PSSSF haina value for money and time

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,395
512
Naomba PSSSF mpokee huu ushari. Ndani ya mfuko pawe vitengo viwili tofauti vyakushughulikia mafao. Mosi kitengo cha mafao ya kufukuzwa kazi na kukosa ajira na pili kiwe kitengo cha kushughulikia mafao ya waastaafu.

Ili linapokuja swala lakulipana kila kitengo kifanye kazi kwa haraka. Mfano, huyu wa kufukuzwa kazi, au kukosa ajira anamahitaji ja hana kipato kingine, basi muwayisheni malipo yake ili ajikimu na familia yake. Mukimucheleweshea, muna munathiri kifedha.

Ana madeni na huduna za kulupia. Munajua, katita utumishi, watu hawana akiba walio wengi. Walipeni kwa wakati na wao waweze kunya biashar na shughuli zingine zakuwaingizia kipato.

Aliyestaafu, mara moja anaanza kulipwa pensheni ya kila mwezi, huyu anauafadhali kuliko alive fukukuzwa au kukosa ajira. Tafadhali angalieni hill kwa jicho laki pekee.

Nikitu chaajabu sana munahitaji wateja, wakati huohuo, huduma kwa mteja ni hafifu anapokumbwa na tatizo. Kwa mwenendo huu mutakosa wateja, huduma zenu kiwe kielelezo tosha cha kuwavutia wateja. Badilikeni PSPF a.k.a PSSSF.
 
Dodoma, wameanza tangu mwezi wa nane. Visingizio ni kuangisha mifuko sijui nini? Visababu vya chini kabisa. Nafikiri walikua wanaweka mifumo yao sawa kabla ya tarehe moja August, ili wakianza wameanza. Kwahio walikua wanafanya mini kabla ya mwezi wa nane. Huu ni uzembe na usumbufu kwa wateja. Kabla ya kuanza fumo, inakua tayari mmeshaanda kila kitu, ili munapo badili, ni kitendo cha kuzima hushoto nakuwasha Julia na kazi zinaendelea bila kuathiri huduma kwa wateja. Ni shiiiidaaaah kweli!
 
Mimi kwenye kanuni zao kifungu cha 8(2)(3)(4) ninahitaji ufafanuzi. Nilienda kwenye ofsi zao wakaniambia hata wao hawajapewa semina na hicho kifungu kina watatiza sana. Kwa sababu humu kuna wanasheria naomba anaeweza kufafanua kifungu hicho atufafanulie.
 
Hivi ilikuwa ni lazima hilo litaasisi liwe na lijina lirefu namna hiyo? Eti "PSSSF" kweli hii lugha ilikuja na meli
 
Ndo uone usumbufu utaoka kuwepo. Kama watumishi ndani ya PSSSF hawaelewi vifungu, how will a layman or woman know. Usani na ulaghai kwa wateja. Sijui wanatamaa sana na hela za wateja? Mbona kulipia miradi yao hela inatoka, Ila kulipa wateja hela inakua hamna, na kuzungushana sana.
 
Mtu ametumikia taifa kwa zaidi ya miaka 30 kisha unampa asilimia 25 ya mafao yake. Mbona huu ni wizi na uonevu? Wastaafu wengi watakufa kabla ya siku zao kwa pressure, stress na mawazo. Sere=kali isichezee hela za wastaafu, jasho la mtu haliliwi bure. Mungu atawafuatilia kwa laana hii vizazi na vizazi maana malalamiko ya wastaafu hayataenda bure. Sijui tunaelekea wapi Tanzania.
 
Haya mashirika ni manyonyaji ya karine hii ya 21. Hayana huruma na wanachama wao. Kwanza wanajua fika kwamba mishahara yao ni kiduchu na haiongezeki. Maisha wanayoishi watumishi kwakweli ni ya kishetani kabisa. Hayana staha! Leo akiachishwa kazi au kustaafu kupata stahiki zake ni usumbufu wa hali ya juu.kupigwa tarehe kila siku, wakati wao mishahara inaingia. Sasa unashanga hela zinaenda wapi? Wao wanalipana mishahara minono kweli, michango kila mwezi, kuwalipa watu kwa wakati ni tatizo, basi haina maana yakua na mifuko kama hii. Mfuko huu unapashwa kua mfano wa weredi yaani(professionalism) ya hali ya juu. Ndani ya wiki, mtu keshapata hela yake. Leo kufukuzwa kazi au kustaafu limekua gumzo pamoja nakupata fedha yako.
Wanakuza sana mtaji, Ila mwenye mtaji anapata riba kiduchu. Wizi wa mchana kweupe. Badilike PSSSF na mdogo wako NSSSF
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom