Propaganda za uchawi na ushirikina

Pole sana ndugu. Tafuta sheikh mzuri akupige kisomo mambo yatakaa sawa tu.
Huwa namchukia Sana mtu anayesema hakuna uchawi, huwa nahisi yeye mwenyewe ni participant mkubwa hivyo anajaribu kuwatoa watu kwenye hiyo Imani ili kulinda Siri za kuvu za Giza wazifanyazo.
 
Ndio umjibu huyo mwenzio kuwa kutokuendelea kwa afrika sio kwa sababu ya kuamini uchawi bali ni uzembe wetu au sababu zengine, nimetoa mfano wa wahindi kuonesha kuwa pamoja na kuamini ushirikina sana ila wana maendeleo ingekuwa kuamini uchawi kunafanya usiendelee basi wahindi tusingeona wakifanikiwa kutokana na jinsi walivyokuwa na imani sana kwenye uchawi.

Wazungu sio kwamba hawana uchawi kabisa hakuna sehemu ambayo hakuna uchawi kabisa, tofauti naweza kusema kwamba hawajihusishi sana na uchawi kama ilivyo afrika na hata ya uchawi wanaojihusisha nao ni tofauti na huu wa kwetu wa kuwangiana.
Wazungu wana uchawi hatari sana mkuu sema, hawaumizani kama Sisi. Kuna sehemu njombe huko wajerumani waliacha Mali ila mapaka leo hakuna kiumbe kinaweza chukua kitu. Zaidi ya wao wenyewe.
 
"Mungu hata umtegemee vipi hawezi kutenda wajibu wako.
Yeye atakachokuzuia ni hila za waovu na Shetani. Mengine yote ufanye MWENYEWE."


Mkuu hapa sijaelewa vizuri.


Mungu kamwe hawezi kufanya wajibu wako hata Kwa sababu gani.

Siku ukielewa hili utakuwa huru
 
Umejuaje mama yako wa kambo kamroga baba yako akuone kama mavi..?!

UMEJUAJE..?!!
Si nimehangaika kwa watalaam pia kanizika ihali napumua inshort nilienda kwa Mganga kwa masuala mengine kabisa ila mwishowe akapiga faraq na akiniambia Kuna uchawi ulifanyiwa ktk makabri lengo la Hawa watu usahaulike
 
Huwa namchukia Sana mtu anayesema hakuna uchawi, huwa nahisi yeye mwenyewe ni participant mkubwa hivyo anajaribu kuwatoa watu kwenye hiyo Imani ili kulinda Siri za kuvu za Giza wazifanyazo.
Kweli kabisaa, hata mtaani ukiona yule anaebisha sana kua hakuna uchawi ndie master wa mambo.
Unaweza kuta hapa tunabishana na Mchawi.
Laanatul.
 
Si nimehangaika kwa watalaam pia kanizika ihali napumua inshort nilienda kwa Mganga kwa masuala mengine kabisa ila mwishowe akapiga faraq na akiniambia Kuna uchawi ulifanyiwa ktk makabri lengo la Hawa watu usahaulike
Mkuu kama una ujasiri hapo fanya ka revenge tuu. Hawa watu sio wa kucheka nao kabisaa
 
Wazungu wana uchawi hatari sana mkuu sema, hawaumizani kama Sisi. Kuna sehemu njombe huko wajerumani waliacha Mali ila mapaka leo hakuna kiumbe kinaweza chukua kitu. Zaidi ya wao wenyewe.
Sio kwamba wana uchawi hatari sana bali ni vile ambavyo wamejikita kuutumia uchawi kwenye nini, huku kwetu tumejikita kwenye kuleteaba madhara na ndio maana tupo vizuri kwenye uchawi huo.
 
PROPAGANDA ZA UCHAWI NA USHIRIKINA.

Na, Robert Heriel

Je, uliwahi kuuona uchawi kwa macho?
Je, uliwahi kupatwa na uchawi? Ulijuaje huo ni uchawi?
Je, uliwahi kumuona ndugu yako au jirani aliyelogwa?
Je, ulijuaje amelogwa?
Je, uliwahi kusikia habari za uchawi?
Je, ulijuaje huo ni uchawi pale uliposikia?

Je uliwahi kusikia hadithi za ukifika baadhi ya maeneo kama Tanga, ati ukitembea njiani ukapiga kifuu cha nazi teke basi kifuu hicho kitaongea na kukuambia ukirudisha mahala pake?

Je uliwahi kusikia hadithi za wachawi kunasa katika nyumba za watu? Au kuanguka na ungo kutoka juu?

Je uliwahi kusikia hadithi za wezi walioiba kuku kisha wakalogwa, hatimaye matumbo yao yakawa yanawika kama kuku?

Je unaamini huo ndio uchawi?

Uchawi ni nini?
Unafanyaje kazi?
Mchawi ni nani?
Anafanyaje kazi?
Ili jambo/kitu kiwe uchawi kinatakiwa kiweje?

Uchawi ni elimu ya juu iliyo nje ya milango mikuu mitano ya mwanadamu. Ni elimu isiyokubaliana na akili ya binadamu kwa haraka. Jambo lolote linalofanyika nje ya uwezo wa milango ya fahamu ya mwanadamu huweza kuitwa ni uchawi.

Uchawi ni istilahi hasi ya nguvu itendayo nje ya maarifa ya kawaida ya mwanadamu. Kinyume cha Uchawi ni Muujiza. Muujiza na Uchawi yote ni sawa. Tofauti ni katika kusudio. Kusudi la Uchawi ni kudhuru wakati muujiza ni kuponya.

Mchawi ni mtu yeyote anayefanya uchawi,

AINA ZA UCHAWI
1. Uchawi wa Asili/ Wakuzaliwa
2. Uchawi wa kufundishwa
3. Uchawi wa Kurithishwa
4. Uchawi Pacha

1. UCHAWI WA ASILI/ KUZALIWA
Huu ni ule uchawi ambao mtu anazaliwa nao tangu mbegu yake ikitungwa. Mchakato wa mbegu kutungwa unadukuliwa na falme za kiroho(roho chafu) ambapo kijusi hutolewa kwa njia za kichawi na kulelewa katika falme za kichawi.

Mama ataendelea kuhisi ni mjamzito bila ya kujua nini kinaendelea kwenye tumbo lake. Kisha baada ya miezi saba kijusi hicho kinarudishwa kwenye tumbo la mamaye. Miezi tisa inafika mtoto anazaliwa tayari akiwa ni mchawi.

Mtoto huyu atakuwa na uwezo mkubwa tofauti na watoto wengine.

Mtoto huyu kila kiungo chake ni uchawi. Uchawi upo mwilini mwake. Yeye ni mchawi, na uchawi ndio yeye.
Wachawi wa namna hii huweza kukuangalia tuu na ukapata madhara, au kukusema jambo lolote likakutokea.

Watu wa namna hii ndio wengi huwezi kuwapiga ukabaki salama. Aidha mkono uvimbe au uharibike kwa namna yoyote ile.

Uzuri ni kuwa wachawi wa namna hii ni wachache kutokana na mchakato wa kudukua Fertilazation ya mbegu kipindi cha mimba kutunga kuwa mgumu.

Mchawi wa kuzaliwa huwa na uchawi Halisi, anaweza kuamua kufanya lolote likafanyika. Wachawi hawa ndio huwa viongozi wakubwa katika Makundi ya wachawi katika kila kanda. Hawa hawadhuriki pindi wanapologwa na wachawi wengine. Baadhi ya filamu zilizoweza kuelezea uchawi wa namna hii ni Filamu ya Merlini.

Kwa upande wa miujiza, ambapo watenda miujiza hufahamika kama Manabii au Mitume. Mfano wa Nabii aliyedukuliwa katika mchakato wa mimba kutungwa ni pamoja na Yesu wa Nazareth.

Manabii wa hivi hawadhuriki, wanakuwa mbali kinguvu na wanadamu wa kawaida. Hawa kila kitu kwao wanaweza kukifanyia muujiza. Hawana mipaka. Hata ukimuua anaweza kufufuka. Ni mpaka Mungu mwenyewe apende.

Manabii wa Mfano wa Yesu ambao wamedukuliwa mbegu zao ni wachache sana, sababu ni ile ile, mchakato wa udukuzi ni Mgumu.

Mchawi wa aina hii huweza kujiua na kujifufua, hawa hufa siku Mungu akipenda. Hata ukimuua wewe iwe kwa kumpiga risasi, au kumchoma moto akateketea kabisa, usishangae ukamkuta nyumbani kesho yake.

Kumbuka, hii ni aina ya wachawi wa juu zaidi, na huwa wachache sana.

2. UCHAWI WA KUFUNDISHWA
Huu ni uchawi ambao watu huingia Darasani au kwenda shule kufundishwa. Uchawi huu upo wa aina mbili.
2.1. Uchawi kama uchawi
2.2 Uchawi kama ushirikina.

Mtu yeyote anayeenda kwa waganga wa kienyeji ni mchawi, sema yupo kwenye kundi la uchawi kama ushirikina. Yeye hufundishwa vitu vichache vya kufanya aidha kwa kupewa dawa, au kufanya matendo, au kutoa maneno. Huyu ndiye mchawi wa kiwango cha chini. Hata wewe kama umewahi kwenda kwa waganga wa kienyeji basi jua upo kundi hili.

Uchawi wa kufundishwa ni ule kijana anaamua kujifunza au anafundishwa uchawi. Kijana anaenda kwa Mganga, au mchawi anakula kozi ya miezi mitatu, au miezi sita, au mwaka, au hata miaka mitatu au saba.

Kulingana na aina ya uchawi autakao.
Uchawi huweza kufundishwa katika mazingira yoyote yale na wakati wowote ule, iwe mchana au usiku.

Mara nyingi uchawi hufundishwa kwenye misitu mikubwa, porini au milimani, mitoni, ziwani, na baharini kulingana na dhana za kujifunzia. Ikiwa dhana za kujifunzia zitakazo hitajika nyingi ni za baharini basi mafunzo yatafanyikia karibu na bahari. halikadhalika na maeneo mengine.

Muda sahihi wa mafunzo ya uchawi ni majira ya alfajiri hasa kuanzia saa tisa unusu, lengo kubwa ni kuepusha jamu au foleni katika ulimwengu wa kichawi.

Uchawi pia hufundishiwa katika ndoto za usiku. Wapo wachawi ambao uchawi wao wamejifunzia wakiwa ndotoni. Hulala kisha huwa kama wanaota lakini sio ndoto bali ni matukio halisi.

Waganga wote wengi unaowaendea wakusaidie wengi wapo kwenye kundi la uchawi wa kufundishwa. Kwa maana hata uganga ni uchawi.

Kundi hili la wachawi ndio kundi kubwa sana.
Nguvu ya uchawi huu inategemea na elimu ya mchawi husika, kiwango chake cha elimu katika uchawi.

Wachawi wa kujifunza wanakuwa na mitihani kama vile shuleni, na kuna kufeli kama kawaida, lakini pia kunakufaulu na kupewa zawadi endapo umefaulu kwa viwango vya juu.

Uchawi wa aina hii hutegemea zaidi mazingira, yaani upo nje ya mwili tofauti na ule uchawi wa kuzaliwa ambapo upo ndani ya mwili.

Mchawi katika aina hii huhitajika kujua miti mingi na namna ya kuichanganya, madini mengine na namna ya kuyachanganya, kukariri maneno ambayo huwa wamefundishwa, hivyo inategemea na uwezo wa akili ya mchawi kukariri na kukumbuka.

Mchawi anayefika kiwango cha juu cha elimu ya uchawi ndio anauwezo wa kuuingiza uchawi mwilini mwake. Yaani uchawi ukawa yeye, na yeye ndio akawa huo uchawi. Wengi hushindwa kufika kiwango hiki.

3. UCHAWI WA KURITHISHWA
Huu ni ule uchawi ambao unatokana na ukoo ya mtu. Uchawi huu hauuzwi, bali hurithishwa kutoka kizazi hata kizazi kulingana na matakwa ya mizimu.

Kuna mafungamano makubwa baina ya mizimu ya ukoo husika na uchawi wa aina hii. Uchawi huu hutokana na maagano yaliyofanywa na mababu au mabibi kwenye ukoo ambao walijifungamanisha na roho za kishetani.

Hivyo uchawi wa kurithishwa unatokana na aidha aina moja wapo hapo juu, aidha ni uchawi wa kuzaliwa, au kufundishwa. Kwa maana Moja ya Mababu au Bibi zako aliingia maagano na falme za kishetani kisha akafundishwa, na akataka kwenye ukoo wake mmoja wa kizazi chake naye awe kama yeye. Hivyo uchawi unatoka kwenye uchawi wa kufundishwa mpaka uchawi wa kurithishana.

Hapa utasikia mizimu ya babu/ bibi inataka wewe uwe mchawi, hivyo utasumbuliwa na Biibi/ Babu ambaye amekufa miaka hata mia iliyopita. Huyo sio Bibi bali ni Pepo lililochukua umbo la Bibi/Babu yako.

Uchawi huu nguvu yake inategemea na kiwango cha pepo aliyekula kiapo na Bibi/ Babu yako. Kama ni Pepo dhaifu basi hata hako kauchawi katakuwa kadhaifu. Lakini kama ni Pepo lenye nguvu basi uchawi huo utakuwa na nguvu.

Uchawi wa aina hii unahusu mambo yote ya Matambiko, ibada zote za mizimu, Mazindiko n.k. Ikiwa upo kundi hili basi jua nawe upo kwenye kundi la wachawi, hasa wale wasio na cheo.

4. UCHAWI PACHA
Huu ni ule uchawi ambao mtu hufanya uchawi pasipo kujua anafanya uchawi. Yaani mtu ni mchawi alafu hajui yeye ni mchawi.
Kundi hili lina watu wengi zaidi, asilimia ya watu wengi wapo kwenye kundi hili. Huenda wewe ni mchawi lakini usijijue kuwa wewe ni mchawi.

Ipo hivi, Moja ya vitu muhimu kwenye Uchawi ni damu ya Mtu. Watu wengi hufikiri damu ni kinywaji pekeake kwa wachawi, hasha, kwenye damu kuna kitu muhimu sana kiitwacho DNA/ Vinasaba.

Kinasaba kinachochukuliwa kwenye damu kinalenga zaidi michakato ya maagano. Katika falme za rohoni maagano hufanyika kwa kutumia damu. Wewe ukienda kwa mganga, ukiona anakuambia anataka kukuchanga chale basi jua hapo kinachotafutwa ni agano kati yako na mapepo au majini ya huyo mganga.

Lengo la Kukuchukua DNA ni kwa ajili ya kukusajili katika mfumo wa kichawi, ili popote uwapo waweze kuku-trace kama watakuhitaji. Vitu vingine ni kama Manii au Shahawa, Nywele, kucha, yaani jambo lolote ambalo DNA au vinasaba vyako vinaweza kuchukuliwa basi kwenye uchawi ni muhimu sana.

Moja ya mambo hatari yanayowaingiza watu kwenye kumi na nane za uchawi ni Ngono. Unapofanya ngono na mwanamke asiye wa ndoa basi fahamu kuwa eneo hilo ni potential kwa Wachawi. Ndio sehemu ya wao kuja kuchukua malidhafi za shahawa/manii na kwa wanawake yale maji maji ya uke.

Wachawi hawawezi kuchukua malighafi za ngono kwa wanandoa. Yaani kama unafanya mapenzi na mke wako au mume wako. Mchawi hana uwezo wa kuchukua malighafi zenu.

Lakini ikiwa mnafanya ngono kwa uzinifu na michepuko basi jua upo hatarini kuingia kwenye kumi na nane za ulimwengu wa giza.

Moja ya maeneo muhimu kwa wachawi ni pamoja Nyumba za kulalia wageni iwe Guests, Lodge, na Hoteli. Kwani huko ndiko malighafi za ngono zinapatikana kwa wingi. Kumbuka ukienda na mke au mume wako nyumba za wageni kufanya mapenzi bado wachawi watajua kuwa mbegu hizi ni za wanandoa, hawatazichukua.

Kwa nini wanazichukua Shahawa zako?
Zipo sababu nyingi, ila moja kuu ni kuchukua DNA/ VINASABA vyako na kuvisajili katika mifumo yao ya kichawi. Ukishasajiliwa, inakuwa Rahisi kwa matumizi yao ya badae iwe leo kesho, au hata kesho kutwa, au hata miaka mia ijayo.

Ni rahisi kuvurugwa na wachawi kama wewe ni mzinzi. Ni rahisi kuharibu maisha yako kama wewe ni mzinzi au wazazi wako ni wazinzi. Kwani kupitia uzinzi taarifa zako zote zinakuwa zimepatikana kwa wachawi, hivyo wao wanaweza amua kukufanya lolote walitakalo.

Ukienda kwa waganga ni lazima uambiwe ufanye yafuatayo, utaje majina ya mhusika, kama humjui, basi utaje majina ya wazazi wake, au kama huna yote basi upeleke nywele, kucha, au nguo ya huyo mtu. Na hii ni kwa mtu ambaye taarifa zake haziko katika mfumo wa kichawi. Lakini kama taarifa zake zipo kazi huwa rahisi zaidi.

Uchawi pacha unatumiwa na wachawi wanaokujua fika. Mchawi huweza kukutumia kwa mtu mwingine bila ya wewe kujielewa. Ipo hivi, unaweza ukawa umelala usingizini, punde ukamuota mtu unayemjua anakuja kukufanyia ubaya, labda anakukimbiza, au anakuchoma kisu, au anakuja akiwa anakuwangia ndotoni lakini.

Kumbe mtu huyo aliyekujia wala yeye hausiki kwa lolote, ila kuna mtu anamtumia ili kukupoteza maboya, Aidha anataka kukugombanisha, na mtu huyo au anamtumia mtu huyo kujificha ili usimtambue mchawi halisi.

Mchawi anawezaje kuingilia mfumo wako wa ndoto, hii inawezekana ikiwa tayari amechukua Vinasaba vyako iwe kupitia Nywele. kucha, shahawa n.k.

Uchawi pacha, ndio uchawi unaotumiwa zaidi na wachawi katika shughuli zao kwa sehemu kubwa.

Endapo mchawi anakuhitaji kimapenzi, na anatka kufanya mapenzi na wewe, basi atamtumia Mpenzi wako au mtu unaympenda kufanya mapenzi na wewe usiku unapolala. Hii baadhi ya watu huiita sijui jini Mahaba, lakini kwa sehemu kubwa wachawi ndio hutumia mbinu hii.

Unakuta kibibi kizee au jimama jitu zima linafanya mapenzi na kijana mdogo kwa kumletea ndoto usiku za mapenzi. Hapo litapata raha, lakini pia litachukua Shahawa.

Wazazi ni rahisi sana kutoa taarifa za watoto wetu hasa tunapozisaliti ndoa zetu. Tunatoa taarifa nyeti za kizazi chetu mbele za wachawi pasipo kujua.

Ni rahisi mtu kupatwa na mikosi endapo taarifa zake nyeti zitakuwa Kwenye Mifumo ya kichawi. Wengi huharibiwa mifumo yao kwa namna ya mambo haya.

Zingatia, familia nyingi zenye wazazi wasio waaminifu huwagharimu wao wenyewe au kugharimu kizazi chao.

Hakuna kazi ngumu kama kumloga mtu ambaye huna taarifa zake. Hakuna uchawi wa hivyo. Uchawi lazima alogwe ambaye taarifa zake ziko kwenye mifumo ya kichawi. Taarifa zako zikiwa kwenye mfumo wa kichawi, hata uwe nchi gani, unalogwa tuu bila shida yoyote ile.

Mtu asiyemalaya, au mzinzi sio rahisi kulogwa, itahitajika baadhi ya taarifa zake, itabidi uagizwe ulete vitu vyake iwe kucha, nywele au nguo ya ndani. Au utaje jina la Mama yake ili kama naye ni mzinzi lazima amsome kwenye mfumo lakini kama sio lazima uhangaike.

UCHAWI NA PROPAGANDA.

Nguvu ya Uchawi ni ndogo sana kwenye hii dunia. Ni kama 10% tu ya nguvu zilizopo hapa duniani.

Kinachofanya watu wafikiri Uchawi unanguvu ni Propaganda za uongo. Sio rahisi kwenye maisha ya binadamu kuuona uchawi. 99% ya yale unayosikia ni uchawi ni Propaganda.

Kwa nini Kuwe na Propaganda za Uchawi
Jibu ni rahisi,ambalo ni BIASHARA

Kama kuna biashara tatu ukiambiwa uzitaje hapa duniani, ukaacha kutaja Biashara ya uchawi, basi wewe bado utakuwa hauujui huu ulimwengu vizuri.

Dini karibu zote unazozisikia hapa duniani zote zinapambana na Uchawi. Iwe ni dini ya Kiyahudi, Kikristo, Kiislamu, Kibudha, kIhindu, Shinto, Voodoo n.k Zote zinafanya biashara kwa kushirikiana na uchawi.
Bila Uchawi hakuna dini?
Bila Uchawi waganga watalia wapi?
Bila uchawi mwanadamu atapata wapi visingizio pale anapofanya uzembe?

Uliwahi kusikia Waalimu au madaktari hapa nchini waliopelekwa vijijini wakihamishwa na wachawi kutoka mahali walipolala, mpaka mahali pengine, huenda ni sokoni, chooni, au juu ya miti mikubwa?
Zile ni sanaa tuu na janja za watu wasiotaka kufanya kazi vijijini. Hakuna uchawi wowote ule.
Unakuta mwalimu anaona shule ipo kijijini sana, shule hiana miundombinu rafiki, mtandao wa simu haushiki, hakuna umeme, hakuna usafiri. Basi kwa vile amepachukia anatengeneza igizo, hapo atajiamsha alafajiri na mapema kama saa kumi na moja, kisha ataenda kulala labda ni sokoni. Kisha asubuhi watu watamkuta hapo sokoni naye atajifanya haelewi lolote, kumbe ni sanaa ya maigizo.

Mwisho ataomba uhamisho, kisa na mkasa atasema anachapa sana. Hahahah!
Hiyo ni Propaganda ya kuuhusisha Uchawi kwa lengo la kuhamishwa. Hakuna aliyewahi kulazwa nje. Nimefanya utafiti katika hili. Wewe kawaulize kwa kina waliofanya matukio ya namna hiyo watakupa mchapo.

Au unakuta wachawi wameanguka, yale ni maonyesho tuu, maigizo. Hakuna uhalisia. Au mchawi kakamatwa kwenye nyumba ya fulani. Yale ni maigizo na Propaganda za kibiashara au zenye lengo la ulinzi kwa kuwatishia watu wenye nia ovu na nyumba alikokamatiwa huyo mchawi au mwizi.

Wachungaji bandia wote na Mashekhe karibu wote huutumia uchawi kama ngazi ya kupata pesa. Sheikhe au Mchungaji ambaye amejikita zaidi kujifanya anaondoa sijui mikosi, majini, mapepo, kulogwa, sijui utajiri wengi ni walaghai.

Mwili wa binadamu umeumbwa na kinga ya asili ya kuzuia magonjwa na mikosi ya kiroho. Wachawi wanachokifanya chakwanza ni kuondoa hizo kinga. Kima ilivyo kwa madawa ya kisasa ya kimwili. Lengo biashara ifanyike.

Niishie hapa kwa Leo.
Kumbuka Uchawi hauna nguvu Ikiwa unamtegemea Mungu. Lakini hata kama humtegemei bado amekupa kinga kwa asimilia mia moja. Ukiona mtu kalogwa ujue kinga imeshushwa mpaka imekuwa chini ya 10%

Acha dhambi hakuna mchawi atakugusa.
Uchawi kwa 90% ni propaganda

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Mkuu na wewe unaroga?
 
Back
Top Bottom