye kila eneo; Hakikisha unakuwa kiongozi kwa mpenzi wako kumsaidia asikosee na sio kutumia udhaifu wake kumla. Anaweza kuyumba kihisia,sasa na wewe kama ndo ulikuwa umesubiria huo ufa, fasta tu unakula vitu....

Mlinde na mlindie Heshima yake kwa kuhakikisha mnautunza utakatifu...

Na sisi wanaume tunavyokuwaga na nyege macho yakishapagawa, mpaka unahisi siku ukifika pale unapotamani utang'ang'ania hapo kama sumaku.. hahahaha. Hata sio hivyo guys. Ukishindwa kuwa na nidhamu sasa hata mbele yatakushinda tu

Ukishaoa unagundua kuwa macho hayatosheki na unaye mmoja... Na wengine weeeengi wanaovutia hawaishi.

Ni wanaume tu wanaweza kufanya maamuzi ya kubaki katika maamuzi waliyofanya. Wavulana lazima wataendelea kupepesa macho

R. I. P
Brother Philibert M. Kajuna
#Your Legacy is Living
#Not with us physically but you gave us this still helpfully to us now and tomorrow
 
Ukisikia kutafutiana maneno ndio huku..
Ukihoji kwa nn yy pekee kati ya 5/6 ni shujaa waweza ushukiwe km mwewee.....Kwa mwemvuli wa 'ni Masuala ya huzuni/matatizo' uonekane juha huna ubinadamu.

Anyway..
R.I.P kwa Marehemu wote na poleni wafiwa....
Pole tena kwa mtoa mada.
 
Poleni sana, kuna mtu alikushauri ungepost kwenye ule uzi wa taarifa za msiba. Sasa kila siku unamfungulia mmoja mmoja uzi wake bila maelezo, hauoni ambao hawajui kilichotokea unawaacha hewani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIP!

Nini kimempata huyu bwana?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom