Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Wanabodi,
Kwa kuanzia naileta tuu kwanza hii hoja hapa, ikipata watu wa kutosha,
tutaomba kwa mode, ifunguliwe jukwaa lake, tutalitafutia jina muafaka,
mfano, "Miujiza ya Ukweli!".

Kitu chenye nguvu kabisa katika mwili wa binadamu ni nguvu inayoitwa
"Will Powers" ambayo kila binadamu, anazaliwa nayo, ila wengine
wanabahatika kwa nguvu hizo kujionyesha bayana, huku wengine wengi
wakiwa nazo bila kujijua kuwa wanazo nguvu hizo!.

Wale wahubiri wafanya miujiza ya uponyaji, wote wanatumia nguvu hizi,
kufanya hayo wanayoyafanya, ila pia, wanga, wachawi, waganga, watabiri,
wavumbuzi, matajiri wa kutisha, watawala wenye nguvu, nao pia hutumia
nguvu hizi kupata mafanikio makubwa katika maisha yao!.

Matumizi ya neno "Katika Jina la Bwana", "Yesu", "Mungu" au jina lolote
utakalotumia, ni kiashiria tuu cha kuufungua mlango wa nguvu hizo, ili
ziweze kutenda miujiza, hata wasiotumia majina hayo, au maneno hayo
huweza kutenda miujiza!.

Matumizi ya nguvu hizo, yanapotumika kutenda mema, huitwa nguvu za
"Mungu", "Yesu", au "Roho Mtakatifu", na nguvu hizo zinapotumika kutenda
maovu kama uchawi, majanga, magonjwa, etc huitwa "Nguvu za giza!".

Kwa vile nguvu hizi kila mtu anazo, hata hao wanaofanya miujiza ya
uponyaji, wanachofanya ni kufungua tuu milango, ili nguvu zilizo ndani
yako, ziweze kutenda hiyo miujiza, na ukipona, kilichokuponya sio huyo
mponyaji, wala lile jina la Yesu, au jina Mungu, bali ni nguvu zilizo
ndani yako!, "the powers from within!".

Hatua ya kwanza ya kufungua nguvu hizi ni "imani" kuamini kuwa "you have
the powers" and that "you can do anything!", or "you can be anybody".
Kuamini Mungu, Yesu, Mtume, Allah, Roho Mtakatifu, Bikira Maria,
Watakatifu, Wachungaji, Wahubiri, Baba Mtakatifu, Sangoma, Sheriffu,
Mlingotini, Chini ya Mti, Chini ya Mbuyu, Mlimani, Pangoni, Kisimani,
Mtoni, Ziwani, Kwa Mganga, Vitabu Vitakatifu etc, ni njia rahisi ya
kuanzia kufungua milango ya "higher power" to open up your doors for
powers from within!" to act on you for you!.

"I know I can, be what I wanna be!"

Wale wenzetu wajanja, waliojitambua kuwa wanazo, wengi wanazitumia
kutengezea mapesa kwa kisingizio chochote kiwe ni cha wahubiri, waganga,
"wazee wa busara", "watenda miujiza", "wafukuza mapepo" kwa kukusanya
sadaka na kujitajirisha, ambao mimi naita ni "wizi mtupu", huku waumini
wakendelea kukamuliwa na kuachwa katika umasikini uliotopea!.

Nguvu hizi zimegawanyika matika makundi mengi tofauti, hivyo nimekuwekea
baadhi ya makundi hapa chini, just take your time kuyatambua,
ujiangalie na wewe unazo nguvu zipi, ili sasa uzitumie nguvu hizo, to
"make things happen!".

This is a list of
psychic abilities that
have been attributed to real-world people. These are also sometimes
known as
extrasensory
perception
or a sixth sense. Inclusion in this list does
not imply scientific recognition of the existence of an ability.
Superhuman
abilities from fiction
are not included.

 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu Pasco, kipindi fulani katika maisha yangu nilitamani sana kujifunza uchawi mwenye tija, nikajikuta nimeangukia kwenye temple moja south Africa iliyokuwa inafundisha Buddhism Yoga meditation na supernatural powers

Yalikuwa ni masomo magumu ya ajabu na yenye kushangaza kwa jinsi yake, kwa ufupi ni kwamba hakuna chenye nguvu duniani kama bongo(mind) ya binadamu, na tunachokitumia katika mind zetu ni theluthi tu ya kile chote kilichopo

Tunafundishwa kuwa kuna 5senses, lakini Zipo 8 ambapo mtu ukiweza kuzifanyia kazi utafanya maajabu mengi , mind ya mwanadamu imejazwa takataka nyingi mno, illusions na dillusions ukiweza kuziondoa kwenye bongo yako ukabaki na pure and stable mind unakuwa mtu mwingine kabisa mwenye maono na nguvu za ajabu mno

Medition ni kitu cha Mwanzo kabisa kuendea kwenye kudevelop supernatural powers, nilifanya meditation zote, chanting, yoga nikiwa vegitarian kwa miaka mitano nikajikuta nabadilika nikaogopa nikaacha , kwakuwa niliona wazimu kuna mafundisho yanapingana waziwazi na imani yangu

Nimeipenda mada yako sana. Nakaribisha maswali na ufafanuzi nimeisoma sana Buddhism, Taiosm, Satanism na Kshna consciousness

Mwenye kupenda hii mambo atafute kitabu kiitwacho Analects: Way and Its Power.
Mkuu Mshana,
Nakubaliana na wewe, hata mimi kuna wakati niliishi India, nikasoma sana buthiism, na ku practice ayuverda na pranayaana hivo nika turn vegetarian, pia nimemsoma sana krishna, niliporudi bongo, nikajikuta nashindwa ku mix na watu wangu!, kwanza nilianza kuirudia wine, kisha kuendelea kupiga kinywaji na hatimaye kurudia nyama!.

Wakati wa practive ni kweli nilikuwa poweful, nikajikuta badala ya kuishi kwa raha kufuation high state of alert, unajikuta unaishi kwa mateso, mathalan unagundua baadhi ya watu waliokuzunguka wako kinyume na wewe!, au kuna hiyo siku wife alitoka party ya kazini, sixth sense imekuambia mwenzako "tayari" ili kukuzuga, ajajifanya yuko "high!" akihitaji huduma!. "Mzee" aligoma! lakini aliamshwa!, na kwenye "game" ilibidi ajitahidi sana na ku fake "kufika" mapema kuliko kawaida!. Kupitia mazoezi hayo, unaweza kudistinguish "kufika" kweli na "kufika" fake ili kunizunga!.
Unakuja ile genuine trust, love na happyness inayeyuka kwa kujua you are cheated!.

Hivyo info nyingine unaachana nazo for love peace of mind and tranquility ya mahusiano!.

Ndio maana ukiwachunguza matajiri wengi, utagundua they are not real happy!. Unaweza kuwajua kwa kuwatazama machoni!. Nimejiamulia bora kubaki masikini happy kuliko tajiri huzuni!. Na sometime ukifuatilia life stily za hao matajiri, licha kula dinner Kempinsky, hawa enjoy kama sisi tunakula chips vumbi!.
Wee acha tuu!.
Pasco.
 
Uzi huu umenivuta kutaka kujua zaidi,hasa hapo kwenye ndoto,mara nyingi kila niliotalo hutokea ni nini hii?msaada zaidi,hrf sijui vizuri kingereza sa pale ulipomwaga ngeli umeniacha.nahitaji msaada zaidi,na swali je!hapo hakuna uhusiano wa kiimani za kidini kama vile maono au kuongozwa na roho mtakatifu?na nini imani yako khs imani za dini?hapa niko njiapanda huwa sijui huku ni kuongozwa kwa nguvu za mizimu au nguvu za mungu?leo nikutana na nguvu zilizo ndani yetu?
 
Asante sana Pasco kwa mada hii.Hili ni jambo ambalo limenitatiza kwa muda mrefu na nimekua nikitamani nifungulie nguvu hizi lakini bado sijafika huko.Nimesoma sana kuhusu haya mambo na ninashukuru kupata kitabu cha The Master Key hiki ndicho kilichonitambulisha kwenye ulimwengu huu.

Ninaendelea kujisomea kila siku na sasa nimejikita kwenye maandiko ya Tibet hssa hasa mafundisho ya Atisha.Ninatumaini nitagika huko ninakokutazamia kwa maana yote haya ni nguvu ya Mind.
 
Pasco hebu nijibu hili swali

watu huwa 'wanaibiwa ' huu uwezo?

manake mimi zamani nilikuwa na uwezo wa ajabu wa mambo meengi mno

now naona kama kuna mtu ameniibia hayo mambo,
je nifanyaje?

The Boss kama nimesoma kwa usahihi kwenye The Book of Wisdom ya Osho,Inasemwa ya kwamba nguvu hizi ni vigumu sana kuzitambua kama uko nazo lakini ni rahisi sana kuzipoteza.Mara nyingi kinachofanya nguvu hizi zikimbie ni Ego..yaani mtu akishaacha kuwa Aware (awareness ni
jambo la muhimu kulifahamu) na kuanza kutumia Ego basi ngivu hizi zinapotea kama zimechukuliwa na upepo wa kisulisuli.Ni sawa tu na wale ambao wanaifungua ile Lotus ya Kundalini vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Pasco hebu nijibu hili swali

watu huwa 'wanaibiwa ' huu uwezo?

manake mimi zamani nilikuwa na uwezo wa ajabu wa mambo meengi mno

now naona kama kuna mtu ameniibia hayo mambo,
je nifanyaje?
Mkuu The Boss, hakuna aliyekuibia, hizo powers bado zipo na unazo, ila zimekuwa dormant kwa sababu hazikutumika!.

Kama nilivyosema mwanzo, kila mtu anazaliwa nazo!, infact zinaanza ku exist since the time of conception!. Ndio maana mtoto akiwa tumboni, unashauriwa zungumza nae, mwambie unampenda!, mkeo akiwa mja mzito, sometimes shika shika tuu tumbo la wife ongea na mtoto kuwa nnamsubiri kwa hamu!.

Baadhi ya watoto ambao mimba zao zilitaka kutolewa zikagoma, wanajua!, hivyo wanakuwa wamezaliwa huku subconcious ikiwaambia "they were rejected!". Letter in life, wanakuja kuwa ma psychopath kwa kufanya mambo ya ajabu, ikiwemo hata kuwa serial killer!, by the time wanayafanya hayo matendo, wanakuwa sio wao, ni sub concious mind yao inakuwa imetake charge, normal concious ikirudi, wanajuta!.

Mtoto akishazaliwa powers zinakuwa very distinct!, mara kibao anaweza kuanguka toka kitandani, akalia tuu ila kiukweli anakua hajaumia kabisa, kihivyo!. Mtoto mchanga akikuangalia anakusoma your mind, kama unampenda anaona, kama unamchukia anajua, anasikia japo hawezi kusema!, ndio maana wakija wachawi anawaona, au akija mtu mbaya, mtoto anastuka analia.

Kadri unavyokuwa, ndivyo powers hizi zinakwenda zikipungua mwisha zinapotea kutokana na kutotumika!.

Mfano mimi nayakumbuka baadhi ya majina ya baadhi ya wanafunzi niliosoma nao nursery school. Nilisoma shule ya St. Petrers Kindagarten Tanga nikiwa just 4 years!, Mpaka leo nayakumbuka baadhi ya majina-Robert Kilala na Ana Kilala, walikuwa wanaletwa shule na baba yao kwenye pikipiki. Kuna David Naburi, Alex Shaba, Jane Mutayoba, Cecilia Minja, na kuna drama nilicheza shule mimi nilikuwa King!. Bado nakumbuka nyimbo za Baba Black sheep etc!.

Lakini cha ajabu, siwakumbuki wanafuanzi niliosoma nao darasa la kwanza na la pili pale Nyanza Mwanza zaidi ya Leonard Mpupua n.a. wimbo wa "sasa sasa saa ya kwenda kwetu!". Na huwezi kuamini, kuna watu nimemaliza nao chuo pale UDSM, wao ndio wananikumbuka kuwa tumesoma darasa moja!.

Ili kwa mujibu wa michango yako humu jf, Mkuu the Boss, unajulisha wazi, "you have the powers!", issue ni kuzifuatilia tuu na kuzifufua!. Ila kama hizo powers ni strange powers, bora ziache tuu ili uishi normal life!.
Pasco.
 
Mh hapa sasa ndio penyewe nimekua nikifanya kitu nahisi kama kuna siku nilishakifanya lakin tatizo sikumbuki ni wapi na lini kwa mfano naweza kukutana na mtu popote pale iwe njiani au kwenye gari na tukianza kupiga piga stori nakuwa kama napata picha ya hayo tunayozungumzia yalishapita lakini kiuhalisia haijawahi kutokea, hapa nitakua katika kundi gani mkuu Pasco
 
Last edited by a moderator:
Pasco huo uwezo wa 'kata funua' bila kusema neno sipati picha
hizo pm za watu uwafundishe utakazopata lol

kikazi je uwezo ako ulikusaidia kupata kazi? kazi ipi kwa mfano?

Na wabongo tunavyopenda habari kama hizi na kwa uwezo wa Pasco kujieleza, akiamua anaweza kuwa milionea kwa muda mfupi sana though anachoeleza kina make sense.
pasco dunia ni yako chaguo ni lako, amua kuendesha Range Rover leo!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Mshana,
Nakubaliana na wewe, hata mimi kuna wakati niliishi India, nikasoma sana buthiism, na ku practice ayuverda na pranayaana hivo nika turn vegetarian, pia nimemsoma sana krishna, niliporudi bongo, nikajikuta nashindwa ku mix na watu wangu!, kwanza nilianza kuirudia wine, kisha kuendelea kupiga kinywaji na hatimaye kurudia nyama!.

Wakati wa practive ni kweli nilikuwa poweful, nikajikuta badala ya kuishi kwa raha kufuation high state of alert, unajikuta unaishi kwa mateso, mathalan unagundua baadhi ya watu waliokuzunguka wako kinyume na wewe!, au kuna hiyo siku wife alitoka party ya kazini, sixth sense imekuambia mwenzako "tayari" ili kukuzuga, ajajifanya yuko "high!" akihitaji huduma!. "Mzee" aligoma! lakini aliamshwa!, na kwenye "game" ilibidi ajitahidi sana na ku fake "kufika" mapema kuliko kawaida!. Kupitia mazoezi hayo, unaweza kudistinguish "kufika" kweli na "kufika" fake ili kunizunga!.
Unakuja ile genuine trust, love na happyness inayeyuka kwa kujua you are cheated!.

Hivyo info nyingine unaachana nazo for love peace of mind and tranquility ya mahusiano!.

Ndio maana ukiwachunguza matajiri wengi, utagundua they are not real happy!. Unaweza kuwajua kwa kuwatazama machoni!. Nimejiamulia bora kubaki masikini happy kuliko tajiri huzuni!. Na sometime ukifuatilia life stily za hao matajiri, licha kula dinner Kempinsky, hawa enjoy kama sisi tunakula chips vumbi!.
Wee acha tuu!.
Pasco.

Kama sijakuelewa hivi, ina maana matajiri wote lazima wawe na huu uwezo.?
 
Back
Top Bottom