Castr
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 31,967
- 63,983
Urasimu kwenye hii nchi ni jangaHaya ndio ya kujadiliwa ili kuwasaidia watu kupata stahiki zao lakini cha ajabu nyuzi kama hizi hata michango inakuwa michache
Panapotokea mambo kama yakina lijualikali,sijui chadema kinajifia michango inakuwa kama yote..ikumbukwe ya kwamba hivyo vyama vina watu ambao ni wafanyakazi ambao ni wastaafu watarajiwa,kila siku tunaimba humu siasa ndio inayoamua hatma ya mfumo wetu wa kimaisha pamoja na waki-nchi.
PSSSF nanyi ni majipu,wengine mpaka leo tuna suffer kukamilisha taaratibu za kupata mafao yetu kwa tulioachishwa kazi,Mara lete barua ya mwanasheria yenye kuthibitisha kama hujapata kazi,sijui copy kitambulisho ipigwe muhuri wa mwanasheria,sijui andika barua kwanini mchango wako ulichelewa kuingizwa baada ya wewe kuanza kazi, basi tafrani tupu.
Kwa hili la wastaafu tafadhali wafanyie wepesi kupata stahiki zao,si mlikuwa mnasema kuwa tumeondoa fao LA kujitoa Pamoja na kutengeneza kikokoto kipya eti kisa mnatuonea huruma tukifika kuwa wazee tutateseka, Sasa wazee ndio hao wameshastaafu muwaone huruma kwa kuwalipa mafao yao.
Yaani hii nchi inataratibu za kishenzi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app