PSSSF haina ufanisi katika kulipa mafao kwa wakati. Maana ya Rais kuunganisha mifuko haionekani

kitimtim

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,600
1,921
Yaani malipo ya wateja ni delays ambazo hazieleweki, ni majuto kufanyakazi na hawa watu kweli, wako na visuti na tai humo efficiency chini kabisa, bado tunapiga hesabu, tunasubiri baada ya uchaguzi, tunalipa kwa awamu hii inamuhusu mteja au big results ndo failure.
 
Hela zote zimeingizwa kwenye miradi kama manunuzi ya ndege, SGR nk. Hamna hela kwenye hiyo mifuko boss. Nyingine ndio hizo watu wanagaiwa cash barabarani kwenye ziara za yesu. Lengo la kuunganisha hiyo mifuko ilikuwa ni kurahisisha uchotwaji wa hizo hela. Na usitegemee ufanisi wa hiyo mifuko, maana biashara ya ndege ina changamoto kubwa.
 
Mwakani serikali itachota tena pesa nyingi Kwenye mifuko ya hifadhi kwajili ya kununua ndege 5...
Kuna Sheria zingine zinakuja kupitishwa na Bunge February mwakani juu ya hizi pesa za Kwenye mifuko
 
Hii mifuko ni kichomi kilichokomaa usipokuwa na roho ngumu kipindi unadai chako either utaipata pressure ama hata kufa kwa sonona.
 
Psssf wanatesa sana wastaafu,miaka 4 mafao ni kuzungushana tu.

Wanasema wanasubiri rais asaini ili pesa ilipwe kwa wastaafu.
 
Back
Top Bottom