Propaganda Za Mitandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda Za Mitandao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, May 2, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  May 2, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  PROPAGANDA ZA MITANDAO

  Mwaka jana niliwahi kuandika makala moja kuhusu propaganda za mitandao katika makala hiyo niliongelea kidogo kuhusu baadhi ya watu kwa kusukumwa na ushabiki wao wa kitu fulani , uhuni wao tu , ugonjwa tu , na matatizo yao mengine mbali mbali waliyonayo wanaamua kukaa katika computer zao na kuanza kuandika na kusambaza habari mbaya kuhusu watu wengine , vikundi au kampuni za wengine kwa makusudi kabisa bila kuwa na udhibitisho na habari hizo .

  Watu hawa wana blogu wengine ni maarufu katika forum za watanzania na wengine wanaaminika sana kiasi kwamba wakisema chochote kwa manufaa yao basi watu wote huwafuata wao na kusikiliza kile wao wanachosema hata kama sio kwa masilahi ya taifa hili tukufu la Tanzania .

  Wananchi wanaosoma blogu hizi , forum hizi na aina nyingi ya vipeperusi wawe makini sana na matangazo yao , watu hawa hawana nia njema kwa maisha ya watanzania walio wengi , wanaharifu fani ya habari na taaluma yake kwa ujumla na ndio maana wanatumia majini tofauti tofauti kujitetea au kuhalalisha hizo habari zao .

  Ni kweli mtandao hauna mipaka , kabila dini wala chama lakini wengi wao wanaonekana kuishushia hadhi serikali ya tanzania , baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na chama tawala chama cha mapinduzi kwa propaganda zao ambazo hazina masilahi yoyote

  Tunaheshimu uhuru wa mtu kusema au kuandika chochote katika mtandao lakini mtu anapofikia kutuma habari za uwongo zinazochochea vurugu na fujo nyingine katika jamii mtu au kundi hilo la watu hatutalivumilia wala kulikalia kimya

  Watatafutwa na kufikichwa katika vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizi za kusambaza habari za uwongo , chuki na visasi
   
 2. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Usitake kutisha watu wewe kibaraka mkubwa wa Mafisadi
  Na wewe unaweza kuwa mmoja wapo wa propaganda za Mtandao, na eti unajiita Researcher??
  Haya vielelzo vya hayo maneno yako kuwa watu wanaandika habari za uongo kuhusu serikali, viongozi, na chama tawala viko wapi?

  Hivi wewe ndio unasema kweli eti unaliteta taifa na wananchi wake??
  Acha unafiki na ufaidhina wewe, wewe unawezekana punguani kabisa, unaacha kufanya mambo ya muhimu ya kuwafikisha mafisadi kwenye sheria unakuja na porojo za kutisha watu!!

  Sasa tutaendelea kuisema serikali pale inapokosea , viongozi wake, na chama chenu cha Mifisadi, ukiona kama ni uongo weka vigezo na kuwahakikishia wananchi kuwa hii sio kweli, sio kuja na kuleta porojo hapa!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Thank you BabaH. You made my day and there is nothing more to add.
   
 4. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Shy

  Hii haijatulia kabisa na kwa maana ya jina ulilolichagua la Shy linaendana na mtindo wako wa kupachika hoja hapa jamvini na kukimbia pembeni ili uone what the reaction will be.

  Unataka kuwa jasusi? Tazama movie za "Recruit", "Training Day" na hizo ni baadhi tu na zinafundisha kuwa mwangalifu na mtindo wa kufuata mikumbo na ushawishi usio na maana, ili mradi tu unataka kuwa mtu fulani.

  Mtindo wa kutishia watu bila sababu za msingi ni ujinga kama si upumbavu. Kama hujui ni kwamba kuna tofauti kubwa kati ya mtu mjinga na yule mpumbavu. Kwa hio jinsi ukakavoendelea kuleta hoja zako zisizo kichwa wala miguu, unaweza ukajikuta una-fit katika moja ya hizo "criterias".

  Kwanza ni nani amekutuma kuleta hio ajenda yako hapa?

  Wakikutuma tena wewe changanua kwanza kabla ya kuanza kuandika hayo mambo yako ya ajabu.
   
Loading...