diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
NI neema tupu: Hivi ndivyo unavyoweza kueleza baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kuanza kulipa wastaafu tofauti ya fedha iliyokuwa haijalipwa kutokana na matumizi ya kikokotoo kipya.
Kanuni hizo zilianza kufanya kazi Agosti mwaka jana, baada ya marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii iliyounganisha mifuko wa PSPF, PPF, LEPF na GEPF na kuunda mfuko wa PSSSF. Watumishi waliostaafu kuanzia Agosti mosi, mwaka jana walilipwa mafao yao kwa kikokotoo kipya cha asilimia 25 na baada ya uamuzi wa Rais John Magufuli wa kurudisha kikokotoo cha zamani cha asimilia 50, wastaafu wa PSSSF wataanza kuongezewa walichopunjwa. Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Eliud Sanga, alisema wastaafu hao wanastahili kulipwa Sh. bilioni 119.
Alisema tangu kutolewa kwa agizo la rais Desemba 28, mwaka jana, walianza kuwatambua na kuwalipa wale waliopunjwa malipo ya mkupuo na wanaendelea kuwalipa. “Tulishaanza kuwalipa ile tofauti ya fedha ya asilimia 25 ili kutimiza asilimia 50 kwa mujibu wa kikokotoo cha zamani cha PSPF, tunaendelea kuwalipa kwa kadiri hadi tutakapomaliza,” alisema na kuongeza: “Agizo la rais ni la kutekeleza moja kwa moja halina kusubiri, nasi tulishaanza kuwalipa wastaafu.
wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, ni kuwa mfuko wa NSSF ambao ni kwa ajili ya sekta binafsi na PSSF zingelipa mafao kwa kikokotoo kimoja. Kikokotoo kilichokuwa kimependekezwa ni asilimia 25 ya malipo ya mkupuo, ambayo fomula yake ni moja ya 580 mara jumla ya mishahara mara mishahara minono ya miaka mitatu katika miaka kumi ya kukaribia kustaafu mara 12.5 mara asilimia 25. Pensheni ya kila mwezi ni moja ya 580 mara jumla ya mishahara mara mishahara minono ya miezi mitatu kwa miaka 10 ya mwisho ya mstaafu mara asilimia 75 mara 1/12.
Desemba 28, mwaka jana, Rais alikutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wakuu wa mifuko ya PSSSF na NSSF, Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira, na baada ya majadiliano ya muda mrefu alitangaza kufuta kikokotoo kipya na kutaka kila mfuko kurejea kwenye kikokotoo walichokuwa wanatumia kabla. Kwa mabadiliko hayo, NSSF itaendelea kutumia kikokotoo cha asilimia 25 kwa kuwa ndicho kilichokuwa kwenye kanuni za mwaka 2014 ambazo zilitumika kwenye mifuko yote. Kwa mabadiliko hayo kwa sasa kutakuwa na vikokotoo viwili ambavyo vinatofautiana miaka ya makadirio ya kuishi ikiwa ni NSSF miaka 12.5 na PSSSF ni miaka 15.5.