Pua ya mbwa ikishapata madhara ya kukosa uwezo wa kunusa, kifo chake kimekaribia

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,210
Kwakuwa Tanzania ni nchi yetu sote, namimi kama mtanzania naomba nichangie haya kwa leo. Sina hakika kama nitakuwa katika mkumbo wa makosa ya mtandao, au kukashifu uongozi au vinginevyo maana sasa hivi ukitaka kichangia kitu katika mtandao hakikisha umeaga kwanza. Nimeisha aga!

Kuna usemi wa kihaya unasema " Orulaita embwa rugibanza enyindo" maana rahisi ni kwamba pua ya mbwa ikiisha pata madhara ya kukosa uwezo wa kunusa , kifo chake kimekaribia. Kifo chake kimekaribia maana hawezi kunusa harufu ya fisi, chui wala simba, matokeo yake anakamatwa kiulaini. Hii ilihusu zaidi jamii ya watu walioishi vijijini enzi hizo waliozungukwa na wanyama wakali.

Unapoona uongozi kwa makusudi unaacha kisimamia haki za raia wake, anakandamiza uhuru wa watu wake, anadharau maoni ya watu anaowaongoza anakuwa anawasaliti watawala kwa kuamsha zaidi hasira za wananchi kwa kisingizio cha kuonyesha wenzake kwamba awabana huku akijua kuwa anaamsha zaidi hasira zao, lakini pia kwa kutojua majibu ya anachokifanya anawadhoofisha wenzake kwa kugandamiza zaidi wananchi ambao katika kujinasua hujibu mapigo kwa kishindo kisichotarajiwa ambacho huwa na gharama kubwa kukizima (mfano Syria) au kushindwa kabisa kukabiliana nacho (mfano Algeria).

Nina mashaka saana na aina ya uongozi wa serikali ya kutegemea zaidi vyombo vya dola. Ni kutokana na kushindwa kwa njia hii ya utawala ndio aina ya kuongoza kwa maridhiano au demokrasia kukajitokeza. Style ya uongozi wa mabavu ilikuwa muafaka saana miaka ya kikoloni, lakini miaka hii ya watu kujitawala, kujichagulia uongozi kwa njia ya demokrasia uongozi wa aina hii hauwezi kufauru. Utawala wa mabavu ukilazimishwa saana hutengeneza mgandamizo wa fikra za watu na kusababisha harakati mbalimabali zikiambatana na kuunganisha nguvu za hata wale waliodhaniwa maadui dhidi ya wagandamizaji. Tuliisha ona UKAWA hapa, sasa tutatengenea kundi jingine. Gharama ya kushughulika na harakati hizi ni kubwa mno. Tuliona moto wa UKAWA katika uchaguzi na nguvu iliyotumika kushinda umoja huo. Hatua ya kiharakati kwa njia ya muungano wa makundi mbalimbali ikifikiwa itapelekea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika vyombo vya dola ili kukabiliana nayo ikiwemo kuajiri idadi kubwa sana na askari polisi, wanajeshi, magereza na hii inaenda sambamba na vitendea kazi vyao ikiwemo idadi kubwa ya bunduki, vifaru, magari ya washawasha FFU n.k. Itasababisha kubadilisha bajeti ya maendeleo kuwa bajeti ya ulinzi na usalama. Lakini hii Itatisha watu kwa muda tu halafu watu watakuwa sugu na italazimika kutumia nguvu zaidi ambayo itaishia kutangazwa kwa hali ya hatari. Matokeo yake kutatokea mlipuko, ni wa kiasi gani? mimi sijui!

Tukifika katika hatua hii, badala ya watu kupata maendeleo uliyokusudia kuwapa wataishia kuvuruga hata kilichokwisha patikana miaka 50 iliyopita. Kuatokea kuharibu miundombinu, migomo, vita n.k. Hii itapelekea vifo vy raia wasio na hatia, viongozi kutolewa madarakani au kuongoza kwa nguvu ya dola. Watawala wataongoza wanajeshi, polisi, majeruhi, yatima, vilema na vikongwe wasio kuwa na uwezo wa kukimbia. Wenye uwezo wa kukimbia watakuwa wakimbizi Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Malawi, Msubiji, Zambia na Congo.

Hivi kuna haja ya kufika hatua hii? kisa utawala! maana sio uongozi tena!

Mzee Mwinyi aliweka muda wa kila Ijumaa kusikiliza kero za wananchi, hakupungukiwa heshima ya urais wake. Naamini hata Rais wangu mpendwa JPM anaweza kuanzisha kitu kama hicho kwa style yake si kwa wananchi tu bali hata vyama vya siasa na taasisi mbalimabli. wananchi wakisikia jambao kama hili nyongo hurudi mahala pake na tabasamu hujaa usoni mwao. hata ukiwaambia hapa kazi tu wanashangilia, ukiwaambia kulipa kodi ni wajibu wanaitikia kwa furaha.

Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na kile kinachotokea bungeni, uhasama kati ya wabunge wa CCM na wa UKAWA. Hivi kusikiliza wapinzani wanataka kusema nini imeanzalini kuwa haramu? Kwani wapinzani wakitoa hoja za uongo, serikali hawawezi kuzikanusha? Tuhuma zikiwa za ukweli serikali haiwezi kuzitolea maelezo? Kama kuna makosa yalifanyika, srikali haiwezi kukiri na kutoa ufafanuzi wa jinsi walivyojipanga kurekebisha makosa hayo? Hivi hiyo ikifanyika mboan Ackson ataweza achia wenyeviti waendeshe vikao tu! Hivi Tulia akiungua Bunge litahairishwa? HII style ya kutegemea mtedaji mmoja mbona haijengi?

Nilipenda saana usemi wa Baraka Obama alioutoa alipopata urais kwa mara ya kwanza, alisema atapokea ushauri wa watu wote na hasahasa wenye mtazamo tofauti nayeye maana hao ndio anahoja ya kutafakari. Nashauri viongozi wetu waige tabia hii ya kusikiliza mawazo mbadala. Mgomnano wa mawazo huchochea maendeleo. Mawazo ya upande mmoja hudumaza maendeleo.

napenda pia kushauri neno upinzani ufutwe kabisa , litumike neno mbadala. Tuseme vyama Mbadala, mawazo mbadala, kambi mbadala bungeni, kiongozi wa vyama mbadala bungeni labda hii itabadilisha mtazamo wa viongozi kuona vyama mbadala ni maadui wa taifa.

Wahaya pia wana usemi unasema "Empisi ekanyampila eibale eti norwo'toyetengya kyonka wakahulila" Tafsiri ya moja kwa moja kwa maba Chui alikaa juu ya mwamba na katoa ushuzi. Chui anaamini katika ukali wa hewa yake chafu. Alitegemea kuona mwamba unalalamika kwa kujitikisa lakini hilo halikutokea. Imani ya Chui ni kwamba kwa vyovyote vile jiwe hilo limepata habari yake ndipo akasema japo umekaa kimya lakini chamoto umekipata. Hapa nataka kusema kwamba n kawaida ya watawala kusikia hoja zenye mashiko na kuzitupilia mbali. Kwa hoja hii nasema tena kwamba "Bagambila balinsi bali'iguru kuhurila" maana yake - mwenye masikio na asikie!

Sidhani kama huu ni uchochezi!
 
Sisi wananchi ndio wajinga wakati yeye anaunganisha nguvu na bunge na akiwatumia polisi popote anapoona inafaa basi sisi lazima tujue nani wa kuungana nao ili tuendeleze mapambano ya kudai haki na demokrasia.

Tuungane na wafanyabiashara, wafanyakazi na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kuandaa kila aina ya mgomo mpaka serikali ikubali kukaa meza moja na wanasiasa ili kujadili hatima ya Nchi yetu.
 
Maneno kuntu haya na jamaa hawachelewi kukuita mhaini kuwa karibu na ubalozi wa EU for any kinds of threats .
 
Back
Top Bottom