Pumzika kwa amani Father Privatus Karugendo

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Huwa sijajua hadi leo kati ya tabia na mazoea ni kipi kilimtangulia mwenzake. Kwenye makuzi yangu nilikua katika mazingira ya usomaji kwa kuwa baba yangu ni mpenzi msomaji wa vitabu pamoja na maandiko mbalimbali. Alikuwa ni msomaji wa gazeti la Rai Mwema ambalo lilikuwa likitoka kila alhamisi lakini kutokana na miundombinu ya kipindi kile kufika hadi nyumbani iliweza kufika Ijumaa au Jumamosi.

Ilikuwa likifika Bukoba mjini baba analiagiza watu wa daladala za kuja nyumbani na mimi mara nyingi ndio nilienda kulipokea.
Nikiwa tu shule ya msingi niliweza kusoma mawazo ya waandishi kama wakina Maggid, Jenerali Ulimwengu pamoja na Padri Privatus Karugendo.

Leo hii asubuhi nimesikitika sana kuona mwandishi gwiji Privatus Karugendo katutoka na hayupo nasi tena. Nilimsoma nikiwa bado kinda hata ukubwani nimemsoma kwenye magazeti ya Raia mwema, Tanzania daima na Mwanahalisi.

Kwetu wapenzi wasomaji huu ni msiba mkubwa na tumepoteza maestro katika taaluma ya uandishi.Alikuwa na uwezo wa kutengeneza sanamu na katika maandishi yake akakuaminisha ni binadamu na mwishowe ukakubaliana naye.

Binafsi mlimwengu mimi nakuombea mapumziko mema ya milele na kwangu utabaki kuwa mwandishi gwiji wa kusimamia kile ulichokiamini kwa kutumia bongo yako na kalamu yako.

Rest in peace Padri P. Karugendo

#mlimwengumimi
 
Ulale salama, kaka, rafiki na jirani yangu wa karibu. Kazi umeimaliza ingawa kwa makonakona ambavyo wenzio waliamua kuwa wanafiki wewe ukawa muwazi na ukaruhusiwa kuoa.

Nitakukumbuka daima kaka yangu na mtakutana na school mate wako cha pombe magu huko. Mwambie Hi ila wengine tumeshamsahau tunasubiri neema toka kwa mama.

Unajua tangu tupate uhuru kwetu hatuna barabara na ndo zone inayozalisha kahawa na ndizi kibao. Tuliingizwa organic crops. Mweleze baba Mungu atukumbuke.
 
Pole sana Mohamed. Nami namlilia Padri Privatus Kalugendo. Mwandishi, mchambuzi aliyejenga hoja na kukuvutia msomaji hatimaye akakubaliana naye.

Hawa wakina Privatus Kalugendo kizazi cha wasomi kutoka Wilaya ya Bukoba(ya zamani) waliosoma na kukuzwa kwa namna ambayo inatia tafakuri sana.

Ilikuwaje Bukoba ya zamani alitoa watu wenye fikra kubwa na zakujitegemea kifikra?. Jenerali Ulimwengu, John Kiimbira, Privatus na Prudence Karugendo, Prof Baregu, Prof Anna Tibaijuka, Stan Katabalo, wengineo.

RCC ya Kagera ikae na kuja na azimio na kuweka kumbukumbu za kizazi hiki. Vizazi vijavyo vitakuwa na rejea yenye kujivunia

Tangulia Privarus Karugendo.
 
Kuna watu wakifa lazima mtu usikitike kama huyu nguli Privatus Karugendo lakini kuna midude mingine ikitangulia huko kwa shetani unaweza furahi hadi kunywa mvinyo wa maana kuisifu kazi ya Mwenyezi Mungu kama ilivyokuwa kwa bwana misifa.
 
Gazeti la RAI kila Alhamisi lazima Baba Yangu anunue miaka iyo ya nyuma. Iliniazimu kupenda makala za waandishi wawili tu
A. Padri Karugendo
B. Mzee Ulimwengu

Pumzika kwa Amani Mzee wetu Padri Karugendo.
 
Hii imetutokea wengi. Miaka ya Olevel Babu yangu alikuwa msomaji sana. Alikuwa akinunua hili akilipiga na mimi naanza kulidoea. Nilipenda sana makala za Karugendo na Mihangwa.
 
Back
Top Bottom