PSPF,mfuko pekee wa pensheni unaoweka mazingira ya wazi ya rushwa kutoka kwa wanaodai mafao!

PSPF ndo mfuko unatoa mafao bora kuliko mifuko yote. Mimi babangu ni mstaafu wa PSPF.
Wastaafu wa PSPF Wanalipwa pensheni mara mbili kwa mwezi LAPF mara moja. Kwa mwanachama wa PSPF Bahati mbaya akifariki wategemezi wake mjane au mgane analipwa mpaka atakapoondoka duniani. LAPF analipwa miaka mitatu tu. Halafu kwa mifuko yote PSPF ndo mfuko unaoendeshwa vizuri kuliko yote. Matumizi ya PSPF kujiendesha kwa mwaka uliopita ilikuwa 5% ya michango yote ya wanachama. Mfuko uliotumia gharama kubwa kujiendesha ni LAPF. LAPF Walitumia 21% ya michango ya wanachama kujiendesha badala ya kulipa mafao. Kiwango cha juu kabisa kinachoruhusiwa na SSRA ni 10%. Anayetaka kuhakikisha soma SSRA Reports. Ndiyo maana hata Financial reports za LAPF Zimefichwa, hata kwenye website yao hawaweki. Acheni kusifia vilivyooza. LAPF ni jipu
Unawalalamikia LAPF kutumia fedha nyingi kwenye kuhudumia Wateja wake halafu nyie Huduma mbovu mnajisifu kwa Huduma mbovu ili mbane matumizi wakati Wateja wanalia
 
Mimi nimeshuhudia kwa macho yangu hawa matapeli wanawafokea wazee watu wazima,mmoja analalamika kwamba mwenzie alitoa pesa ndipo akashughulikiwa haraka,wenyewe wanaita hela ya kukimbiza faili,huyu mwingine hana,kastaafu na bado anasomesha,hana hela za kuwahonga hawa nduli wa PSPF na wanamfokea kama mtoto wakati ana miaka 60,hii inatokea karibu ofisi zao zote na wana mitandao wa kugawana hela inayotolewa kuanzia mikoani mpaka huko wanakojua
Duuu...kwahiyo wewe umehudumiwa na Ofisi za mikoa yote? Uko vizuri sana
 
Tofautisha administrative cost na gharama za kuhudumia wanachama. Wametumia 21% administrative cost. Haijumuhishi gharama za kuhudumia wanachama kulipa mafao. Hizo ni gharama za kulipa mishahara, kununua mafuta ya magari, kununua vitafunio etc. Ndiyo maana mdhibiti ameweka kiwango cha juu ambacho ni 10%. Mfuko hautakiwi kuvuka hapo. LAPF Wametumia 21%. Acha kutete ujinga
 
Muulize vizuri mzee wako kama hakutoa rushwa kwa hao vijana,vinginevyo alikuwa mtu mkubwa serikalini,ushahidi upo wa genge la wala rushwa hapo PSPF na mkibisha sana tutawaanika hapa hapa kwa ofisi mbalimbali achilia mbali makao makuu,

Na wajue huu mchezo wao hautawafikisha pazuri,bora hao wachache wabomoke kuliko wabomoe nchi
Samahani lakini he, unaweza kumtaja hata mmoja hapa aliye toa rushwa? Kwasababu PSPF umewataja ni vyema ukawataja walio toa Rushwa. Pia wazee wengine wanajinadi tu kuonekana wao wanaweza kuforce mambo na hata kusema wengine wanatoa kitu kidogo kumbe kuwarusha roho wale ambao wanafatilia malipo yao.
Vilevile hayo malalamiko yanaenda kwa nani? Km wewe nishuhuda weka wazi hapa ntakujibu kwa ufasaha kabisa tena kwa vielelezo
Kwa wale wanao tumwa mitandaoni kuwanywesha sumu mbaya wahitimu ili wasijiunge na PSPF fanyeni kazi nyingine
 
Mkuu mfuko wa PSPF una Deficit ya kiasi cha Fedha za kitanzania Trillion 11. Hii ni kwa mujibu wa Audited Financial statement za 2014/15

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisikia wehu au kuropoka ikiwa mifuko yote haijafikisha 7 iweje PSPF wawe na upungufu wa 11 kuweni macho na magazeti uchwara.
Pia km PSPF inadai serikali iweje muilaumu badala ya serikali inayo daiwa.

Jingine kumbuka PSPF pekee inalipa pesa tangu 2003 hadi 2030 hawa wote michango yao ilawekwa au ilikusanywa na serikali na 2036 hapo itaanza kumlipa mteja baye michango yake yote imekusanywa na PSPF, hivyo nimfuko unao Fanya kazi kwa umakini na kujari wateja wake
 
kwa nini PSPF haitaki kutoa mikopo ya fedha za biashara kwa wanachama wake kama kweli inawajali na kuwathamini wateja wake. waache kuwa hadaa wanachama kwa mafao yasio na tija.
Kasome kazi za SS na Benk au na Financial institution.

Kiufupi nenda SSRA na BoT utaelewa unacho kiwaA
 
kwa nini PSPF haitaki kutoa mikopo ya fedha za biashara kwa wanachama wake kama kweli inawajali na kuwathamini wateja wake. waache kuwa hadaa wanachama kwa mafao yasio na tija.
Pesa zinatolewa ila wapokeaji hufanyia wanavyo weza wao kwa Mf. Pesa ya kuanza maisha mteja akiamua kuanzisha au kuendeleza biashara kuna tatizo gani
 
kwa nini PSPF haitaki kutoa mikopo ya fedha za biashara kwa wanachama wake kama kweli inawajali na kuwathamini wateja wake. waache kuwa hadaa wanachama kwa mafao yasio na tija.
Kwa wazee wastaafu hukopeshwa pia
 
Ukisikia wehu au kuropoka ikiwa mifuko yote haijafikisha 7 iweje PSPF wawe na upungufu wa 11 kuweni macho na magazeti uchwara.
Pia km PSPF inadai serikali iweje muilaumu badala ya serikali inayo daiwa.

Jingine kumbuka PSPF pekee inalipa pesa tangu 2003 hadi 2030 hawa wote michango yao ilawekwa au ilikusanywa na serikali na 2036 hapo itaanza kumlipa mteja baye michango yake yote imekusanywa na PSPF, hivyo nimfuko unao Fanya kazi kwa umakini na kujari wateja wake
Mkuu Kumbuka reference iliyotolewa ni Ripoti ya CAG. Sasa labda utuaminishe kuwa wewe credible kuliko CAG. Usipoteze povu lako bure.
 
Ukisikia wehu au kuropoka ikiwa mifuko yote haijafikisha 7 iweje PSPF wawe na upungufu wa 11 kuweni macho na magazeti uchwara.
Pia km PSPF inadai serikali iweje muilaumu badala ya serikali inayo daiwa.
Povu jiingi alafu hautakatishi nguo. Angalia usijiaibishe, Issue ya Deficit ya Tril. 11.5 imetolewa na kwenye Financial Statements za PSPF zilizoidhinishwa na Bodi. Later on imekuwa-cited kama emphasis of matter kwenye CAG opinion. Sasa kama Financial Statement zilizoandaliwa na Menejiment na kisha kuidhinishwa na Bodi ya wakurugenzi chini Yambesi ni magazeti uchwara itakuwa ni ajabu sana. Lakini pia inawezekana wehu au walioropoka ni hiyo menejimenti na bodi husika.
 
Ukisikia wehu au kuropoka ikiwa mifuko yote haijafikisha 7 iweje PSPF wawe na upungufu wa 11 kuweni macho na magazeti uchwara.
Pia km PSPF inadai serikali iweje muilaumu badala ya serikali inayo daiwa.

Unqualified Opinion
In my opinion, the financial statements present fairly, in all material respects, the Net Assets available for benefits of Public Service Pension Fund as at 30 June 2015 and its Changes in Net Assets Available for benefits and Cash flows for the year then ended in accord the International Financial Reporting Standards and in compliance with the Public Service Retirement Benefit Act No. 2 of 1999.

Emphasis of matter
Without qualifying my opinion, I draw attention to the following matters:

Actuarial valuation
Based on Actuarial Valuation carried out in 2014, the Fund had an actuarial deficit of TZS 11.15 trillion as at 30 June 2014 this valuation was carried out by an independent firm of Actuaries the financial position of the Fund has deteriorated since the previous actuarial valuation which was carried out in 2010 the Fund had a deficit of TZS 6.45trillion. For details please refer to Note 7 to the financial statements.
 
Kama kuna ukurasa mpya katika vita ya kuziba mianya ya rushwa basi iko Pspf.

Shirika hili linasumbua wanaodai mafao kiasi kwamba linahitaji uongozi wa shirika uamke kabla Takukuru haijaanza kuwadaka vijana wanaofanya kazi hapo kama kuku

Utoaji Huduma wa hili shirika ni wazi wanataka rushwa ili kuharakisha malipo,Mara kadhaa nimezhuhudia wazee wakilia mbele yana vijana hao au kufokeana kwa sauti kubwa kisa hawaa vijana wanakwamisha malipo

Japo nawapongeza watu wanaoandaa matangazo,lakini nashauri Takukuru wapige kambi hapo na washirikiane vizuri na wadai mafao

Haitapita mwezi watakamata aliyenona

Wakurugenzi na Bodi amkeni kabla hamjaamshwa na mwenye nyumba mkaondoka kwa aibu

Mkuu uzi wako ushaharibika. Naona kuna ushabiki kati PSPF na LAPF so hakuna ishu itakayokuwa addressed. Mi nilidhani kutakuwa na great thinkers ambao wangeona concern ya PSPF na wanachama wake pamoja na future ya Social Security nchini ila naona hao pro PSPF wenyewe ni mihemuko tu.
 
Hawajibu barua kwa wakati,barua kujibiwa inachukua miezi miwili mitatu na hapo mpaka wamuone mlalamikaji,hili shirika livunjwe,fukuza kuanzia Bodi mpaka wafagiaji,shughuli zao zote zihamie LAPF,iitwe tu LAPF Provident Fund,kama ilivyo CRDB Bank,hao GEPF,futa,peleka LAPF wote
 
tafiti zinaonyesha mfuko wa PSPF
ndio unaongoza kwa kulalamikiwa na wanachama wake zaidi kuliko mifuko mingine!
Hii inaonyesha mfuko huu una matatizo makubwa, watendaji wa mfuko huu wasipo badilika ni hatari sana kwa usalama wa mfuko huu.
pspf wanachezea haki za watu.

Wanadhani wapo salama kwa kuwa wana idadi kubwa ya wanachama hivyo wamebweteka!!!

Wanapaswa kubadilika kwa kuangalia hali halisi ya maisha ya watanzania,

mafao yatolewe kulingana na mahitaji, wakusanye maoni wajue wanachama wanataka nini sio kama ilivyo sasa.
 
Nina maswali ya msingi kwa PSPF

Mnachukua muda gani kuprocess mafao ya mteja? Wenzenu LAPF wanasema mwezi mmoja kabla wanakuwa wameandaa malipo na wanamlipa siku moja kabla hajatoka ofisini kwa kustaafu,ni kweli nyie mnalipa mafao kwa watumishi mnachukua mpaka miaka miwili?

Je kwa kuchelewa huko huwa inawalazimu kuwalipa mishahara hao watumishi kwa kipindi mlichowachelewesha,kuna mtu anadai ilibidi mumpe mishahara ya miezi tisa kwa kuwa mlichelewa kumlipa kwa miezi tisa, hamuoni kama mnapata hasara?

Je mnachukua muda gani kujibu barua za Wateja(muajiri na mwananchi)? Kuna tetesi kwamba huwa hamjibu kwa kiburi tu na hakuna anayefuatilia kama mwananchi kajibiwa na kwa nini hajajibiwa na imechukua muda gani kujibu,mnatumia formula ya fundi cherehani,akimuona mteja ndio anashika nguo kumzuga,akiondoka anaweka nguo chini

Je mfuko wenu una nguvu kiasi gani kuhimili kulipa mafao kwa kuwa kuna ripoti ya CAG imewekwa humu ikidai kwamba mmefilisika

Je MNA mfumo gani wa kushughulikia mambo ya Wateja? Mnachukua namba zao za simu ili kuwapigia hatua zilizofika kushighulikia mambo yao? MNA customer service charter? Inasemaje kuhusu haki za mteja? Kama zipo mbona mnalalamikiwa sana?

Je huwa mnafanya vikao na waajiri wa Wateja wenu ili kupata muafaka wa kero za Wateja wenu au mnasubiri mfatwe ofisini? Mnafanya vikao na maafisa utumishi,makatibu wakuu,na HR? Mbona hawa sio mabalozi wenu wazuri na wanaowaona kama kero?

Ni kweli mnajibu malalamiko baada ya miezi mitatu minne?

Ni kweli mna pensheni hewa na hamzirudishi serikalini?mmekaa nazo muonekane MNA hela nyingi? Hili nalo paka mzee mpango awakurupushe msafishe hesabu zenu?

MNA mawasiliano ya karibu kiasi gani na makatibu wakuu na wakurugenzi wa Taasisi ili muwe up-to-date na taarifa zao? Nani ana wajibu huo na anaufanya kila baada ya muda gani? Mara ya mwisho ilikuwa lini?
 
Acha povu. LAPF Unajisifia kwa huduma zipi? Unawahi kulipa lakini kiduchu. Afadhali mtu asubiri alipwe 100m badala ya 20m. Pension unalipa mara moja PSPF mara mbili. Ofisi zipo kanda tu wakati PSPF Zipo nchi nzima. PSPF. Halafu mnatumia zaidi ya 21% ya michango ya wanachama kujaza mabango na kujenga mabanda sabasaba badali ya kukuza mfuko. Mnatumia zaidi ya mara mbili kujiendesha ya kiasi kinachoruhusiwa 10%. Si ajabu bodi ya LAPF Ilitumbuliwa. Nadhani mgmt inafuata maana inatumbua hela za wanachama kwa vitu ambavyo havina faida kwa wanachama
 
Back
Top Bottom