PSSSF ijitathimini kwa kutokulipa mafao kwa wakati

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,342
1,300
Jana kamati ya bunge imeitaka Psssf kujitathimini endapo Ina uwezo wa kulipa mafao ya wastasafu kwa wakati. Kuna uzembe Psssf kulipa mafao kwa wakati.

Wale waliokuwa kwa kanuni ya kikokotoo Cha 25% baadhi yao hawajalipwa mapunjo. Hotuba ya rais Magufuli 28/12/2018 alifuta kikokotoo hicho na kuagiza wastasfu wale walipwe mapunjo yao. Hadi Sasa bado wapo wastasfu wengi hawajalipwa mapunjo yao.

Ni muda Sasa waziri husika kufanya ziara kwenye ofisi za mfuko ili kujiridhisha na utendaji kazi katika mfuko mbali ya kutoa tu maagizo bila kufuatilia.

Tatizo Ni wastasfu kutokuwa na wafuatiliaji wanawawakilisha. Hivi Sasa ili update hela kwa wakati inabidi ufunge safari Hadi Dodoma kufuatilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale Lijualikali anapoenda kuishtaki CHADEMA polisi kutokana na kashkash alizopewa na polisi kwasababu ya CHADEMA.
 
Ila hali ni mbaya sana. Yupo mstaafu mama mmoja ametumikia taifa kwa uaminifu mkubwa na amestaafu hana vitu vya maana za nyumba aliyojenga kwa mikopo lakini mafao yake zaidi ya mwaka na nusu halipwi na mbaya zaidi hata fedha za kujikimu hajawahi kupata hata senti moja! Sasa anaishi kwa michango ya ndugu! Mtu aliyesoma vizuri enzi hizo na kutumikia taifa kwa uaminifu!

Tunajenga picha gani na mwamko gani kwa watu wanaomzunguka? Hivi hakuna hata utaratibu wa kusaidia hawa wazee? Mtu kila siku ni safari za kwenda kufatilia na anapewa majibu yasio na matumaini. Hivi kama kuna michango taasisi haijalipa inageuka kuwa deni la mstaafu wakati alikatwa kwenye msharaha wake? Hatari sana sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlipeni George Gerald Mwashimaha hela Yake, mmemsotesha sana
Bora umetaja jina. Yupo mstaafu mmoja wanamzungusha sana tena kwasababu ambazo hazimuhusu. Nakusanya evidence alafu nitatumia hadi PA ili wajue wanachofanya ni uhuni.

Wao wakistaafu wanaweza kuishi miaka miwili bila hata senti moja kulipwa? Wastaafu wananyanyasika sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa wanajua kutoa matamko ya kuchambana uchadema na uccm lakini huwezi kuona harakati halisi kama hizi. Kama mnapata nyaraka huko mafichoni si mpate na hizi za wastaafu wanaodai muda mrefu hawalipwi?

Tunatengeneza mafisadi wenyewe kwa mifano mibovu wakati wa kulipa wastaafu. Mnakataa kumlipa mstaafu kisa taasisi haijalipa baadhi ya michango, mnataka mstaafu afanye nini? Wakati alishakatwa kupitia mishahara yake. Aende na panga kwenye hiyo taasisi walipe?

Kumekuwa na hamasa watu binafsi kuchangia hii mifuko ya hifadhi jamii lakini wengi wanaogopa kutokana na trend mbovu ya kulipa mafao. Bila kujenga uaminifu hii mifuko itakuwa hatarini huko mbele.

Mifuko mingine wamekuwa na miradi ya hovyo kama alivyosema JPM na matokeo yake ni kuyumba na kusumbua wastaafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana kamati ya bunge imeitaka Psssf kujitathimini endapo Ina uwezo wa kulipa mafao ya wastasafu kwa wakati. Kuna uzembe Psssf kulipa mafao kwa wakati. Wale waliokuwa kwa kanuni ya kikokotoo Cha 25% baadhi yao hawajalipwa mapunjo. Hotuba ya rais Magufuli 28/12/2018 alifuta kikokotoo hicho na kuagiza wastasfu wale walipwe mapunjo yao. Hadi Sasa bado wapo wastasfu wengi hawajalipwa mapunjo yao.
Ni muda Sasa waziri husika kufanya ziara kwenye ofisi za mfuko ili kujiridhisha na utendaji kazi katika mfuko mbali ya kutoa tu maagizo bila kufuatilia. Tatizo Ni wastasfu kutokuwa na wafuatiliaji wanawawakilisha. Hivi Sasa ili update hela kwa wakati inabidi ufunge safari Hadi Dodoma kufuatilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazee wetu wanadai mafao toka 2017 mpaka leo wanahangaika utadhani ni mkopo halafu tunaambiwa Serikali ya kuwapigania Wanyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh ni hatari hawa watu.

Fomu imeandikwa kwa kiingereza anayetakiwa kuijaza alikua ni mfagiaji tu wa ofisi.

Yanarudishwa majibu kwamba hakuna uthibitisho wa mwajiri.

Uthibitisho unapatikana. Akili yangu inaniambia zoezi litaanzia lilipokwamia kutokana na kukosekana huo uthibitisho.

Kumbe nilikua siijui PSSSF.

Wakasema process nzima inatakiwa ianze mwanzo. Hapo hilo jibu limekuja baada ya miezi minne.

So process ikaanza mwanzo. Huu ni mwaka sasa tangu process kukamilika.

Na nikafikiri labda ni sisi tu.
 
Haya ndio ya kujadiliwa ili kuwasaidia watu kupata stahiki zao lakini cha ajabu nyuzi kama hizi hata michango inakuwa michache

Panapotokea mambo kama yakina lijualikali,sijui chadema kinajifia michango inakuwa kama yote..ikumbukwe ya kwamba hivyo vyama vina watu ambao ni wafanyakazi ambao ni wastaafu watarajiwa,kila siku tunaimba humu siasa ndio inayoamua hatma ya mfumo wetu wa kimaisha pamoja na waki-nchi.

PSSSF nanyi ni majipu,wengine mpaka leo tuna suffer kukamilisha taaratibu za kupata mafao yetu kwa tulioachishwa kazi,Mara lete barua ya mwanasheria yenye kuthibitisha kama hujapata kazi,sijui copy kitambulisho ipigwe muhuri wa mwanasheria,sijui andika barua kwanini mchango wako ulichelewa kuingizwa baada ya wewe kuanza kazi, basi tafrani tupu.

Kwa hili la wastaafu tafadhali wafanyie wepesi kupata stahiki zao,si mlikuwa mnasema kuwa tumeondoa fao LA kujitoa Pamoja na kutengeneza kikokoto kipya eti kisa mnatuonea huruma tukifika kuwa wazee tutateseka, Sasa wazee ndio hao wameshastaafu muwaone huruma kwa kuwalipa mafao yao.

Yaani hii nchi inataratibu za kishenzi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh ni hatari hawa watu.

Fomu imeandikwa kwa kiingereza anayetakiwa kuijaza alikua ni mfagiaji tu wa ofisi.

Yanarudishwa majibu kwamba hakuna uthibitisho wa mwajiri.

Uthibitisho unapatikana. Akili yangu inaniambia zoezi litaanzia lilipokwamia kutokana na kukosekana huo uthibitisho.

Kumbe nilikua siijui PSSSF.

Wakasema process nzima inatakiwa ianze mwanzo. Hapo hilo jibu limekuja baada ya miezi minne.

So process ikaanza mwanzo. Huu ni mwaka sasa tangu process kukamilika.

Na nikafikiri labda ni sisi tu.
Wahanga Ni wengi ukienda ofisini utatamani kulia Mara file linashughulikiwa ukienda Tena utaambiwa system hakuna saa zingine utaambiwa subiri mwezi ujao tuangalie.... Kero tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom