PUFDEA: Ni upatu au nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PUFDEA: Ni upatu au nini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mpendanchi-2, Apr 9, 2009.

 1. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna mchezo mwingine unaitwa PUFDEA ofisi zao zipo pale Manzese Tip Top oposite na Post Bank jengo linaitwa Usangi House barabara ya Morogoro kushoto kama unakwenda Moro. Wanajitangaza kwenye vyombo vyote vya redio na TV kuwa wanasaidia kutoa mikopo isiyo na riba na kutoa misaada ya pesa za kujenga shule, na kutoa ajira, kusomesha watoto hadi Chuo kikuu n.k.

  Nimefanya juhudi za kufika na kuongea nao, inaonekana kama jamii ya Upatu kwani ukifika pale unaambiwa kwanza nunua FORM ( 2000) single page, Pili utalipa kiingilio 300,000/- then kama ni mwanafunzi atasaidiwa kusoma hadi chuo kikuu. Nikauliza kama kuna watu wameanza waliniambia wanasubiri wawe wengi, that was last year 2008 by August. Nimekwenda tena last month baada ya kusikia bado wanaendelea kutangaza, wanazidi kufungua branches mikoani na kukusanya pesa za watu, but No one ameshapewa hizo pesa.

  Mikoani wanawambia wananchi wanawasomesha kwa wiki mbili , then wanawapa ajira za kuelimisha wengine wajiunge, na wanawambia ili wasome hiyo course ya wiki mbili walipe ada ya 540,000/=

  Miongoni mwa wamilki wa hiyo PUFDEA ni watu kutoka Uganda.


  Kama kuna aliyepata kufaidika naomba atuambie hapa ili tumwulize maswali ya msingi na tushawishi wengine kujiunga.


  SWALI HAPA:

  Kwa nini vyombo vya dola vinaanza kufuatilia baada ya watu kuibiwa? Na kwa nini wakati mchezo unaanza tu wasifuatilie? Au kuna wakubwa wapo behind? Najua if you are an intellegent people trained to do so, You MUST be aware of what is going on katika society zetu. Na kwa kuwa tunaishi nao hawa watu ni dhahiri wanajua haya.
   
 2. apakati

  apakati Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kosa letu kubwa ni kupenda kumsikiliza mpitanjia. Umekwenda huko manzese mara mbili, hujaweza kupata uhakika wanafanyanini hasa, unataka kuskia toka kwetu. Makosa. Ulitakiwa usimame kidete wakwambie wanafanyaje na unafaidikaje. Km hukua na muda nakushauri uende tena. Jua undani wa kitu kabla hujaja kuweka katika kadamnasi. Umehitimisha NO ONE ameshafaidika bado unauliza km kati yetu kuna anaefaidika, inawezekanaje. Pia, mkopo bila riba si upatu. Kiingilio si lazima upatu hata mabenki yakuwa na viingilio vikubwa tu vya huduma zao (uliza nbc/crdb internet banking kujiunga ni pesa). Kuweka 'WAGANDA' ni kutaka kutahadharisha, haipendezi kujenga dhana za wasio watz ni walaghai. Hatutaweza kuwa watz peke yetu nchini.

  HITIMISHO: rudi kwao na uje na habari kamili, ustegemee wachangiaji. Hata saccoss ikianza leo itangojea watu wengi waweke ndio wengine wakope.
   
 3. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Unaweza kuwa umechangia kitu bila kuelewa ujumbe wa taarifa nzima, unapochangia sometimes tulia then soma tangu heading , Heading inauliza ili wengine ambao nao wamefika na kuijua hii kitu watoe mawazo yao. Haina maana kuandika hapa kidogo kwamba sijafanya uchunguzi wa kutosha la hasha, ila natoa nafasi na wengine wafanye ndipo tuweke Conclussion, ndiyo maana nimetoa Adress ya ofisi ilipo kukupa uwezo na wewe kwenda na kuja na mawazo yako. Kwenye mjadala usipende kufikiri Conclussion on behalf of others.

  Kutoona wachangiaji doesnt mean watu hawasomi na kupata ujumbe, some they have to go and see by themselves ndipo watakuja na hoja.
   
 4. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna POWERCLUB,TUMAINI same SCHEME??
   
 5. Mnhenwa Ndege

  Mnhenwa Ndege JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mpe huyo bwana ukweli, pia lugha anayotumia huyo bwana si nzuri.
   
 6. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Uchunguzi unaonesha hii PUFDEA nayo ni Kampuni imesajiriwa BRELA na ni Company Limited by Shares, maana yake ina wakurugenzi wake. Hivyo kinachofanyika hakina tofauti na DECI, na hii pia baadhi ya Makanisa yameingia share ili kupata waumini. Mojawapo ni Kanisa la Mama Lwakatare Mikocheni B , ambaye anahimiza waumini kuingia huko na kuwaeleza kuwa watapata faida sana . Mikoani nako wanaingia kwa kupitia baadhi ya wachungaji. Na hii ni kwa sababu wachungaji wanaonekana kuwa na kishawishi kwa waumini.

  Sasa: Hivi vyombo vya Dola vinasubiri watu wengi wakishaingia ndipo vianze uchunguzi!!!!??? Kwa nini wasianze na hizi zinazochipukia ili Watanzania wanaowatumikia wasipate hasara!!?? Sipati jibu na Sirikali hiiiii
   
 7. a

  ashikudire New Member

  #7
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua sisi waafrika tunatakiwa tufanye juhudi za ziada ili kujitoa katika umaskini uliokidhiri. Inavyoonekana hakuna kiongozi anaeingia madarakani kwa nia ya kusaidia au kujitoa kwa moyo kuona watu wanajitoka kwenye umaskini. Hii ni hali ya hatari na inayofanya wafrika wengi kuishi maisha magumu kupindukia.

  Viongozi wa Tz wako kujikusanyia mali wao na vizazi vyao kama vitano mbele there is no way mtu wa namna hii akakumbuka kwamba Muhimbili na hosp. nyingine hazina vifaa vya kutosha, wako watu hawajui watakula nini kesho au hata wakiumwa watatibiwa wapi' inasikitisha sana. Kwa namna hiyo hiyo serikali haiwezi kufuatilia mambo kama haya ya deci mpaka inataka kuleta hasara kwa wananchi na kuwaua kwa presure. Kama tutaingia madarakani kwa mtindo wa kujikusanyia mali na si kuwajibika tujue kwamba kila mtu atavuna alichopanda, mali tunazokusanya kwa kutokuwajibika zitatutokea puani siku moja, viongozi ninyi mnaweza kuwa salama kwa kipindi kifupi lakini mnaweza kuwaachia watoto au vizazi vyenu shida mambo hayatakuwa shwari kwenu siku zote mjue hilo acheni kujisahau na kuopna watized ni wajinga hawawezi kufanya lolote. Nawaambia ya kwamba iko siku mtajutia ulafi na roho zenu mbaya zisizo na huruma kwa watu wengine. Naona mnajiona ninyi ni miungu kuna hatari kubwa mbele yenu. Iko siku kilio hichi cha wananchi kitafika mbele za Mungu na atajibu tu Mungu si dhalimu kuwaacha wala hajalala usingizi na hamjamtia upofu kwa ujanja wenu kama aliwajibu waisraeli kule misri atajibu hata TZ.

  Mmetufikisha pabaya sana kiasi cha kushindwa kijizuia........
   
 8. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Niliandika hapa JF kuomba msaada tarehe 31 Jan 2009 kuhusiana na Peoples Unity For Development In Africa.
  Niliomba kujua habari za shirika hili.
  lilofungua ofisi mikoani mf Kagera Bukoba mjini kwenye majengo ya bohari ya mkoa inaitwa Peoples Unity for Development in Africa. Hawa jamaa wanasema hii ni NGO inakuwa funded na Global network USA. Wanasema inatoa misaada ya kulipia watu karo. Kiwango ni Tsh 570,000 kwa term wale wa primary na 980,000 kwa wale wa sekondari. Sharti ni kuwa mzazi amchangie kila mtoto Tsh 60000 sasa na mtoto ataanza kulipiwa fedha shuleni kuanzia July. Wale wa vyuo na vyuo vikuu watalipiwa Tsh 2,640,000 kwa muhula.
  Pia watatoa msaada wa kujenga majumba wa Tsh 6000000 kwa mtu atakayelipia kiingilio cha Tsh 400000. Wenye mashule watapewa Tsh 46,000,000. ikiwa wanalipa kiingilio cha laki sita. Fedha yote wanayotoa si mkopo. Mwanfunzi atakayebahatika kuingizwa katika mpango huu ataendelea kulipiwa kwa miaka 20.
  Bronchure yao inasema ofisi zao kuu zipo Tip Top Manzese, Morogoro Rd Usangi House ghorofa ya kwanza. Pia wana matawi Temeke Changombe Rd karibu na shule ya sekoondari Kibasila phone 0787 706802, Ilala Bungoni msaada garage phone 075 222625 , Morogoro ccm house phone 0755 075901.

  Watu Bukoba wameanza kumininika kwa wingi kulipa hivyo viingilio ili wasipitwe na bahati hii ya mtende.

  Naomba msaada kujua kama hii ni genuine organisation au kuna mtu anajaribu kutafuta karo ya watoto wake? Huko USA kuna hiyo orgnisation inayosaidia katika capacity ilitajwa na hawa jamaa?

  Na walio Dar kuna kitu kama hicho?

  Mpaka leo sijapa jibu lolote kwenu wana Jf ambao ndio macho yetu sisi tulioko vijijini. Mnasemaje?
   
 9. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Samahani wana JF sikuwa nimeiona hii post. Hivyo tayari nimeanza kupata mawazo fulani kutokana na michango iliyotangulia. Pasi na shaka ni upatu au uhuni wa aina nyingine. Nafikiri watu wanawa target walokole na watu wa makanisani kwa vile wanaonekana kuamini haraka viongozi wao. Nadhani inatulazimu kurudi katika biblia na kufuata ushauri wa Mtume Yohane sura ya nne mst wa kwanza. Msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwani manabii wengi wa uongo wamekwishatokea duniani.
  Mtume Mathayo anasema katika sura ya saba mst 16 anasema mtawatambua kwa matunda yao (na wala si kwa maelezo yao).
  Ahsante JF
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  mkuu omulangi hawa ni matadeci na wala si DECI afadhali DECI wanavuna
  imagine waliwatangazia watu wanaajiri mishahara minono ofisi zao zipo pale manzese
  u know what walichofanya baada ya trainning wakaamua kupata members wa mikoani na kuwaambia wataanza kuwalipa mishahra mwezi wa nane mwaka jana mwezi ulipopita walikuja na sera watatoa nauli tu na ya vyakula walikuwa wanategemea hela kutoka marekani mpaka mwezi wa 12;watu wakawa na imani na wamechangishwa wengi kweli mi kuna mzee wetu mmoja amewakimbia alikuwa anajitolea kweli ilipofika feb nikamuuliza mbona unarudi na malalamiko kila siku akasema hawa ni matapeli nimeamua kuacha kazi zao nikamwambia...pole
  so kama serikali wamejiona na mapunguufu kuruhusu DECI basi waje waziwahi kama hizi maafa yasiwe mazito zaidi.....polen
   
 11. R

  Rwey Senior Member

  #11
  Apr 18, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watanzania tuachane na haya mambo ya upatu, ndio yanayosababisha inflation au mfumuko wa bei kila mara since fedha zinazunguka tuu bila uzalishaji wowote. Lets use our money to make productions from resources we have and not damping somewhere. So bad..:confused:
   
 12. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Tatizo hali ngumu ya Maisha inatuponza, kila kukicha unaona afadhali ya jana !!!!! People are becoming poorer and poorer as time goes!! Hii ndiyo inafanya mtu akisikia tu kuna pesa ya msaada anakwenda , finally anajikuta yeye ndiye anatoa msaada kwa kupeleka kile kidogo alichonacho.
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Being poor is also a state of mind, nimebahatika kwenda nchi mbalimbali za Aisa na siamini kama maskini wa Philipines au Thailand ana pesa zaidi ya maskini wa Tanzania, it is just the attitude. Badala ya kukaa na kulalamika, maskini wa Thailand, India au Bangladesh yuko busy anahangaika kuongeza kipato. and beleive me kule hawana elimu ya bure na huduma ya afya bure kama tunavyodai!
  Rwey mkuu, umenena! Ni ujanja huu unaoongeza mfumuko wa bei kwani bada la pesa hizi kuwekezwa katika uzalishaji imebaki katika mzunguko na watu huzitumia for pure consumption kununua magari, simu nk.
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Oscar Mbuza; Tarehe: 16th May 2009 @ 06:37 Imesomwa na watu: 14; Jumla ya maoni: 0

  Wakati mamia ya Watanzania wakiwa bado na kilio cha kupoteza fedha zao nyingi kutokana na kusitishwa kwa shughuli za Kampuni ya Development for Community Initiative (DECI) hivi karibuni, sakata lingine limeibuka baada ya wanachama wa taasisi nyingine ya Umoja wa Wananchi katika Maendeleo Afrika (PUFDIA), kuingiwa na hofu juu ya mwenendo wa taasisi hiyo, ambayo inadaiwa kujikusanyia mabilioni ya fedha kutoka kwa wananchi.

  Wananchi waliojisajili na taasisi hiyo ya Pufdia, walieleza wasiwasi wao jana pale viongozi wa taasisi walipoitisha mkutano wa wanachama katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam uliokuwa na lengo la kuwaeleza masuala mbalimbali kuhusu taasisi yao. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margaret Sitta, ndiye aliyetangazwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo ingawa hakutokea.

  Wananchi waliofika viwanjani hapo walielezwa kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwafahamisha wanachama wa Pufdia kuwa ni lini wataanza kunufaika na taasisi hiyo, baada ya kuchanga fedha zao ili baadaye wasaidiwe katika ujenzi wa nyumba nafuu, wapate mikopo, elimu kwa watoto wao na pia ujenzi wa shule.

  Pufdia pia inaelezwa kuwa na lengo la kusaidia utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, kutoa msaada na ushauri kwa waathirika na wagonjwa wa Ukimwi, kufungua vituo vya kutibu na kukabiliana na malaria na kutoa vyandarua, kuwatafutia ajira wanachama, kujenga makanisa na kutoa mafunzo ya kilimo bora na cha kisasa kwa watu masikini.

  Saa 4 asubuhi, mshereheshaji wa mkutano huo, aliwatangazia wanachama kuwa mgeni rasmi (Sitta), angewasili katika viwanja hivyo saa 5.45. Na ilipotimia saa tano kamili asubuhi, aliwasili Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Evance Balama, ambaye hata hivyo muda mfupi baadaye aliondoka na kurejea tena katika viwanja hivyo ili kuwahi kumpokea Waziri Sitta.

  Baadaye mshereheshaji aliwatangazia wanachama na wananchi waliokuwa katika viwanja hivyo, kwamba Waziri Sitta hakuwa na muda wa kutosha hivyo angefika mara moja kwa muda wa nusu saa na kisha angeondoka na kumwachia usimamizi wa shughuli hiyo aliyemtaja kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii kutoka wizarani.

  Hata hivyo, muda uliendelea kwenda bila Waziri Sitta wala Mkurugenzi huyo kutokea, hatua iliyoanza kuibua wasiwasi kutoka kwa wanachama kwamba huenda taasisi hiyo ilikuwa inaendesha shughuli zake kwa mtindo kama wa taasisi zingine za upatu ambazo zimepigwa marufuku. Katika kipindi hicho, Mkuu wa Wilaya alikuwa jukwaani akisubiri kumpokea Waziri.

  Baada ya muda mrefu kupita, viongozi wa Pufdia walijadiliana na kuamua kuanza mkutano huo bila mgeni rasmi, kwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Tawi la Tanzania, Jackson Odeki ambaye ni raia wa Uganda, kuwaeleza wananchi kwamba taasisi hiyo imelenga kuwakomboa wananchi wa kipato cha chini.

  Odeki alisema imelenga kuwasaidia Watanzania kujenga shule, zahanati, kukarabati nyumba zao kwa gharama nafuu na kuwasaidia kupata mikopo kutoka kwa wafadhili wa Marekani, Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya.

  Odeki aliyekuwa akizungumza kwa Kiingereza huku akiwa na mkalimani, alisema ili kuonyesha kuwa hakuna ubabaishaji katika uendeshaji wa shughuli hizo alikuwa amewaalika wageni kutoka Marekani, Ujerumani, Kenya na Uganda ili wawadhihirishie Watanzania uhalali wa taasisi hiyo na namna inavyowasaidia watu mbalimbali.

  Aliwataja wageni hao kuwa ni Anke Weisheit kutoka Ujerumani na Aaron Siribaleka kutoka Uganda. Pamoja na kupewa nafasi ya kuwahutubia wanachama wa taasisi hiyo, wageni hao walishindwa kukata kiu ya wanachama hao ya kutaka kujua namna na ni lini wataanza kupata misaada hiyo zaidi ya wote kuwaahidi kuwasaidia kuipata kutoka kwa wafadhili.

  Baadaye Balama alipewa nafasi ya kuzungumza na wanachama hao kutokana na mgeni rasmi kushindwa kufika, na kwa namna fulani aliwatahadharisha wananchi juu ya kushiriki katika masuala wasiyokuwa na uhakika nayo.

  “Mimi nimechukuliwa tu na hawa jamaa (Pufdia) nikijua yupo mgeni rasmi. Hata hivyo, naomba kuwaambia Watanzania, tufanye kazi bila kutegemea mambo ya bahati bahati. Shirikianeni na taasisi hii, wasikilizeni lakini mtumie akili zenu msije mkaingia kichwa kichwa halafu mkajutia baadaye,” alionya Balama.

  Baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kutoa tahadhari hiyo, wanachama wengi walionekana kupatwa na hofu na waliendelea kuhoji namna na siku watakapoanza kupata misaada hiyo, hatua iliyoufanya uongozi kuanza kuzungumza na vikundi katika hoteli ya Peacock ili kuwapa ufafanuzi zaidi, kazi ambayo ilikuwa ikiendelea hadi jana jioni.

  Mmoja wa wanachama wa Pufdia, Suleiman Kato, alisema ili kujiunga na taasisi hiyo, mwanachama hutakiwa kulipa Sh 670,000 kama anataka msaada wa kujenga shule, Sh 470,000 kusaidia kujenga nyumba, Sh 120,000 mtoto wake kusomeshwa kuanzia msingi hadi chuo kikuu.

  “Hizo ni fedha tunazotoa unapojisajili, ili kuwa mwanachama kwa lengo la kusaidiwa hapo baadaye. Hadi sasa tumeelezwa kuwa taasisi imeshakusanya zaidi ya Sh bilioni tano, lakini tuna wasiwasi kwamba huenda tukapoteza fedha zetu maana hatuelewi kinachoendelea,” alisema Kato.

  Hadi sasa taasisi hiyo inadaiwa kuwa na wanachama 25,000 nchini, ikiwa na makao makuu yake katika jengo la Usangi, Manzese, Dar es Salaam, ikiwa pia na matawi 26 katika mikoa 26 na mpango wa kuanzisha matawi wilayani.

  Katibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwandesi, alipoombwa kueleza sababu za Waziri Sitta kutofika katika mkutano huo, alisema ingawa Waziri alikuwa katika mkutano nyeti, lakini pia alikuwa hajazijua vema shughuli za taasisi hiyo.

  Hata hivyo, katika tukio la kushangaza, tayari kulikuwa na hotuba iliyokuwa inaonyesha kuwa ni ya Waziri Sitta ambayo angeisoma katika mkutano huo, na sehemu kubwa ilikuwa inasifu shughuli za taasisi hiyo na kuwataka Watanzania kuiunga mkono ili kujikomboa na kuondokana na umasikini.

  PDADO
   
 15. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Na bado kuna nyingine inaitwa malingumu..... ni suala moja kupanda then kuvuna

  Mi nawashauri watanzania waache kupenda bure bure....
   
 16. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inasemekana leo watakuwa na mkutano na wanachama wao huko Zanzibar na kuwatambulisha hao WASUNGU wanaotoa misaada.

  Mimi nafikiri iko haja kwa wananchi kuifungulia mashitaka serikali kwa kuruhusu hizi taasisi zinazowaibia wananchi na kuendelea kutumbukia katika dimbwi la umasikini. Kwani taasisi hizi huwa zinapata usajiri, kutokana na matangazo yaliyokuwa yakirushwa na chombo cha habari kimojawapo Zanzibar juu ya mkutano wao utakaofanyika tarehe 16/5/09 wamekuwa wakisoma na registration number kutoka kwa msajili kuoyesha uhalali wao.

  Mpaka sasa hivi wamecshachota bilioni tano (5) za watanzania, pesa zinazoibiwa kimachomamcho na hata hakuna anayeonekana kuzuia uhalifu huu.

  Hebu naomba wana JF tusaidiane kimawazo nini kifanyike kunusuru fedha za watanzania ambao wengi wao hawana upeo mkumbwa katika mambo mbalimbali zisiendelee kutapeliwa na baadhi ya watu tena wengi wao ni wageni.
   
 17. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Naona tusiwalaumu sana watanzania kwani vyombo hivi vanakuwa na usajili, kama hawa wanajiita taasisi ya kutoa misaada. Mtu yeyote anaposikia neno msaada ni rahisi kujisogeza.
   
 18. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sikiliza kaka ... suala la kusema kuwa ni misaada sikatai kuwa mtu atakuwa anajisogeza ili apate unafuu wa maisha ila kwa upande huu mi sidhani kuwa watu wanatafuta misaada ila wanatafuta rahisi.. just imagine kuwa mtu anataka asiaidiwe mtaji wa biashara then anatakiwa alipe ada ya kujisajili, au ajenge nyumba lazima alipe ada ya kujisajili na ada hizi zinatofautiana kutokana na ukubwa wa mradi..


  sasa kwa nini mtu asianze kuuza vitumbua na mtaji wa 120,000 afu apande pande kidogo na hatimaye aanze kupandisha msingi wa nyumba?

  Mi nakuambia kuwa wabongo wengi wanapenda vya bure ndio maana wanatapeliwa ..then huwa hawaogopi mpaka watapeliwe kwanza hata kama jirani kaibiwa yeye hujifanya haoni mpaka aibiwe yeye..sasa kama hawa si wajinga ina maana mabibo na manzese ni mbali sana? kilichotokea kule hawakijui?

  Then serekali ina shtaka la kujibu kuhusu hili.....
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli Watz hatuoni kiasi kwamba ***** ye yote na kimradi chake anaweza kuja na kujichotea fedha kiuraini hivi? Inatisha sana.
   
 20. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
Loading...