Public executions by firing squads: Nigeria

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,005
112,653
Miaka ya 1960 [1960s] na 1970 [1970s], nchi ya Nigeria ilikuwa imeghubikwa na mapinduzi ya kijeshi kwa serikali zilizokuwepo madarakani kwa nyakati hizo.

Moja ya njia zao za kukabiliana na uhalifu kwenye jamii, hususan uhalifu wa mauaji, kulikuwepo na sheria za kunyonga watu waliopatikana na hatia baada ya kutuhumiwa kutenda uhalifu wa kuua.

Moja ya njia zilizotumika kuwanyonga wahalifu hao ilikuwa ni njia ya kuwatandika risasi hadharani wakosaji hao [public execution by firing squads].

Baada ya kuhukumiwa, wahalifu hao walikuwa wanapelekwa sehemu, wanafungwa na kamba kwenye miti au milingoti, halafu wanatandikwa risasi hadharani huku kukiwepo na umati wa watu uliojitokeza kushuhudia.

Kunyongwa kwa kupigwa risasi ni moja ya njia za kikatili sana za kumnyonga mtu, licha ya kwamba kitendo chochote kile kinachoondoa uhai wa mtu hususan pasipo na sababu ya msingi, bado ni ukatili. Lakini pia ukatili nao una viwango vyake.

Hapa chini naambatanisha video kadhaa za unyongaji huo wa kupigwa risasi hadharani. Ni video ambazo ni ngumu kuzitazama, hususan kama una moyo mwepesi. Hivyo zitazame kwa tahadhari.

Hebu ona hao washuhu

Inatia simanzi hata kama yanayouliwa ni majambazi, hususan kama hukuyaona yakitenda ukatili wao.

Jambazi likinyongwa ufukweni mwa bahari. Dah!

Nashukuru Tanzania hatukuwa na mambo haya. La, kama sheria ya kunyonga kwa kupigwa risasi ilikuwepo, basi ilikuwa haitekelezwi.
 
Dah; walivyofungwa kwenye hiyo miti nimemkumbuka Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu JESUS CHRIST aliyenyongwa msalabani kana kwamba ni mhalifu ili kwa damu yake tukombolewe.

Tofauti ya hawa na Yeye, Jua halikwenda kiza yapata saa sita hadi saa kenda; wala Pazia la Hekalu halikuraruka toka juu hata chini Patakatifu pa Patakatifu pakaoneka; wala hawakutamka Lile neno kuu IMEKWISHA bali walikufa katika uhalifu wao! Tena wangalipo udongoni hata leo wakati Mwamba wa miamba akisepa zake siku tatu tu baadaye.

Praize thy name O Lord!
 
So cruel.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom