PUBLIC RELATIONS: Waziri Kabudi alikosea kuikana kauli yake juu ya kifo cha Azory. Alipaswa kukiri ni kweli alifariki ndani ya mioyo ya wanaharakati

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
12,853
2,000
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiJorums.

Ninajua fika baada ya kuandika thread hii kuna watu watanitukana sana, wengine watasema ninajipendekeza kwa wakubwa, wengine watasema ninatafuta uteuzi, wengine watasema mbona ninajishushia hadhi.

Ila ninachosema mimi ni kuwa sipo hapa jukwaani kwa minadi ya kufurahisha watu. Bali nipo hapa kuongelea ukweli kama ambavyo unapaswa kusemwa.

images (7).jpg

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi aliwahi kukanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas alimnukuu Profesa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

Lakini Prof Kabudi pia alisema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Kabudi alisema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

images (8).jpg

USHAURI WANGU WAZIRI KABUDI ANGESEMA MANENO HAYA
=====
Nilichokisema kuhusiana na kifo cha Azory Gwanda ni kweli kabisa na hata sikukosea. Azory alikufa ndani ya mawazo, akili pamoja na mioyo ya wanaharakati ambao kila uchwao walikuwa wakiisumbua serikali kwa kuihoji juu ya taarifa sahihi za mahali alipo na hatua za upelelezi zilizofikiwa na jeshi letu la Polisi.

Sisi kama serikali tunatambua vema mchango wa makundi haya ya watetezi wa haki za binadamu pamoja na asasi za kiraia katika kutukosoa na kutukumbusha juu ya wajibu wetu kwa jamii ya watanzania iliyotupa dhamana ya kuwaongoza.

Kwa niaba ya waziri wa mambo ya ndani, ninapenda kutoa tena salamu za pole familia ya Azory kwa kupotelewa na mpendwa wao na taarifa kamili juu ya tukio hili zitatolewa pindi upelelezi utakapokuwa umekamilika.

Tunaahidi kuwa tutahakikisha kunaendelea kuwa na mazingira bora, salama na rafiki kwa wanataaluma wote wa tasnia hii ya habari kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.

=====

Ni bora baba yangu mzee Kabudi angesema maneno haya.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

Generalist

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,031
2,000
Huenda kama kuna Mtu ambaye anaifanya Hadhi ya Uprofesa Kuanza Kudharaulika nchini Tanzania akawa ni Waziri Kabudi hadi Mchumi Lipumba.
 

Lugano James

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
793
500
Me huwa nawazaga mke watoto baba mama ndugu jamaa na marafiki hali wanayopitia. Bora umzike ujue ashakufa kulipo kusubiri iko siku utamwona. Mama anawahidi watoto baba atarudi kasafiri, mama kiu anayo, ada,matunzo ya familia matunzo ya wazazi. Ndugu. Jamaa. Na jamii

Sikia kwa jirani.
Msalime sana shemeji
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom