Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha.

Huyu mtu anarudisha juhudi za serikali nyumba ikiwa Mhe Rais alitamka wazi kua sisi siyo kisiwa hatuwezi kujitenga na na dunia, mpotoshaji moja anasoma na kumdhihaki Mama eti anashadadia pesa za Bilgate kweli?

Eti anaombea madaktari wanahimiza na kuchanja watu wafe,huyu mtu ni chizi si mzima. Na atakufa yeye kwanza Corona tunamuombea kama yeye anavyoombea watu.

Gwajima anajifanya yeye mtu wa Mungu wakati ameiba kura za ubunge mchana kweupe dunia inajua, anapata wapi Moral authority ya kunyooshea watu vidole mtu huyu wakati anakula vya halamu? Chama tunajua kuwa aliiba kura na ushindi wake ni haramu tumemnyamazia na akiendelea tutamuumbua.

Huyu mtu ni wa kupuuza anaendelea kurudisha mapambano ya serikali nyuma, lakini akiendelea hivi akamatwe. Hawa ndio waliompotosha mzee kwa kiasi kikubwa tukajikuta tumeingia katika matatizo makubwa. Hivyo kabisa na wapuuzwe. Pesa za Bilgate ndio nini? Kwani Corona haipo?
 
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha. Huyu mtu anarudisha juhudi za serikali nyumba ikiwa Mhe Rais alitamka wazi kua sisi

Serikali yenyewe inasema litakalokukuta haiwahusu uwo kuna sinema hapo
 
Huo ni uhuru wa kuongea na kutoka maoni yake tusitake kuwanyamazisha watu kwa kuwatisha, kila mmoja atapima mwenyewe lipi jema kuchanjwa au kutochanjwa bahati nzuri serikali imetoa hiari.

Wanaosema Gwajima akamatwe je mnataka nchi irudi enzi za unafiki?
 
Pumbavu kabisa, hapo ulipo umejaa makovu ya chanjo za surua, ndui, TB na polio u ulizochanjwa na mama yako kabla akili yako haijajaa matope.
Mimi si mshabiki wa Askofu Gwajima. Lakini nakubaliana naye kwa ishu ya chanjo. Ni mtu mjinga pekee ndio anaweza kubali Chanjo. Mungu hakosei kuhusu immunity aliyomuumba nayo mtu. Why chanjo now?
 
Yaani Gwajima ndio wa kupingana na Kauli ya Amiri Jeshi Mkuu? Eti Askari wasichanjwe? Eti Madaktri wasichanjwe? Eti Rais amepokea pesa ili akubali Chanjo?

Hata kama chanjo ingekua na makosa/mapungufu bado sio sahihi kwa Gwajima kutumia Umaarufu wake kuyapinga tena hadharani maelekezo ya Rais

Msipomkemea Gwajima, wallah wabillah nawaapia kuna siku ataiingiza hii nchi kwenye shida kubwa huku mlivyo wajinga mkiwakamata na kuwaharasi Chadema.

Wacha tukae kimya tumpigie makofi...
 
Acheni kubadili maana ya mahubiri ya Gwajima nyie popona, alichosema Gwajima ni kwamba kabla chanjo haijaanza kutumika nivizuri wataalam wetu wajiridhishe ubora wa hiyo chanjo na pia uhalisia wake isije ikawa tumeletewa kitu kingine na c chanjo.

Kuhusu Madaktari alisema kuwa wasishadadie watu wa chanjwe bila kuwepo uhakika wa chanjo husika na ndipo akasema atakaye fanya hivyo na Afe.

Akaenda mbali zaidi kusema hiyo anaye shadadia watu wa chanjwe(Gaidi)yy ana maslahi tayari na hiyo chanjo.
 
Mimi si mshabiki wa Askofu Gwajima. Lakini nakubaliana naye kwa ishu ya chanjo. Ni mtu mjinga pekee ndio anaweza kubali Chanjo. Mungu hakosei kuhusu immunity aliyomuumba nayo mtu. Why chanjo now?
Vipi kuhusu watu ambao wamekufa kwa corona, wao immunity yao ilikosewa?

Kwa hiyo tufunge mahospitali na kila mtu ajitibu kwa immunity yake?
 
Acheni kubadili maana ya mahubiri ya Gwajima nyie popona, alichosema Gwajima ni kwamba kabla chanjo haijaanza kutumika nivizuri wataalam wetu wajiridhishe ubora wa hiyo chanjo na pia uhalisia wake isije ikawa tumeletewa kitu kingine na c chanjo,
Kuhusu Madaktari alisema kuwa wasishadadie watu wa chanjwe bila kuwepo uhakika wa chanjo husika na ndipo akasema atakaye fanya hivyo na Afe,
Akaenda mbali zaidi kusema hiyo anaye shadadia watu wa chanjwe(Gaidi)yy ana maslahi tayari na hiyo chanjo
Sasa huu ndio upuuzi wa CCM ninaoukemea daily
 
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha.

Huyu mtu anarudisha juhudi za serikali nyumba ikiwa Mhe Rais alitamka wazi kua sisi siyo kisiwa hatuwezi kujitenga na na dunia, mpotoshaji moja anasoma na kumdhihaki Mama eti anashadadia pesa za Bilgate kweli?

Eti anaombea madaktari wanahimiza na kuchanja watu wafe,huyu mtu ni chizi si mzima. Na atakufa yeye kwanza Corona tunamuombea kama yeye anavyoombea watu.

Gwajima anajifanya yeye mtu wa Mungu wakati ameiba kura za ubunge mchana kweupe dunia inajua, anapata wapi Moral authority ya kunyooshea watu vidole mtu huyu wakati anakula vya halamu? Chama tunajua kuwa aliiba kura na ushindi wake ni haramu tumemnyamazia na akiendelea tutamuumbua.

Huyu mtu ni wa kupuuza anaendelea kurudisha mapambano ya serikali nyuma, lakini akiendelea hivi akamatwe. Hawa ndio waliompotosha mzee kwa kiasi kikubwa tukajikuta tumeingia katika matatizo makubwa. Hivyo kabisa na wapuuzwe. Pesa za Bilgate ndio nini? Kwani Corona haipo?

Hatutaki kugandisha damu zetuu.

#YNWA
 
Nakwambia watalia, subiri wamuendekeze tu huyu pimbi
Ngoja "wafuasi" wake wenye hasira kali waende kuchoma hilo ghala wanalotumia kuhifadhia hizo chanjo...au wawachome moto wahudumu wa afya watakaoenda kuelimisha watu kuhusu chanjo🐒
 
Back
Top Bottom