PTI yakana kutengeneza ARV’s bandia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PTI yakana kutengeneza ARV’s bandia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rosemarie, Oct 12, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  KIWANDA cha Tanzania Pharmaceutical Indusrties Ltd (TPI), kimekanusha kuhusika na usambazaji, uzalishaji wa dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV’s).Kiwanda hicho kinachomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali asilimia 40 na wamiliki wazawa asilimia 60, kimesema kuwa kinazalisha dawa ya TT-VIR 30 na si TT-VR30 ambayo ni bandia huku utaalamu wao wakiupata kutoka nchini Thailand.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TPI, Zarina Madabida, alisema kuwa kiwanda hicho hakijawahi kutengeneza dawa hiyo.Madabida ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum (CCM), alisema kuwa kiwanda hicho hakiwezi kutengeneza dawa bandia ikizingatiwa kuwa ni teknolojia yao inachanganya dawa na kuwa katika muonekano mmoja na si rangi tofauti kama dawa hizo bandia.Badala yake, mbunge huyo alihusisha tuhuma hizo na harakati za kuchafuana ili kiwanda hicho kifungwe.Alisisitiza kuwa kutokana na hali hiyo wanaunda timu yao ya uchunguzi kuhusiana na jambo hilo ili wajue nani aliyefanya mchezo huo wa kiuaji na wakishetani na kwamba hawatakubali mpaka wezi hao wakamatwe.Madabida aliongeza kuwa anashangazwa na dawa hizo kukamatwa Agosti wakati wao dawa zao zilipelekwa kwa msambazaji (MSD) Machi 2011.“Mimi nashangaa sana sisi dawa zetu zilitoka Machi na muda wote huo hatujatengeneza, sasa iweje zionekane feki Agosti?Alihoji na kuongeza kuwa “hatuwezi kuua ndugu zetu wala kuharibu biashara yetu hapa nimechezewa faulo.”Kuhusu kiwanda hicho kufungiwa na serikali ili kupisha uchunguzi, alisema bado hajapata taarifa bali amepewa barua na TFDA kujieleza ndani ya siku 14 kwanini asifungiwe.Akizungumzia wagonjwa wanaotumia dawa hizo kuandamana alisema kuwa wana haki ya kufanya hivyo kwani wanatetea uhai wao.Kiwanda cha TPI, ni kiwanda kikubwa cha dawa kwa ukanda wa Afrika Mashariki kilichokuwa kizinduliwe Novemba mwaka huu kikiwa kimewezeshwa euro milioni 5 na Shirika la Afya Duniani (WHO).
   
 2. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Kila kashfa CCM wapo ! dah
   
 3. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Rekebisha heading kidogo ni TPI sio PTI
   
Loading...