Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Mimi umenigusa sana kuna nguvu na mimi ninazo hapo,kwa mfano unaweza ukanisimulia story kuhusu watu au mtu fulani siku nyingine kabla haujanitambulisha naweza kukisia majina yao kutokana na story yako na kweli inakua hivyo

Nguvu nyingine ni ile uswahilin inaitwa machale kwa mfano wakati nasoma nilikua naotea sana maswali kabla ya mtihani,vile vile naweza nikaunganisha matukio kwa mfano mtu anapiga misele sister nikimuona tu mtaani nilikua nikimuhis ni kweli au nikikaa karibu na mtu mbaya jiran sehemu kama bar huwa nahis na siku moja nilishawah hama meza kwa kuhis jiran si mtu mzur baadae mwenyej wangu alivyokuja kabla sijamuhadithia akaniambia "unamuona yule dada ukimtongoza ukakaa naye meza moja anakuwekea madawa kwenye bia au anakutengenezea fumaniz fake ili wakupore na masela wake"

Maajabu yule dada ni mzur na amekaa kistaarab na mimi ni mgeni hiyo mitaa hadi mwenyewe nilijiogopa yale machale
 
hizi ni akili za wahashi huru! kumwambia mtu kuwa aamini kuwa hata kama huamini hakuna Mungu unaweza kufanya muujiza hakuna kitu kama hicho!
nijuavyo mimi anayeweza kufanya miujiza ni lazima aamini upande mmoja wa shilingi either Mungu au shetani tofauti na hapo hakuna muujiza wowote, hata vitabu vya dini vimethibitisha uwepo wa nguvu nyingine kutoka upande wa pili.
 
Mkuu Mshana,
Nakubaliana na wewe, hata mimi kuna wakati niliishi India, nikasoma sana buthiism, na ku practice ayuverda na pranayaana hivo nika turn vegetarian, pia nimemsoma sana krishna, niliporudi bongo, nikajikuta nashindwa ku mix na watu wangu!, kwanza nilianza kuirudia wine, kisha kuendelea kupiga kinywaji na hatimaye kurudia nyama!.

Wakati wa practive ni kweli nilikuwa poweful, nikajikuta badala ya kuishi kwa raha kufuation high state of alert, unajikuta unaishi kwa mateso, mathalan unagundua baadhi ya watu waliokuzunguka wako kinyume na wewe!, au kuna hiyo siku wife alitoka party ya kazini, sixth sense imekuambia mwenzako "tayari" ili kukuzuga, ajajifanya yuko "high!" akihitaji huduma!. "Mzee" aligoma! lakini aliamshwa!, na kwenye "game" ilibidi ajitahidi sana na ku fake "kufika" mapema kuliko kawaida!. Kupitia mazoezi hayo, unaweza kudistinguish "kufika" kweli na "kufika" fake ili kunizunga!.
Unakuja ile genuine trust, love na happyness inayeyuka kwa kujua you are cheated!.

Hivyo info nyingine unaachana nazo for love peace of mind and tranquility ya mahusiano!.

Ndio maana ukiwachunguza matajiri wengi, utagundua they are not real happy!. Unaweza kuwajua kwa kuwatazama machoni!. Nimejiamulia bora kubaki masikini happy kuliko tajiri huzuni!. Na sometime ukifuatilia life stily za hao matajiri, licha kula dinner Kempinsky, hawa enjoy kama sisi tunakula chips vumbi!.
Wee acha tuu!.
Pasco.

Very same xperience kaka mimi baada ya kurudi bongo nikashindwa nikakimbilia Nairobi kwa wakrishna lakini nguvu ya wazazi na ndugu jamaa na marafiki ikanirudisha bongo nikafuata mkondo kama wako mengine siwezi kuyaweka Hapa is too personal lakini ile elimu ina nguvu ya ajabu mno itabidi tuonane tunaweza fanya kitu
 
Na wabongo tunavyopenda habari kama hizi na kwa uwezo wa Pasco kujieleza, akiamua anaweza kuwa milionea kwa muda mfupi sana though anachoeleza kina make sense.
pasco dunia ni yako chaguo ni lako, amua kuendesha Range Rover leo!

ha haaa Pasco ukitunga tu kitabu title
'namna ya kupata mwanamke yeyote unaemtaka bila jasjo'
utaendesha Range so soon lol
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Pasco kwa mada hii.Hili ni jambo ambalo limenitatiza kwa muda mrefu na nimekua nikitamani nifungulie nguvu hizi lakini bado sijafika huko.Nimesoma sana kuhusu haya mambo na ninashukuru kupata kitabu cha The Master Key hiki ndicho kilichonitambulisha kwenye ulimwengu huu.

Ninaendelea kujisomea kila siku na sasa nimejikita kwenye maandiko ya Tibet hssa hasa mafundisho ya Atisha.Ninatumaini nitagika huko ninakokutazamia kwa maana yote haya ni nguvu ya Mind.[/QUOTE

Nipe jina la muhandishi wa the Master key?
 
Mh hapa sasa ndio penyewe nimekua nikifanya kitu nahisi kama kuna siku nilishakifanya lakin tatizo sikumbuki ni wapi na lini kwa mfano naweza kukutana na mtu popote pale iwe njiani au kwenye gari na tukianza kupiga piga stori nakuwa kama napata picha ya hayo tunayozungumzia yalishapita lakini kiuhalisia haijawahi kutokea, hapa nitakua katika kundi gani mkuu Pasco

haa hii hali hata mimi huwa inanikuta mara kwa mara,pia na matukio ya kwenye ndoto yananitokea in real world..nimejaribu kusoma vitu mbalimbali ila naamini Pasco atatufafanulia zaidi..
 
Last edited by a moderator:
Mi kuna wakati nilianza kidogo kufuatilia haya mambo nikaona nakua kama taahira nikaacha. Ila kuna baadhi ya mambo mazuri ambayo niligundua. Mfano njia zao za relaxation mi nilizipenda sana na mpaka sasa huwa nazitumia. Yaani kuna wakati labda unaweza kupata mshtuko moyo ukawa unaenda mbio.. lakini ukitumia hizi mbinu za kurelax kama alivyoeleza mdau unajikuta unarudi kwenye hali ya kawaida very soon. Pia usiku kama umekosa usingizi au unataka kulala mchana ukifanya relaxation na ku clear mind hata kama una mawazo kiasi gani yani ni dakika unaishia usingizini..! Otherwise mambo ya sijui kukodolea macho mshumaa hapana..!!
 
Asante sana Pasco kwa mada hii.Hili ni jambo ambalo limenitatiza kwa muda mrefu na nimekua nikitamani nifungulie nguvu hizi lakini bado sijafika huko.Nimesoma sana kuhusu haya mambo na ninashukuru kupata kitabu cha The Master Key hiki ndicho kilichonitambulisha kwenye ulimwengu huu.

Ninaendelea kujisomea kila siku na sasa nimejikita kwenye maandiko ya Tibet hssa hasa mafundisho ya Atisha.Ninatumaini nitagika huko ninakokutazamia kwa maana yote haya ni nguvu ya Mind.[/QUOTE

Nipe jina la muhandishi wa the Master key?

Mkuu mwandishi ni Charles F Haneel
 
Pasco huo uwezo wa 'kata funua' bila kusema neno sipati picha
hizo pm za watu uwafundishe utakazopata lol

kikazi je uwezo ako ulikusaidia kupata kazi? kazi ipi kwa mfano?
Mkuu The Boss, kiukweli, wanawake wengi huwa wako tayari kwa lolote, na kuna wengi wanakuhitaji bila wewe kujua, ikitokea mmoja amekuzimia, ukishika tuu mkono ni "twende!" bila kutia neno lolote!. Zile zunga za kujifanya kusubiri kuanza, au akianza kujifanya ana sita sita au kukataa ni aibu tuu ya kawida ya kike ya kiafrika!, ukimkuta kwenye angle muafaka!, huwezi amini, hatii neno!.

Mimi nakumbuka one day mitaa ya gymkana kwenye vile viti vya cement enzi hizo, nimejikalia na kabinti ka watu mpaka giza lilipoingia, kuangalia huku na kule hakuna mtu!, "tukaendelea!", kumbe kule huwa kunalindwa na FFU wa Ikulu!. Si wakaibuka!, kumbe walituona kitambo.. wakatulia kuangalia sinema ya bure, tulipomaliza. jamaa hao!.."usipime!, tena enzi hizo mtu huna hata chapaa!,

Kikazi, umenisaidia sana. Kwanza niliachishwa kazi TBC 2002 kwa sababu fulani!, kwa hasira nikaamua sitaki kuajiriwa tena!. Tangu pale nikawa mtangazaji wa kujitegemea!. 2008 I got a very bad bike accident, nikalazwa for 6 months na kuwa partially paralysed!. Hivyo nikajua siwezi tena kuendelea na utangazaji, by that time nikiwa tayari ni mwana jf, nikaona tangazo fulani la kazi humu jf, nikaomba.

Iterview ya kwanza ilifanywa Radar. Jamaa wakaniita kwenye oral interview wakaniambia nina qualify ila nimeweka too high expectations kuliko matakwa ya muajiri, kama kweli ninaitaka hiyo kazi, nikubali kushuka kidogo!. Kwa vile nilikuwa desparete nilishuka!. Tulikuwa watu 20 ambao ni short selected, ndio tukaingia kwenye writen interview, walitupa several amptitude interviews za kupima IQ kwa kufanya mitihani mitatu timed test za 30 min each!. nilizipiga each for 20 minutes!. Matokea nikaambiwa ni mimi ndio niliongoza!.

Wakafanya final short listing tukabaki 6, ndio tunakwenda kwa wazungu!. Kati ya hao 6, wawili walikuwa Ph.D holders, watatu walikuwa na Masters, mimi peke yangu ndio nilikuwa na Ist degree!. Tulipigwa interview ya 1 hour each!, aliyeshinda hiyo job ni mimi!. From there kwanza nilimtafuta mode wa jf, na kuweka commitment ya kuichangia jf six figure each year!, its a commitment ninayoitekeleza mpaka kesho!.

After two years nikajikuta nina recover taratibu, nika realize licha ya paralysis, bado niliweza kutangaza. After two years, nikawaaga na kuendelea na kazi yangu ya kutangaza!, kwanza hawakuamini, mtu unaweza kuacha high profile well paying job kama ile!. Niliwaambia tuu kuwa I just opt to do what I love!, it makes me happy japo I don't make much kama ile job!. Sometimes its not about money, its job satisfaction!, I'm just on my own.

Nikijiuliza niliwezaje hayo!, nikagundua its work of powers, baada ya kuumia uoga wa nitaishije uka open up hizo powers, nikawapiga chini watu na Ph.D na masters zao, nikachukuliwa mimi.

Kuna kazi kibao naziona, well paying jobs nikizitaka nazipata just for a click of a finger, but don't attempt kwa sababu sipendi tena kutumwa!, najiuliza will this job make me happy?, jibu likiwa no, then I don't. Niliwahi kuuliziwa na master lobysit fulani kama niko interested kuupata U-DC akanilobie!, amini usiamini, nilisema no!, mimi niwe DC for what?!. Nilipomweleza mshahara niliouacha kwa wale wazungu, alafu nije niutafute U-DC, ingekuwa kichekesho!.

Pasco.
 
ha haaa Pasco ukitunga tu kitabu title
'namna ya kupata mwanamke yeyote unaemtaka bila jasjo'
utaendesha Range so soon lol

Exactly, yaani ajikite hapohapo ni ukweli ulio wazi atatengeneza fedha balaa.

Lakini pia nyakati hizo anazosema akimtizama msichana tu anamfuata angeamua kuutumia huo ujuzi kama mtaji leo akina Rahma al haroos au Madame matalent wangekuwa mikononi mwake na akila bila jasho jingi lol!! Lakini kwa sababu Pasco Msukuma mwenzangu utajiri ni ng'ombe na wake wengi akaishia 'kupiga' akina Mwajuma wa Magomeni!

Ila kwa ujumla anachokisema kina ukweli.........Kuna nguvu tunakuwa nayo alkini kadri muda unavyoenda ndivyo tunavyoipoteza. Mathalani nikiwa mdogo nilikuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi Watu walionizunguka, kwa mfano inawezekana miongoni mwa marafiki zangu ikaamuliwa twende sehemu A lakini mimi sijaridhika, nikiamua ndani ya kichwa changu kwamba tutaenda sehemu B nikifunua kinywa changu lazima nitabadili tu maamuzi yao tena hata bila nguvu wala hoja ya maana sana.

Kaka yangu nyakati fulani akiwa 'managerial position' alifanyiwa vitimbi vingi ndani na nje ya Kampuni ili apoteze nafasi yake lakini aka-survive, na ukitazama 'package' iliyokuwa ikipelekwa kwenye Board unashangaa aliweza vipi kuchomoka, na si hapo tu ni sehemu kadhaa alizopita.......................Siku moja kuna mtu alimuuliza, akajibu kwa namna tofauti kwamba kuna watu wana kitu kinaitwa "tough guy" ndani yao unaweza ukafanya yoote lakini wanajua mlango wa kutokea kabla hata hamjakamilisha mipango.

Wakati mwingine nawaza labda pengine nguvu kama hizi hupungua ama kuisha kwa sababu ya hizi dhambi tunazozifanya!

Further:
Pasco Na wale waopiga ramli unaweza kuwaelezea kidogo. Tunaambiwa anaweza kukueleza mambo yoote uliyopitia na yale yanayokuja!!
 
ha haaaa kwa target zako naona ungekuwa wewe ungeenda
kumuoa binti wa Dangote kabisa lol
 
Uzi huu umenivuta kutaka kujua zaidi,hasa hapo kwenye ndoto,mara nyingi kila niliotalo hutokea ni nini hii?msaada zaidi,hrf sijui vizuri kingereza sa pale ulipomwaga ngeli umeniacha.nahitaji msaada zaidi,na swali je!hapo hakuna uhusiano wa kiimani za kidini kama vile maono au kuongozwa na roho mtakatifu?na nini imani yako khs imani za dini?hapa niko njiapanda huwa sijui huku ni kuongozwa kwa nguvu za mizimu au nguvu za mungu?leo nikutana na nguvu zilizo ndani yetu?
Mkuu Slow, Mungu alipomuumba Adam, alimpa uwezo!. Yesu alipokuja alifanya miujiza, na kila muujiza alisema "imani yako ndiyo imekuponya!", kasome Marko 10 : 52 - Yesu akamwambia, \"Nenda, imani yako imekuponya, na Mathayo 9:22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu;imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile, au [h=3]Luka 17:19 "[/h]Akamwambia, ``Inuka, uende; imani yako imekuponya..hiyo imani yako ndio "powers from within!". Akasema laiti watu wangekuwa na imani kama punje ya haradali, wangeiambia milima ondoka!, na milima ikahama!", ina maana hizi imani tunazotumia ni ndogo tuu kama mbegu ya mchicha!.

Shetani pia ana powers, ikumbuke hapo mwanzo shetani ndiye aliyekuwa malaika mkuu, alipoasi, alifukuzwa ila hakunyang'anwa zile powers, ndiye aliyemrubuni Eva kule lile "tunda!". Nguvu za shetani hufanya maovu, nazo pia zimo ndani yetu kama hizo nguvu za Mungu!.

Kitendo cha kuamini, ni kufungua tuu milango. Mimi ni Mkristu Mkatoliki, kwa sababu nimezaliwa huku. Wengi hufuata imani fulani kwa kujikuta ndiko walikozaliwa na wanaendelea kujifungia humo humo kwa kuto look beyond!. Nilipokuwa India, nikasoma kidogo imani za Hindu ndipo nikagundua kumbe Christianity ni dini ya juzu juzi tuu, kwa taarifa tuu, dini za kale zaidi ni shamanism na animism, ambazo zilikuwepo miaka 300,000 kabla ya Kristu ila baadae zilifutika!. Kwa sasa dini ya kale zaidi iliyopo ni Hinduism ikifuatiwa na Buddhism zote za India ndipo ikaja Judaism ya Mashariki ya Kati, Israel, ikaja Taoism ya China na Shitoism ya Japan ndipo ikaja Christianity!. Hapo dini zetu za asili, hazitajiwi kabisa kwa sababu hazikuandikwa!.

Uki take time kutoka nje ya box la Ukristu au Uislamu ambamo ndiomo wengi wetu tumejifungia humo, ukachungulia ndani ya Hinduism au Buddhism, ndiko utakutana na real powers za "enlightenment!", kwa sababu dini hizi zinaamini kwenye "higher powers" bila kumtaja Mungu, Ukristu na Uislamu umezifungia milango, ili ukifuatilia uthabiti wa imani, discpline, na nguvu za kusali, utagundua sisi Wakristu na Waislamu tunatania tuu!.

Kiukweli ukizama sana kwenye hizi powers, unaweza kuingia kanisani na kujikuta unashutukia jinsi watu wanavyofungwa kamba, unaweza ukaacha kwenda!. Mimi bado ni Mkatoliki Die hard japo kuna mambo tunafanya ndivyo sivyo, ukishayangundua, unaachana nayo, bali unaendelea kuenenda kanisani kwa kufuata mafundisho ya Biblia na sio lazima yale yote ya kanisa ambayo umeisha yastukia kuwa sio!.

Wengi wakistuka, huamia makanisa ya wakovu, huko pia huwa nina hudhuria Mama yangu ni Esemblies og God, huko nako ndiko sio tuu unakuta kamba nene, bali watu wanapurushwa na kukamuliwa mpaka wanabaki mifupa!. Wale Wachungaji wameishajistukia jinsi ya kutumia hizi powers kucontrol waumini wao!. Wale wanaopataga mwanga hustuka na kujihamia kimya kimya, wengine wenye imani upofu, ni watumwa wa Wachungaji wao na wachungaji hao huwafanya lolote ikiwemo kuwa nani hii wake zao!, wao wakijua ndio baraka zenyewe kumhudumia mtumishi wa Mungu!.

Bwana wetu Yesu Krisu alisema wazi, watakuja watu, watahubiri kwa jina langu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!. Ukifuatilia sana the working of powers, unaweza kuogopa kuendelea ku practice, ila ukiisoma vizuri Bibilia, utagundua mahali mengi pameandikwa "nguvu imo ndani yako"!. Mungu alituumba kwa mfano wake, na katupa nguvu ambazo ndizo hizo powers from "within".
Pasco.
 
Kwa kuanzia inabidi upate mwalimu kuna temple moja pale karibu na makaburi ya Muhimbili wanakuwa na meditation sessions kila week waweza fikra pale

Kama unataka kufanya mwenyewe nitajaribu kukutafutia vitabu, kwakuwa kuna mengi ya kufanya kuanzia mavazi lishe vinywaji nk nk kwa mfano kwenye mavazi: Nguo za kubana sana si nzuri, chakula mara nyingi linatakiwa kiwe cha asili na fresh kisiungwe sana ,Epuka vyakula, vya supermarket , soda na hz juice za viwandani vyote c vizr kwa afya ya akili kuna mengi ya kufahamu, kukaa kulala kutembea ni mengi

Mkuu nashukuru sana, nitafuatilia kwa ukaribu, na naomba utuwekee vitabu hapa.

Wakati nasoma, yupo mwalimu wangu wa philosophy taught us abt mediation, hyponotation, akatufundisha namna ya kutengeneza subliminal massages but it was just th tip of ice bag.

All those things nlifundishw kw introduction, jana Pasco alivyoweka huu uzi nkaanza kukumbuka kuwa my teacher mentioned about the power within human being (na he spoke of mediation and yoga)

CC Pasco
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Slow, Mungu alipomuumba Adam, alimpa uwezo!. Yesu alipokuja alifanya miujiza, na kila muujiza alisema "imani yako ndiyo imekuponya!", kasome Marko 10 : 52 - Yesu akamwambia, \"Nenda, imani yako imekuponya, na Mathayo 9:22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu;imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile, au [h=3]Luka 17:19 "[/h]Akamwambia, ``Inuka, uende; imani yako imekuponya..hiyo imani yako ndio "powers from within!". Akasema laiti watu wangekuwa na imani kama punje ya haradali, wangeiambia milima ondoka!, na milima ikahama!", ina maana hizi imani tunazotumia ni ndogo tuu kama mbegu ya mchicha!.

Shetani pia ana powers, ikumbuke hapo mwanzo shetani ndiye aliyekuwa malaika mkuu, alipoasi, alifukuzwa ila hakunyang'anwa zile powers, ndiye aliyemrubuni Eva kule lile "tunda!". Nguvu za shetani hufanya maovu, nazo pia zimo ndani yetu kama hizo nguvu za Mungu!.

Kitendo cha kuamini, ni kufungua tuu milango. Mimi ni Mkristu Mkatoliki, kwa sababu nimezaliwa huku. Wengi hufuata imani fulani kwa kujikuta ndiko walikozaliwa na wanaendelea kujifungia humo humo kwa kuto look beyond!. Nilipokuwa India, nikasoma kidogo imani za Hindu ndipo nikagundua kumbe Christianity ni dini ya juzu juzi tuu, kwa taarifa tuu, dini za kale zaidi ni shamanism na animism, ambazo zilikuwepo miaka 300,000 kabla ya Kristu ila baadae zilifutika!. Kwa sasa dini ya kale zaidi iliyopo ni Hinduism ikifuatiwa na Buddhism zote za India ndipo ikaja Judaism ya Mashariki ya Kati, Israel, ikaja Taoism ya China na Shitoism ya Japan ndipo ikaja Christianity!. Hapo dini zetu za asili, hazitajiwi kabisa kwa sababu hazikuandikwa!.

Uki take time kutoka nje ya box la Ukristu au Uislamu ambamo ndiomo wengi wetu tumejifungia humo, ukachungulia ndani ya Hinduism au Buddhism, ndiko utakutana na real powers za "enlightenment!", kwa sababu dini hizi zinaamini kwenye "higher powers" bila kumtaja Mungu, Ukristu na Uislamu umezifungia milango, ili ukifuatilia uthabiti wa imani, discpline, na nguvu za kusali, utagundua sisi Wakristu na Waislamu tunatania tuu!.

Kiukweli ukizama sana kwenye hizi powers, unaweza kuingia kanisani na kujikuta unashutukia jinsi watu wanavyofungwa kamba, unaweza ukaacha kwenda!. Mimi bado ni Mkatoliki Die hard japo kuna mambo tunafanya ndivyo sivyo, ukishayangundua, unaachana nayo, bali unaendelea kuenenda kanisani kwa kufuata mafundisho ya Biblia na sio lazima yale yote ya kanisa ambayo umeisha yastukia kuwa sio!.

Wengi wakistuka, huamia makanisa ya wakovu, huko pia huwa nina hudhuria Mama yangu ni Esemblies og God, huko nako ndiko sio tuu unakuta kamba nene, bali watu wanapurushwa na kukamuliwa mpaka wanabaki mifupa!. Wale Wachungaji wameishajistukia jinsi ya kutumia hizi powers kucontrol waumini wao!. Wale wanaopataga mwanga hustuka na kujihamia kimya kimya, wengine wenye imani upofu, ni watumwa wa Wachungaji wao na wachungaji hao huwafanya lolote ikiwemo kuwa nani hii wake zao!, wao wakijua ndio baraka zenyewe kumhudumia mtumishi wa Mungu!.

Bwana wetu Yesu Krisu alisema wazi, watakuja watu, watahubiri kwa jina langu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!. Ukifuatilia sana the working of powers, unaweza kuogopa kuendelea ku practice, ila ukiisoma vizuri Bibilia, utagundua mahali mengi pameandikwa "nguvu imo ndani yako"!. Mungu alituumba kwa mfano wake, na katupa nguvu ambazo ndizo hizo powers from "within".
Pasco.

Mkuu pasco, unanifanya naconcentrate kupita kiasi.

Mimi kuna wakati naamini kuwa sisi (binadamu) ni miungu pia, kwa sababu katika kitabu cha Mwanzo kinaelezea kuwa tumeumbwa kwa mfano wa mungu (from this point we ar just a copy) then if yo go to Luke chapter 17 smthing like 21st vers anasema "and thy kingdom of God is within you"

Na ukifuatilia mazungumzo ya Yesu as u ve be tryn to show us alikuwa anademand "Imani" ilifika mahali akasema kama ukiwa na imani hata kama chembe ya haradani unaweza kuambia huu mlima ung'oke ukajitose katika kilindi cha bahari.

Huwa nataka nijue ni vitu gani hasa vinaweza kukufanya imani yako ikakua??
 
Lakini pia nyakati hizo anazosema akimtizama msichana tu anamfuata angeamua kuutumia huo ujuzi kama mtaji leo akina Rahma al haroos au Madame matalent wangekuwa mikononi mwake na akila bila jasho jingi lol!! Lakini kwa sababu Pasco Msukuma mwenzangu utajiri ni ng'ombe na wake wengi akaishia 'kupiga' akina Mwajuma wa Magomeni!
Mkuu Plato, kiukweli kuna wakati, niliutumia vibaya, concentration was only the number, na gratification ni kuwa na "hapa nilipita!", nilijikuta kuna sehemu, ni beauty queen wa kutisha, figure, figure, shape, shape, sura, sura, leggy line mwisho!, nywele mpaka mabegani, kwa kufupi kama ameshushwa, hakuumbwa!, kuja kupita, unakutana na kipande cha mua cha juu!, unabaki ukijiuliza "hivi huyu mume wake anapata nini?!, kuna watu wanaoa tuu sura au figure, furaha yao ni vile tuu vya kuonekanika ila in reality they get nothing!.
Wakati mwingine nawaza labda pengine nguvu kama hizi hupungua ama kuisha kwa sababu ya hizi dhambi tunazozifanya!
Hili ni kweli kabisa!, kadri unavyofanya dhambi nguvu hizi zinapungua kwa utaratibu unaitwa "karma", ukifanya dhabi nyingi, unakuwa na bad karma!. ukitenda mema unakuwa na "good karma", ukiwa na bad karma sio tuu nguvu zinapotea, bali pia mabalaa yanakuandama!. Kwenye ulimwengu wa "powers", hakuna bahati mbaya!, kila kinachokutokea ni "premeditated move" kilikuwa kitokee, ni jukumu lako kuwa "enlightened kuzuia mabaya yasitokee!". Na mabaya yakikkuta, ujue una fidia tuu yale uliyoyatenda!".
Further:
Pasco Na wale waopiga ramli unaweza kuwaelezea kidogo. Tunaambiwa anaweza kukueleza mambo yoote uliyopitia na yale yanayokuja!!
Yes wapiga ramli pia ni powers, wako kwenye makundi haya ya Psychometry or psychoscopy -. wanajifanya waganga kupata taarifa za watu. Clairaudience - wanachukua taarifa toka marehemu kwa kujidai wanazungumza na mizimu!. Clairvoyance, second sight - ni mtu kuzungumza au kuwasiliana na wafu wanaikujua, hawa hujiita medium!. Death-warning - ni uwezo wa kukiona kifo kinakuja kabla hakijafika hivyo unaweza kukizuia kama saa yako haijafika!. Divination - ni kuwa na powers za kwenda kuangalia kijiji kwako mambo vipi?. Dowsing - ni uwezo wa kugundua a ku trace kitu kilichopotea au chenye thamani, yule Myahudi Uri Geller aliutumia uwezo huu kugundua sehemu zenye mafuta, kwa malipo ya per cent fulani, sasa ni tajiri mkubwa!. Scrying - ni wale wanaojifanya kutumia televisheni ya sili kukuonyesha mahali etc.

Nilisema hata wanga, waganga, walizi, wachawi hutumia nguvu hizi!. The dividing line baina ya zipi ni nguvu za Mungu na zipi ni za Sgetani au nguvu za giza is very thin!, ninachozungumzia humu ni "use of powers from within!".
Pasco.
 
Back
Top Bottom