King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,581
2,000
Gwajiboy aligombea ujumbe wa NEC mama na kamati yake wakamuona hatoshi wakampiga panga. Hiki kitu kilimuuma sana Gwajiboy.

Sasa hivi anatumia chanjo kummaliza mama kisiasa. Ajenda ya Gwajiboy sio kupinga chanjo ila ni kummaliza mama kisiasa.
Mama awe makini. Gwaji atatumia chanjo na ukabila kummaliza.

Mkono wa BAUNSA ni Tapeli.
 

mgaka12

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
567
1,000
Tanzania ni moja ya taifa la ajabu kabisa Gwajima ametoa hoja zake mjibuni kwa hoja si kuleta maneno maneno pia Gwajima hayupo peke yake ukitaka kujua hayupo peke yake mguseni tu.
 

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,121
2,000
Hana hoja zaidi ya kupotosha na kuleta taharuki.
Unataka Hoja gani zaidi ya Hoja ya Uhakika wa Chanjo? Form ya Wizara ya Afya kujitoa katika kuwajibika kwa madhara yatokanayo na Chanjo sio uthibitisho kuwa hawana uhakika na Chanjo hiyo? Umewahi kusainishwa Form kama hiyo kwa Chanjo zingine?
 

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
600
1,000
Tanzania ni moja ya taifa la ajabu kabisa Gwajima ametoa hoja zake mjibuni kwa hoja si kuleta maneno maneno pia Gwajima hayupo peke yake ukitaka kujua hayupo peke yake mguseni tu.
Gwajima hana hoja. Ngoja nikukumbushe uongo wake kuhusu Corona.

1. Mwaka jana alisema Corona imesababishwa na teknolojia ya 5G. Kwa hiyo Tanzania haiwezi kufika kwa kuwa hatuna 5G.

2. Mwaka huu anasema Corona ni mpango wa shetani kuunganisha watu.

3. Pia ikumbukwe alisema anaenda Amana kwenye wodi ya Corona kwenda kuwaombea ila akaingia mitini.

Aonywe aache kutafuta kiki kwenye mambo ya kisayansi.
 

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
600
1,000
Unataka Hoja gani zaidi ya Hoja ya Uhakika wa Chanjo? Form ya Wizara ya Afya kujitoa katika kuwajibika kwa madhara yatokanayo na Chanjo sio uthibitisho kuwa hawana uhakika na Chanjo hiy
Hizo form hospitali zipo miaka yote zimeandikwa hivyo. Mfano ukiwa unafanyiwa upasuaji mkubwa kabla ya kupigwa sindano ya usingizi/NUSU KAPUTI lazima ndugu zako wasaini fomu kama hizo.
 

Christine1

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
14,543
2,000
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha.

Huyu mtu anarudisha juhudi za serikali nyumba ikiwa Mhe Rais alitamka wazi kua sisi siyo kisiwa hatuwezi kujitenga na na dunia, mpotoshaji moja anasoma na kumdhihaki Mama eti anashadadia pesa za Bilgate kweli?

Eti anaombea madaktari wanahimiza na kuchanja watu wafe,huyu mtu ni chizi si mzima. Na atakufa yeye kwanza Corona tunamuombea kama yeye anavyoombea watu.

Gwajima anajifanya yeye mtu wa Mungu wakati ameiba kura za ubunge mchana kweupe dunia inajua, anapata wapi Moral authority ya kunyooshea watu vidole mtu huyu wakati anakula vya halamu? Chama tunajua kuwa aliiba kura na ushindi wake ni haramu tumemnyamazia na akiendelea tutamuumbua.

Huyu mtu ni wa kupuuza anaendelea kurudisha mapambano ya serikali nyuma, lakini akiendelea hivi akamatwe. Hawa ndio waliompotosha mzee kwa kiasi kikubwa tukajikuta tumeingia katika matatizo makubwa. Hivyo kabisa na wapuuzwe. Pesa za Bilgate ndio nini? Kwani Corona haipo?
We ndo wa kupuuzwa sio Gwajima!
Muwe mnafikiria kabla hamjajibu!
Instead of kujadiri hoja alizozitoa unaanza kumjadiri yeye ndo akili hizi?
 

F-Merylin

Senior Member
Dec 26, 2016
115
250
Natamani kukuelimisha vema zaidi kuhusu chanzo za corona na madhara yake kulingana madaktari bingwa wa US na UK na witnesses za wagonjwa waliochanjwa. Na pia siri nyingi nyuma ya pazia. Lakini kwa vile sidhani kama una uwezo wa kuelewa Kachanje tu na baada ya miaka mitatu niambie experience yako.

Gwajima katika hili haongei kama kiongozi wa dini bali kwa niaba ya watu wengi sana wanaojua madhara ya chanjo lakini wanaona Samia Suluhu anatafuta urafiki na Kaizari kwa sababu ya Pesa na Umaarufu! Anasahau soon watam-damp kama walivyofanyiwa marais wengine wengi sana huko nyuma! Kwanza kaishawaudhi tayari kwa Mbowe.

Huwezi kuniambia korona imekuwa kubwa ghafla baada tu ya Magufuli kufa. Kutoka 100 to 300 to 700 na soon itakuwa elfu 10. Kujenga tu hofu.... na baadaye nini? Nilishamwambia Samia kuwa kama anaipeleka nchi kwenye Lockdown ili apate hela aandae Risasi mapema kutuua.

Approach ya mwanzo ilikuwa sahihi. Hakuna chanjo iliyosalama wala inayozuia kwa 100% kuambukiza au kuambukizwa au kutougua tena. Na hakuna chanjo ambayo sio majaribio! Na madhara ni makubwa sana kwa waliokuwa affected. Katika hali hii only fools can take it without thinking eti kwa vile Rais kasema!

By the way Chanjo ni Hiari. Kama unaitaka hakuna anayekuzuia.
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,704
2,000
Ni bora zijibiwe hoja za Gwajima juu ya Chanjo hiyo kuliko kuhusisha mambo mengine ambayo yeye Gwajima hajayasema! Mbona Marehemu Magufuli naye aliwahi kutoa tahadhari juu ya Chanjo kama hizi?
Exactly, Gwajima anabezwa tu! Hii nchi hakuna reasoning. Mchungaji katoa hoja hajibiwi zinaanza kejeli.

Hakuna anayekataa chanjo ila kuna controversial nyingi hata wanataaluma wenyewe.

Mfano mdogo why matokeo/madhara wanasema ni juu ya mtumiaji? Mbona zipo taarifa za wazi kuwa wengi waliochoma chanjo wanapata maambukizi? Haraka haraka za nini? Tunawahi nini?
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,435
2,000
Wandugu watanzania ni kazi sana kuwaelewa akili zao. Sasa kuna hawa wanapinga sana chanjo wakiongozwa na Gwajima. Wanasema zitawafanya kuwa mazombie, na ameshauri eti askari wasipewe. Sasa katika chanjo zilizopo, kuna ya China, Sputnik ya Urusi, Moderna, ya Astra-Zeneca, Johnson&Jonson na ya Pfizer. Sasa ni ipi hasa inayosababisha uzombie?

Miaka ya nyuma kidogo UKIMWI ulipopamba moto Thabo Mbeki na waziri wake wa afya wakasema kuwa hamna kitu kinachoitwa UKIMWI, wakasema watu wasitumie dawa na kama upo wanaweza kuutibu kwa Malimao na Kitunguu saumu. Hii ikapelekea watu wa South Kutojali na kupata UKIMWI kwa wingi. Mtikila naye amewahi sema amepata dwa ya UKIMWI.

Serikali inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kuhusu chanjo ili mtu anapochagua kuchoma au kutochoma afanye informed decision. Lakini kwa ilivyo sasa watu wanafanya maamuzi kupitia taarifa za kina Gwajima na wapotoshaji wengine.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,567
2,000
Hoja za kipumbavu za askofu uchwara
Exactly, Gwajima anabezwa tu! Hii nchi hakuna reasoning. Mchungaji katoa hoja hajibiwi zinaanza kejeli.

Hakuna anayekataa chanjo ila kuna controversial nyingi hata wanataaluma wenyewe.

Mfano mdogo why matokeo/madhara wanasema ni juu ya mtumiaji? Mbona zipo taarifa za wazi kuwa wengi waliochoma chanjo wanapata maambukizi? Haraka haraka za nini? Tunawahi nini?
 

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,753
2,000
Huku mtaani eti watu wameanza kuogopa CHANJO kuliko CORONA yenyewe wanaishi na mzimu wa mwendazake kwenye kuamini kuwa wazungu(wagunduzi wa chanjo) wana nia ovu kupitia hizi chanjo.
Hebu tujiulize je wazungu wakiamua kutumaliza tunaweza kuwa kwepea wapi mambo mengine tunaonekana nyani kwa mawazo yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom