Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,449
Wanabodi

Kati ya udhaifu mkubwa sana wa media zetu Tanzania, sii redio, TV na Magazeti, hatuna competent people wa kufanya news analysis, kazi kubwa media zetu ni kufanya reportage tuu ya matukio, lakini hatuna uchambuzi wa matukio na hatuna wachambuzi.

Kwa vile mimi ni miongoni mwa waandishi wa habari wachache wenye uwezo wa kufanya news analysis, mara moja moja nipatapo nafasi nitakuwa nawaletea news analysis ya baadhi ya matukio muhimu kwa taifa letu.

Uchambuzi wa leo, nitawachambulia kuhusu mfululizo wa matukio ya rais Magufuli kuombwa msamaha na baadhi ya wanasiasa baada ya voice notes zao ku leak kwenye public domain.

Waomba msamaha ambao tayari wameomba msamaha ni January Makamba, huyu ameomba msamaha for strategic reasons, sio kwa sababu amekosa. Ngeleja kaomba msamaha kwa kujikomba tuu, Nape kaomba msamaha kwa uoga wa kitakacho mkuta. Bado kuna watu watatu wengine ambao voice notes zao zili leak na hawajaomba msamaha, hawa ni Makamba Senior, Benard Membe na Abrahaman Kinana. Kuna swali watu wanajiuliza who is next kwenda kwa rais Magufuli kuomba msamaha. The next is Makamba Snr, huyu ataomba msamaha kwa sababu rais Magufuli kasema ametukanwa, Membe will never kneel down kwa Magufuli kuomba msamaha for Pride, Kiburi na Jeuri, na Kinana pia, will never beg for mercy for Integrity reasons, aombe msamaha kwa kosa gani?.

Nauweka uchambuzi in points format ili iwe rahisi kuulizia any specific point.

Kwa utangulizi, kwa vile humu mitandaoni, kila siku kuna watu ni wageni, naomba nianze na utambulisho wa psychoanalysis ni nini.

1. Psychoanalysis ni Nini, na ya Kazi Gani?
Kuna msemo usemao, information is power, yaani ukiwa na taarifa sahihi, unakuwa na nguvu, hivyo hii psychoanalysis ni somo la kujifunza kwa nini watu wana behave kwa namna fulani kwenye situations fulani. Hivyo ukijua tabia za watu, kwa nini they behave the way they behave, wewe unakuwa na power ya kuwafahamu na sometimes bila wenyewe kujifamu, hivyo kwa kuandika humu kuhusu human behaviors, hii inaweza kuwasaidia kubadilika, and changing for the better kwa kupunguza maneno na kuongeza vitendo. Waalimu wakuu wa hili somo la psychoanalysis, ni wawili, Carl Jung na Sigmund Freud
Kujua zaidi Psychoanalysis tembeleeni

2. Msamaha ni Confidential, Uki Forgive You Forget, Kwanini Rais Magufuli Amekuwa Mkweli na Muwazi?.
Mimi ni Mkristu Mkatoliki, ukifanya dhambi yeyote, unakwenda kuungama dhambi zako mbele ya padre, anakuondolea dhambi zako kwa kupewa sacrament ya Kitubio, kisha unaadhibiwa adhabu ya kufanya malipizi kutokana na ukubwa wa dhambi zako. Process yote ya kutubu dhambi kwa Wakatoliki ni low profile and very confidential with fiduciaries relationship hata ukitubu wewe ndiye uliyeua mtu, Padri anafanya siri hawezi kukuripoti popote kwanza hakuoni, unawekewa kitambaa cha opaque, haoni mtu, anasikia sauti tuu.

Hivyo kitendo cha rais Magufuli kutangaza walioomba msamaha na kuwasamehe is a breach of trust and confidentiality ila rais Magufuli ametangaza kwa nia njema kabisa ya kuonyesha yeye ni Mkristo safi, anayetekeleza sala kwa vitendo, pale kwenye " mtusamehe dhambi zetu kama na sisi tunavyowasamehe waliotukosea" hivyo pamoja na ukali wote wa rais Magufuli ni mtu mwenye upendo na huruma sana.

Ametangaza wazi wazi kwasababu yeye ni mkweli na muwazi, sometimes ni mkweli too much, na muwazi too much, ila pia kwa maoni yangu, ambayo ni reserved, kuna sababu nyingine ya the motive behind rais Magufuli kutangaza aliowasamehe, ila naomba nisiitaje kwa sababu inahusu kutuma ujumbe kwa watu fulani kuwa wenzenu wameomba msamaha hivyo...

3. Msamaha wa January Makamba,
January Makamba ni true serious politician mwenye very high prospects na very bright future kwenye politics. Mambo aliodukuliwa alioongea na baba yake kwenye simu, na Nape, hebu kwanza isikilize
Sauti inayodaiwa ni ya Mzee Makamba na Mwanaye January Makamba ...
kiukweli kabisa ni mambo ya kawaida sana, hakuna popote mtu yoyote ametukanwa, hizi clips ni clips za jinai, hawa walipaswa kushitaki polisi, TCRA imtafute aliyetenda jinai hii ya kusambaza, ashughulikiwe kisheria, hakuna kosa lolote January ametenda, amesema, hakuna kosa lolote Mzee Makamba ametenda, amesema, hakuna kosa lolote Nape ametenda, amesema, kwa vile baada ya ku leak sauti hii, January alitumbuliwa, hilo pekee ni taarifa kuwa the Big Boss is not happy!. Kwa vile January ni carrier politician, na ni diplomat of his own kind, akaamua kuwa mdogo, kujishusha, iwe amekosa au hajakosa, akaamua kuliko kununiwa na kukasirikiwa, bora akaombe msamaha, awe at peace na Top Boss ndipo aendelee na mambo mengine kwa amani.
Kwa msiomfahamu vizuri JM. inaweza kumsoma hapa
January Makamba, very intelligent, humble, down-to-earth! Can make ...
January Makamba Top The List of Most Interactive Politician in TZ ...

4. Msamaha wa William Ngeleja.
Nimeisikiliza clip ya Nape na William Ngeleja, naomba na wewe isikilize tena na mtu aniambie kama kuna mahali popote mtu yoyote ametukanwa.
Clip ya sauti inayodaiwa ni maongezi ya simu ya Wanasiasa William ...

Hayo mambo Ngeleja alioongea humo ni mambo ya ukweli mtupu, kama sasa hata kutoa truthful na genuine opinion za ukweli kabisa ni jambo la mtu kwenda kuomba msamaha, kiukweli, we are not going to be fair to our self, kama haya ndio Ngeleja aliokwenda kuombea msamaha , then kiukweli kabisa, huo ni msamaha tuu wa kujikomba komba baada ya kufumaniwa pants down, lakini alichosema Ngeleja humu ndio ukweli wa moyo wake, kama mtu unasema ukweli wako, Boss anakasirika, mwanaume wa kweli anasimama katika kweli no matter what na sio kujikomba komba kupindukia, hii ya Ngeleja ni kujikomba.

5. Msamaha wa Nape Mnauye.
Nape Mnauye ni born and breed CCM, hata ukimkata na wembe damu yake haitakuwa nyekundu kama damu nyingine, huyu ukimchanja, damu yake itatoka ya rangi ya kijani na njano!. Sauti yake iko kwenye zile clips mbili za mwanzo, kiukweli Nape amastahili kuomba msamaha wa dhati sio tuu kwa sababu ya hizi clips bali kwa tweets zake. Kwa maoni yangu, Nape ameumia sana kutumbuliwa, kwa sababu kiukweli kabisa katika kutumbuliwa kwake, Nape ameonewa na ana haki ya kukasirika. Kwa vile kwa Nape CCM ndio baba, CCM ndio mama, tangu Nape amezaliwa CCM, amelelewa CCM, amekulia CCM, amesomeshwa CCM na ameajiriwa CCM na hajawahi kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya CCM. Kwa vile Rais ni top boss wa CCM, baada ya rais kusema amewasamehe walioomba msamaha, Nape akaamua japo yeye ndio alikosewa na kutumbuliwa bila kosa, kwa vile Boss amesema ametukanwa, then akaona sii busara yeye ni kama mwana mpotevu karejea kwa baba yake kuomba msamaha. Msamaha wa Nape ni very genuine na ni human, baba ni baba, hata akikusea wewe mtoto omba msamaha, kumbuka kanuni ya "The boss is always right".

6.Who is Next Kubisha hodi Ikulu Kuomba Msamaha ni Mzee Yusuph Makamba, Why?.
Kwa mliozisikia hizo clips, mmemsikia Mzee Makamba, kiukweli kabisa, hakuna neno lolote baya Mzee Makamba ametamka, wala hajamtukana mtu, kitakachompeleka Makamba kuomba msamaha sio voice note bali ni ushiriki wake kuandika waraka ule. Kwa mliousoma huo waraka, na jinsi Makamba alivyo, huyu atausema tuu ukweli wake kuhusu waraka huo kuwa yeye alishawishiwa tuu na kuusaini. Atamruka mtu kimanga, sababu ya kufanya hivyo ni ili tuu astaafu kwa amani na kuendelea kuisafisha nyota ya Januari. Hivyo Mzee Makamba, ataomba msamaha kwa uoga tuu, tena atasifu hadi kutoa na misatari ya Biblia!.

7. Comred Kinana.
Huyu is the man of principles and integrity, anakisimamia kile anachoamini, ule waraka ni wake, na yote alioongea ni yake na ni kweli tupu, men of principles and integrity they stand with what they believe, kama ni kuadhibiwa kwa kuusema ukweli, let it be!. Hapa naomba kutoa angalizo kuhusu Kinana, kwa mambo Kinana aliyoifanyia CCM, akija kuadhibiwa adhabu yoyote kwa kuonewa, kwa kuusema ukweli wake, kiukweli kabisa Mungu atampigania!, hiyo karma yake.... usipime!.
Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na ...

8. Benard Membe
Sauti inayodaiwa ni ya Membe na Katibu Kata kijiji cha Rondo video ...
Tangu kuanza kuvuja kwa hizi sauti, hakuna mwingine yoyote ni bold enough kukiri kuwa ni sauti yake, Membe tuu pekee ndio lijitu bold lenye ma confidence ya ajabu, limekiri sauti iliyodukuliwa ni yake na anajua sauti hiyo imedukuliwa na TISS, anajua kudukuliwa ni kosa la jinai hivyo anashangaa rais anatumiaje data zilizopatikana kujinai kuadhibu watu?. Kwa vile Membe bado ana kinyongo cha kushindwa na Magufuli, halafu Magu amemshiti jumla na kumtelekeza, hivyo kwa vile Membe aligombea na Magufuli, anajiona yeye ni bora kuliko Magufuli, hivyo Magufuli kwake japo ni rais wa nchi, lakini Magufuli hajawahi kuwa kachero, kutokana na ukachezo mbobezi anayejua sheria, taratibu na kanuni, anajua kudukua ni kosa la jinai lakini rais anaitumia jinai hiyo kuwatisha watu wanaomkosoa, hivyo kwake, Magufuli sii lolote sii chochote, ana pride fulani, ni kiburi na jeuri ya ukachero. Huyu hataomba msamaha wowote kwa yeyote na popote na yuko tayari kwa lolote, liwalo na liwe!.
9. My Take.
1. Kwanza kitu alichokifanya rais Magufuli cha kuwasamehe wakosaji hawa, ni kitu kizuri sana, rais Magufuli ameonyesha yeye ni mtu mwenye huruma na mwenye upendo. Ningemuomba rais Magufuli ailekeze huruma yake na upendo wake kwa mamia ya Watanzania wanaoozea mahabusu na magerezani, iwe ni wakosaji wa kweli au laa, kuna watu wanaozea magerezani kwa kesi ambazo hazina dhamana bila kesi zao kusikilizwa kwa muda mrefu, hawa ni baadhi yao tuu ninaowafahamu mimi, akiwemo Erick Kabendera, James Rugemalila, Peter Noni, Dr. Ringo Tenga, Harry Kitilya, Jamal Malinzi, Kaburu, Isaack Kasanga, Sioi Sumari, Shose Sinare, Gonzaga Mandago, Asa Mwaipopo, Deo Mwanyika, Dickson Maimu, Alex Lugendo, masheikh wa uamsho, and the list goes on, kiukweli hawa watu wanateseka.
2.Udukuzi ni kosa la jinai, ili nchi yetu kuonyesha inaheshimu utawala wa sheria, baada ya zoezi la misamaha kukamilika, naomba serikali yetu iwachukulie hatua wadukuzi sio waliodukua, maana hawa tunawajua na tunajua udukuzi unaendelea kufanywa kila siku, tena usikute hata mimi ninadukuliwa, bali walio likisha sauti hizo zilizodukuliwa kinyume cha sheria, wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, tena kitu cha ajabu, unaweza kukuta hakuna hata mtu mmoja kati ya walidukuliwa amekwenda kushitaki au kulalamika rasmi mawasiliano yake binafsi kudukuliwa kinyume cha sheria, naijua sababu iliyofanya watu walio dukuliwa wasiende kuripoti popote, naomba kuwafariji kwa kuwaeleza kitu kinachoitwa karma kitawalipia, wadukuzi yatawawakuta ya kuwakuta na walio watuma, na waliodukuliwa na kuwa persecuted, watafidiwa na malipo ni hapa hapa duniani, mbinguni ni hesabu tuu!.

10. Hitimisho.
Huu utamaduni wa mtu kusema ukweli halafu kwenda kuomba msamaha kwa rais na kusamehewa, unatia moyo sana, Hata mimi na kampuni yangu ya PPR, kuna madhila fulani ninayopitia, sasa sijui kama ni lile swali langu la Ikulu siku ile au ni zile makala zangu za kwa maslahi ya taifa magazetini, au ni hii michango yangu humu jf, hivyo nami najifakari mara mbilimbili, hata kama unajua kabisa hujakosa, lakini kama Wazee wanakasirika, nawaombeni sana msinishangae siku mkisikia na mimi nimeomba msamaha kwa maswali yangu, makala zangu na michango yangu humu jf, ambayo haikuwapendeza wakubwa, na nikiona vipi, naombeni msinishangae nikiamua kuachana kabisa na hii kazi ya uandishi wa habari, nikajiunga na chama, nikaunga mkono juhudi na kujitolea kumsaidia ...

Nawatakia Ijumaa Kareem, Furahi Dei Njema.
Paskali
Dodoma.

Paskali.
Update 12/05/2023
Bernard Camilus Membe,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu,
Imani umeitunza,
Mwendo umeumaliza!.
Bwana alileta
Bwana ametwaa
Jina lake Lihimidiwe
RIP Bernard Cammilus Membe
Paskali
 
Ahsante mkuu, ila hili la kwamba ulimchomea Erick Kabendera lina kuweka kwenye kingdom hadi species moja na mashetani wasiojulikana!

That means nawe ni usiyejulikana unayejulikana na unaanza unafiki wako........ Kabendera is deadly sick kwa sasa, how do you benefit?
 
The next Makamba Snr, huyu ataomba msamaha kwa sababu rais Magufuli kasema ametukanwa, Membe will never kneel down kwa Magufuli kuomba msamaha for Pride, Kiburi na Jeuri, na Kinana pia, will never beg for mercy for Integrity reasons, aombe msamaha kwa kosa gani?.
Hapa kwa kiasi kikubwa nakubaliana na wewe, lakini naamini kitakachomfanya Makamba Sr kuwa NEXT sio kwa sababu Rais akasema ametukanwa, bali kwa the very same strategic reasons za Makamba Jr.

Ni the same strategic reasons ambazo zilimfanya Mzee Mwinyi amtolee povu Makamba Jr.
 
Mkuu, naomba nikukumbushe maneno ya mwanaharakati huru kwamba unahitaji kuwa na degree pendwa ili uweze kuwa kwenye hicho chama walichopo hao watu. Kiutendaji Mh. Raisi yuko vizuri kama nilivyoandika kwenye tathmini yangu nimeitoa leo, kwa mantiki hiyo mahesabu yamekaa vibaya hivyo lazima warudi kundini. Come 2020 hakuna wa kusimama naye kwenye hicho chama na kwa kiasi fulani upinzani umebanwa.
 
Wanabodi

Kati ya udhaifu mkubwa sana wa media zetu Tanzania, sii redio, TV na Magazeti, hatuna competent people wa kufanya news analysis, kazi kubwa media zetu ni kufanya reportage tuu ya matukio, lakini hatuna uchambuzi wa matukio na hatuna wachambuzi.

Kwa vile mimi ni miongoni mwa waandishi wa habari, mara moja moja nipatapo nafasi nitakuwa nawaletea news analysis ya baadhi ya matukio muhimu kwa taifa letu.

Uchambuzi wa leo, nitawachambulia kuhusu mfululizo wa matukio ya rais Magufuli kuombwa msamaha na baadhi ya wanasiasa baada ya voice notes zao ku leak kwenye media.

Waomba ambao tayari wameomba msamaha ni January Makamba, huyu ameomba msamaha for strategic reasons, sio kwa sababu amekosa. Ngeleja kaomba msamaha kwa kujikomba tuu, Nape kaomba msamaha kwa uoga wa kitakacho mkuta. Bado kuna watu watatu wengine ambao voice notes zao zili leak na hawajaomba msamaha, hawa ni Makamba Senior, Benard Membe na Abraham Kinana. Kuna swali watu wanajiuliza who is next kwenda kwa rais Magufuli kuomba msamaha. The next Makamba Snr, huyu ataomba msamaha kwa sababu rais Magufuli kasema ametukanwa, Membe will never kneel down kwa Magufuli kuomba msamaha for Pride, Kiburi na Jeuri, na Kinana pia, will never beg for mercy for Integrity reasons, aombe msamaha kwa kosa gani?.

Nauweka uchambuzi in points format ili iwe rahisi kuulizia any specific point.

Kwa utangulizi, kwa vile humu mitandaoni, kila siku kuna watu ni wageni, naomba nianze na utambulisho wa psychoanalysis ni nini.
Karibu uandamane nami.

1. Psychoanalysis ni Nini, na ya Kazi Gani?
Kuna msemo usemao, information is power, yaani ukiwa na taarifa sahihi, unakuwa na nguvu, hivyo hii psychoanalysis ni somo la kujifunza kwa nini watu wana behave kwa namna fulani kwenye situations fulani. Hivyo ukijua tabia za watu, kwa nini they behave the way they behave, wewe unakuwa na power ya kuwafahamu na sometimes bila wenyewe kujifamu, hivyo kwa kuandika humu kuhusu human behaviors, hii inaweza kuwasaidia kubadilika, and changing for the better kwa kupunguza maneno na kuongeza vitendo. Waalimu wakuu wa hili somo la psychoanalysis, ni wawili, Carl Jung na Sigmund Freud
Paskali.
Hivi mwenye akili timamu anaweza kuomba msama kwa kukataa kuita Chepe kijiko kikubwa? Tukubali kuna tatizo hapo jumba jeupe, baba mwenye nyumba anahitaji kufanyiwa psychoanalysis, period.
 
Heshima yako mkuu,
Wasalimie sana Mark na Philipo.

Mark nili-hustle nae kielimu.He is one of the good guys I ever met.Anasifa ya kuona future ,creative, curious and intelligent.

He knows me very well ila sio ID hii.

Nakuheshimu mzee wetu Kwa mafundisho yako unayotupa hapa jukwaani
 
Back
Top Bottom