Propaganda ya mauaji imefanikiwa... CHADEMA fanyeni hiki!

Habari za kwa mama ntilie nazo! Huyu naye ni GT
Wewe ndio Ugreat thinker wako una walakini
Mtoa mada kamaanisha kapita katika makundi yote ya kijamii bila kujalisha level za za kimaisha
na sasa wewe unaonesha dharau kwa hawa mama zetu ambao ni wengi mno kwenye jamii zetu
Shame on you Masanilo
 
Kwanza nianze kusema mimi ni NAM person..sifungumani na Upande wowote Hasa katika Maslahi na matakwa ya wananchi,,im free opened MIND! Ndo maana naweza kusema kuwa CCM sasa kuna baadhi ya Mawaziri wanafanya Vizuri mfano,Kagasheki na Mwakyembe!

Si hata vibaya CDM wakawa wanawapongeza Mawaziri wanaofanya Vizuri ili kuonesha Hawako katika kupinga tuuuu,,kwasababu wanachi wengi wanadhani UPINZANI ni Kupinga tu.ili kuonesha They lay at right SIDE!

Juzi nilitoka kupiga soga na 'Waswahili' mtaani,Kutaka kujua lile tukio la R.I.P Mwangosi wananchi wamelipa uzito gani!Nikapita kwa vibanda vya mamantilie hadi kule kwenye GAHAWA!

Wananchi hasa wale ambao hawana Muda wa kusoma Magazeti wala Kuangalia TV( kutokana na Ugumu wa Maisha) wanalaumu CDM!!Kuwa chama cha MAUAJI na VURUGU!!

Ushauri wangu sasa ili kuwaweka wananchi sawa,

1)Kuna Picha ile ambayo MWANGOSI anaonekana akilipuliwa Laivu,Isambazwe bure mpaka vijijini tena sana...Hii itasaidia kufuta tongotongo na Kuchafua chama.

2)Ile VIDEO ya Mauaji isambazwe kwa CD tena bureee,kila mtu ashuhudie yale mauaji!

BAJETI hai haitazidi 10 millioni,bt manufaa yake yataonekana 2015!

CHADEMA mkipuuza hiki kitawa'COST sana!

Kinyume chake pia ni kweli, ccm hili litawacost sana, kwa sababu ya baadhi ya mambumbu waliofunga ndoa na ccm pamoja na walewanao tafuta vyeo, ambao wanazani wao ndo wanahaki kuliko mtu yeyote ndani ya Tanzania. Hivi ni nani asiyejua uozo wa ccm au habari za mauaji ya mwangosi ndo zinazowafikia hawa wanavijiji? Kama wameweza kujua mauji ya polisi kwenye mikutano ya cdm basi watajua tu kuwa siyo cdm. Hizi nyingine ni propaganda tu. Tunahitaji watu majasiri na wenye uthubutu na uwezo, siyo akina bendera fata upepo. Wape muda tu hao, watakutana na kimbunga.
 
Nimejaribu kuchunguza athari za kutekeleza maoni ya mleta mada sijaona. Sioni hasara, ila ziko faida kadhaa katika kutekeleza hilo.

Ni kweli kuwa si kila Mtanzania aliyeko nchini anaujua ukweli. Na hata wale wenye kuujua sio kwa viwango sawa na sisi wa mijini. So mbali na tukio la kuuawa kwa Daud Mwangosi itakuwa ni fursa ya kujibu na kupanua mawazo ya wanakijiji ktk masuala mengine yenye kufanana na hayo, ambayo sina shaka yako ila tu hayajaibuliwa.

Ni katika dhana nzima ya kuweka general awareness to the public. Sioni madhara ktk hilo.

Of coz huwezi kubagua wapiga kura na pia hutaki kuwa na jamii yenye kuamini mambo ya kusadikika so CHADEMA kupitia M4C au Sangara wakilifanyia hili kazi itakuwa busara tu.
 
Mwananchi yupi wa leo asiyejua hii kitu wewe mtu! hata kama hasomi magazeti wala hatizami tii vii, ataipata story kwenye kijiwe,shambani,kazini,bar,msibani,harusini,hotelini kwenye daladala,ataambiwa na mwanae,babake.mamake,mjombake,shangazie,kaka au dadake!!!!! burazaa huu ni mtiti cos raia wa leo wa nchi hii ni wapya kabisaaa wale wa zamani wamekufa wote!

Ane wai ushauri wako umezingatiwa.

sasa we borakufa mwenzio anasema kafanya utafit maeneo yote asa we hutak au huelew hebu toa upompopo wako
 
Hii kiboko, unashauri wenzio kutumia kifo cha mtu kama mtaji wa kisiasa...
Af ungejisikiaje ingekuwa ni picha au video za kifo cha baba'ko au mama'ko ndo zingesambazwa kwa mtindo huo?
 
Haya twambie hizi habari unazo sema umezitoa vijijini? Au unawasingizia?

Wewe umeongelea mamantilie wawapi?

Hao ni hao uliowasikia wewe redioni, umeshafika vijijini na kusikia watu wanasemaje kuhusu vyama vingi, achilia mbali vifo vya juzi?

Shigela naye ni mwananchi. Kuna watu nyuma yake na wengine wanamsikiliza na kumwamini zaidi ya magazeti na redio kwani wanaamini kwa wadhifa wake anafahamu zaidi. Wassira naye ni mwananchi na ana wafuasi nyuma yake. Nape naye ni mwananchi na ana wafuasi.

Usiseme wananchi wanaelewa as if uliongea nao wote. Kama unakaa Sinza unaweza kudhania hivyo lkn ukienda Buguruni ukamsikia mama lishe anachoongea utasikia kichefu chefu. 'Ah hawa CDM wanataka tu kutuletea fujo wengine sisi tutakimbilia wapi. Miaka yote tumejiuzia maandazi yetu hapa bila shida wao kwa uroho wao wa uongozi kazi kufanya fujo tu. Polisi wameshaambia msifanye kikao leo wanabisha, sasa wao na polisi mwenye nguvu nani, aah'

Mtu mwenye maneno ya hivi unaweza ukamuhesabu katika upande wa harakati?
 
Nimejaribu kuchunguza athari za kutekeleza maoni ya mleta mada sijaona. Sioni hasara, ila ziko faida kadhaa katika kutekeleza hilo.

Ni kweli kuwa si kila Mtanzania aliyeko nchini anaujua ukweli. Na hata wale wenye kuujua sio kwa viwango sawa na sisi wa mijini. So mbali na tukio la kuuawa kwa Daud Mwangosi itakuwa ni fursa ya kujibu na kupanua mawazo ya wanakijiji ktk masuala mengine yenye kufanana na hayo, ambayo sina shaka yako ila tu hayajaibuliwa.

Ni katika dhana nzima ya kuweka general awareness to the public. Sioni madhara ktk hilo.

Of coz huwezi kubagua wapiga kura na pia hutaki kuwa na jamii yenye kuamini mambo ya kusadikika so CHADEMA kupitia M4C au Sangara wakilifanyia hili kazi itakuwa busara tu.

Kweli kabisa,Nilifanya analysis kidogo tu Kigamboni,Temeke,Kimara ambapo kuna jamaa zangu,,,,Unakuta mtu haelewi kabisa kuhsu lile tukio, Sembuse MATOMBO!
 
Hii kiboko, unashauri wenzio kutumia kifo cha mtu kama mtaji wa kisiasa...
Af ungejisikiaje ingekuwa ni picha au video za kifo cha baba'ko au mama'ko ndo zingesambazwa kwa mtindo huo?

Umeninukuu vibaya,Though Jamii inatakia kujua 'wHaTT' was behind the Scene! Kama serikali imeshindwa kufafanua vizuri,Kupata habari ni HAKI ya kila RAIA
 
na huo ndio ukweli ambao cdm mmekua mkiupotosha umma kwa kutumia media, kukashifu kila chombo cha habari chenye mtizamo tofauti nanyi, watanzania ukiacha washabiki wa cdm, ni waelewa and soon mtalitambua hilo.

Na wewe ni mtu?
 
Haya twambie hizi habari unazo sema umezitoa vijijini? Au unawasingizia?

Wewe umeongelea mamantilie wawapi?

Akili yako fupi, tena sana. Kinachotusumbua ni kupenda sifa na kukosoa kila kitu.

Hapa hapa JF ambapo tulikuwa wa kwanza kuona picha za tukio na kupata maelezo ya nini kimetokea wapo watu wasio na aibu kusema chanzo ni CDM, unategemea nini kwa watu wa kijijini wasio na access na mitandao achilia mbali hayo magazeti?

Kama akili zako ndio hizi, hao wasiofikiwa na habari je? Juzi hapa tumeona watu wa mjini kabisa ambao matangazo na ya aina zote yanawafikia, lkn still wakagomea sensa kwa kufuata akili za kuambiwa na mtu ambaye yeye mwenyewe keshahesabiwa. Nini cha kushangaza ikiwa wa kijijini ambao hata maana ya sensa hajui akigoma?

Shida yenu wengine umri na kuzaliwa Buguruni mkaishi Buguruni, mlisoma Ilala na sasa mnaishi Keko. Mkiambiwa Kijiji mnatafsiri kwamba Mjini ni Dar es Salaam na Kijijini ni Dodoma mjini. Unaposhuka kwenye basi pale Nyakato pale sio kijijini. Vijiji viko ndani huko km 170 kutoka Nyakato. Mpaka ufike huko unatumia masaa, muuza magazeti anafika huko lini?

Eti mama ntilie wa wapi, sio mama ntilie tu, hata Shigela na familia yake wana mawazo hayo kwa kuwa hawajisumbui kufikiri kama ulivyo wewe. Kwa wewe ni bahati tu umeangukia upande wa pili
 
Haya twambie hizi habari unazo sema umezitoa vijijini? Au unawasingizia?

Wewe umeongelea mamantilie wawapi?
quote_icon.png
By SUPERXAVERY

na huo ndio ukweli ambao cdm mmekua mkiupotosha umma kwa kutumia media, kukashifu kila chombo cha habari chenye mtizamo tofauti nanyi, watanzania ukiacha washabiki wa cdm, ni waelewa and soon mtalitambua hilo.

Haya huyu ni mama ntilie? Huko anakoishi mtu wa akili hizi hakuna watu mtaani kama mkata majani wa jirani yake, house girl wake n.k ambao wao wataamini kwa mawazo ya huyu?
 
Hivi unajisikiaje unapotea ushauri kwa nia njema halafu ukafukuzwa na mawe na yule unayemshauri???

Ndio unapata picha kamili ya tatizo. Watu wanasema wote tumeelewa ilhali wao tu wameshindwa kuelewa hili dogo namna hii. Nampa pole muanzisha mada, lkn asikate tamaa tutafika tu
 
Toa uongo wako hapa......hakuna mwananchi asiyeujua ukweli wewe......nenda zako na ushauri wako wa giza

Unajifanya hufungamani , basi utakuwa umetumwa na wanaofungamana.....rudi kajipange vizuri!

Ninyi ndio mnao haribu CDM!
Ni ushauri wa maana kufanyiwa kazi.
 
Kweli kabisa,Nilifanya analysis kidogo tu Kigamboni,Temeke,Kimara ambapo kuna jamaa zangu,,,,Unakuta mtu haelewi kabisa kuhsu lile tukio, Sembuse MATOMBO!

Yeah ni moja ya mambo ambayo huwa kama binadam tuna hulka ya kuyapuuza kwa sababu tu ya mtazamo wa ujumla-jumla (generalization of things). Nakubaliana nawe vizuri kwani hata mimi nimeliona hilo. Well done and just keep it up!
 
Ushauri wangu sasa ili kuwaweka wananchi sawa,

1)Kuna Picha ile ambayo MWANGOSI anaonekana akilipuliwa Laivu,Isambazwe bure mpaka vijijini tena sana...Hii itasaidia kufuta tongotongo na Kuchafua chama.

2)Ile VIDEO ya Mauaji isambazwe kwa CD tena bureee,kila mtu ashuhudie yale mauaji!

BAJETI hai haitazidi 10 millioni,bt manufaa yake yataonekana 2015!

CHADEMA mkipuuza hiki kitawa'COST sana!

Mkuu, unawezaje kushauri unyama huu ufanywe na watu makini kama CDM!!!!!?????
I can't believe a great thinker trying to suggest CDM to take advantage of the reporter's death!!! God forbid!

Siamini kwamba mkuu unaitakia mema CDM, japo unajifanya hufungamani na upande wowote.

Hivi marehemu Mwangosi angekuwa ndugu yako, ungeufurahia unyama huu unaoupendekeza wa kusamabaza picha za kutisha kama zile?

Mkuu, kama utafanikiwa kuyasoma haya maoni yangu ninakuomba fikiria japo mara mbili kuhusu ushauri wako kwa CDM.
 
Sio kweli uliyoyasema, ni wananchi wachache sana tena nidra kukutana nao wakilaumu cdm kwenye hayo matukio ya mauaji hata ukisikiliza tu vipindi vya radio utasikia wa kicomment kwa kulaumu jeshi la polisi kutumia nguvu kuizibiti cdm!

Umejaribu kutunga story mkuu!
Kwa hayo matukio kwa kweli jeshi la polisi lina laumiwa sana.

Tena wengine wanahoji kwa nini nchimbi aliwasingizia wafuasi wa cdm kuwa walirusha kitu kizito?

Hao wanao lahumu cdm tena wakati wanajua ukweli ni ccm na mabaraza yake:

Tafadhali usiwasingizie wananchi kabisa wanaelewa kila kitu si watu wa kudanganywa kama huko nyuma walivyo kuwa wanawadanganya/!

Kabla ya kutoa generalized statements kwamba watu wanajua nn kinaendelea ni vema kufanya utafiti wa kina. Bado ninaamini kwamba kuna kundi kubwa bado linahitaji kuelimishwa. Kama mawazo alotoa huyu bwana yanafaa yafanyiwe kazi. Merikani watu wao ni wajuvi wa mambo na wapo exposed sana lakn bado wagombea,Obama na Mitt Romney wanajaribu kuwaelimisha wapiga kura kila cku. Sembuse hawa wabongo?
 
We can't act Kwenye utafiti Wa mama ntilie mmoja ulipoend kula wali na maharaja, leta data za utafiti otherwise hatufanyii Kazi hisia zako, endelea kutofungamana na Upande wowote.

Kwanza nianze kusema mimi ni NAM person..sifungumani na Upande wowote Hasa katika Maslahi na matakwa ya wananchi,,im free opened MIND! Ndo maana naweza kusema kuwa CCM sasa kuna baadhi ya Mawaziri wanafanya Vizuri mfano,Kagasheki na Mwakyembe!

Si hata vibaya CDM wakawa wanawapongeza Mawaziri wanaofanya Vizuri ili kuonesha Hawako katika kupinga tuuuu,,kwasababu wanachi wengi wanadhani UPINZANI ni Kupinga tu.ili kuonesha They lay at right SIDE!

Juzi nilitoka kupiga soga na 'Waswahili' mtaani,Kutaka kujua lile tukio la R.I.P Mwangosi wananchi wamelipa uzito gani!Nikapita kwa vibanda vya mamantilie hadi kule kwenye GAHAWA!

Wananchi hasa wale ambao hawana Muda wa kusoma Magazeti wala Kuangalia TV( kutokana na Ugumu wa Maisha) wanalaumu CDM!!Kuwa chama cha MAUAJI na VURUGU!!

Ushauri wangu sasa ili kuwaweka wananchi sawa,

1)Kuna Picha ile ambayo MWANGOSI anaonekana akilipuliwa Laivu,Isambazwe bure mpaka vijijini tena sana...Hii itasaidia kufuta tongotongo na Kuchafua chama.

2)Ile VIDEO ya Mauaji isambazwe kwa CD tena bureee,kila mtu ashuhudie yale mauaji!

BAJETI hai haitazidi 10 millioni,bt manufaa yake yataonekana 2015!

CHADEMA mkipuuza hiki kitawa'COST sana!
 
mimi nafikiri hili ni wazo zuri sana , jana kulikuwa na mkutano wa ccm katika viwanja Tanganyika parkers kawe(DSM),mda mwingi ulitumiwa na makada hao wa ccm kuelezea kuwa cdm ndo chanzo cha maandamano na vurugu zinazopelekea watu kuuwawa,kwa hiyo kama hii propaganda itaendelea bila kushughulikiwa tusishangae kuona ccm inapata mtaji!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom