Propaganda ya mauaji imefanikiwa... CHADEMA fanyeni hiki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda ya mauaji imefanikiwa... CHADEMA fanyeni hiki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theHAVARD_product, Sep 15, 2012.

 1. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kwanza nianze kusema mimi ni NAM person..sifungumani na Upande wowote Hasa katika Maslahi na matakwa ya wananchi,,im free opened MIND! Ndo maana naweza kusema kuwa CCM sasa kuna baadhi ya Mawaziri wanafanya Vizuri mfano,Kagasheki na Mwakyembe!

  Si hata vibaya CDM wakawa wanawapongeza Mawaziri wanaofanya Vizuri ili kuonesha Hawako katika kupinga tuuuu,,kwasababu wanachi wengi wanadhani UPINZANI ni Kupinga tu.ili kuonesha They lay at right SIDE!

  Juzi nilitoka kupiga soga na 'Waswahili' mtaani,Kutaka kujua lile tukio la R.I.P Mwangosi wananchi wamelipa uzito gani!Nikapita kwa vibanda vya mamantilie hadi kule kwenye GAHAWA!

  Wananchi hasa wale ambao hawana Muda wa kusoma Magazeti wala Kuangalia TV( kutokana na Ugumu wa Maisha) wanalaumu CDM!!Kuwa chama cha MAUAJI na VURUGU!!

  Ushauri wangu sasa ili kuwaweka wananchi sawa,

  1)Kuna Picha ile ambayo MWANGOSI anaonekana akilipuliwa Laivu,Isambazwe bure mpaka vijijini tena sana...Hii itasaidia kufuta tongotongo na Kuchafua chama.

  2)Ile VIDEO ya Mauaji isambazwe kwa CD tena bureee,kila mtu ashuhudie yale mauaji!

  BAJETI hai haitazidi 10 millioni,bt manufaa yake yataonekana 2015!

  CHADEMA mkipuuza hiki kitawa'COST sana!
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwananchi yupi wa leo asiyejua hii kitu wewe mtu! hata kama hasomi magazeti wala hatizami tii vii, ataipata story kwenye kijiwe,shambani,kazini,bar,msibani,harusini,hotelini kwenye daladala,ataambiwa na mwanae,babake.mamake,mjombake,shangazie,kaka au dadake!!!!! burazaa huu ni mtiti cos raia wa leo wa nchi hii ni wapya kabisaaa wale wa zamani wamekufa wote!

  Ane wai ushauri wako umezingatiwa.
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  wazo zuri sana. M4C ilifanyie kazi
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Habari za kwa mama ntilie nazo! Huyu naye ni GT
   
 5. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Binafsi natoa Ushuhuda Leo tarehe 15/09/2012 nilikuwa nasafiri kutoka Moshi kuja Mwanga. Kwenye kibasi watu wakawa wanajdili kuhusu hali ya Nchi ilivyo. Wanashukuru kama sio CDM tusingejua EPA ni nini!

  Kama sio CDM tusingejua misamiati mipya ya Polisi kutuua huku wakisema "Ameuwawa kwa kupigwa na kitu Kizito(BOMU) Ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali (Risasi - Muuza Magazeti Moro) Wamepigwa na Raia wenye Hasira (Wenje na Machemuli Mwanza) kwa hiyo ndugu yangu mleta thread.

  Ukweli we unafungamana na CCmabwepande. Huo ushauri wako upeleke huko huko kwa wanamabwepande wenzako KELB.
   
 6. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Hawa ndo wapiga kura....
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Wapi wewe.kawadanganye magamba wenzako kwa popaganda laini ivyo.
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Sio kweli uliyoyasema, ni wananchi wachache sana tena nidra kukutana nao wakilaumu cdm kwenye hayo matukio ya mauaji hata ukisikiliza tu vipindi vya radio utasikia wa kicomment kwa kulaumu jeshi la polisi kutumia nguvu kuizibiti cdm!

  Umejaribu kutunga story mkuu!
  Kwa hayo matukio kwa kweli jeshi la polisi lina laumiwa sana.

  Tena wengine wanahoji kwa nini nchimbi aliwasingizia wafuasi wa cdm kuwa walirusha kitu kizito?

  Hao wanao lahumu cdm tena wakati wanajua ukweli ni ccm na mabaraza yake:

  Tafadhali usiwasingizie wananchi kabisa wanaelewa kila kitu si watu wa kudanganywa kama huko nyuma walivyo kuwa wanawadanganya/!
   
 9. k

  kapongoliso JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,136
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Sheria zinazotungwa na Said Mwema na kutekelezwa na Kamuhanda! Ha haha ha ha haha usitake nijipalie kwa kucheka. Jaribu kuchukua muda ufuatilie mapinduzi ya Ufaranza (1789) mfalme kilimpata nini na mkeo malkia Antoniette. Wewe uspende kudanganya watu wakose kwa kukimbilia kibao kikigeuka muda si mrefu. Sheria za kikangaroo zimeshapitwa na wakati people are just taking stock who is who, where , when and history will tell and direct the course of events. Atawalaye kwa upanga atakufa kwa upanga. Karaghabau
   
 10. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umekurupuka kumjibu mkuu naamini hukutafakari. Tanzania ni kubwa kuliko unavyoidhania. Kuna watu hapa hapa dar hawana redio wala TV. Wao huzipata habari mtaani kwa kusikia. Najua hata na wewe umeona kuwa yawezekana mtu kupata habari kwa njia hiyo, lkn umeshajiuliza habari atakayoipata mtu toka kwa mjumbe wa nyumba kumi ambaye akisikia CDM anasikia kichefuchefu itakuwa ya ubora gani?

  Hizo habari za mtaani za kusikia kwa mjomba na dada ndio balaa kabisa kwani mjinga mmoja anayeamini CDM wanaleta fujo anaweza akainfluence watu 100 kwa haraka na njia hii yako ikawa most negative

  Tanzania ni kubwa na ujinga ni sehemu ya maisha ya watu wa kijijini. Ushauri wake ni mzuri
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Toa uongo wako hapa......hakuna mwananchi asiyeujua ukweli wewe......nenda zako na ushauri wako wa giza

  Unajifanya hufungamani , basi utakuwa umetumwa na wanaofungamana.....rudi kajipange vizuri!
   
 12. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao ni hao uliowasikia wewe redioni, umeshafika vijijini na kusikia watu wanasemaje kuhusu vyama vingi, achilia mbali vifo vya juzi?

  Shigela naye ni mwananchi. Kuna watu nyuma yake na wengine wanamsikiliza na kumwamini zaidi ya magazeti na redio kwani wanaamini kwa wadhifa wake anafahamu zaidi. Wassira naye ni mwananchi na ana wafuasi nyuma yake. Nape naye ni mwananchi na ana wafuasi.

  Usiseme wananchi wanaelewa as if uliongea nao wote. Kama unakaa Sinza unaweza kudhania hivyo lkn ukienda Buguruni ukamsikia mama lishe anachoongea utasikia kichefu chefu. 'Ah hawa CDM wanataka tu kutuletea fujo wengine sisi tutakimbilia wapi. Miaka yote tumejiuzia maandazi yetu hapa bila shida wao kwa uroho wao wa uongozi kazi kufanya fujo tu. Polisi wameshaambia msifanye kikao leo wanabisha, sasa wao na polisi mwenye nguvu nani, aah'

  Mtu mwenye maneno ya hivi unaweza ukamuhesabu katika upande wa harakati?
   
 13. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa nini wewe na shoga yako mkilielewa jambo mnadhani limeeleweka nchi nzima? Wewe ni mfano wa watu wasiofikiri. Hebu jaribu kufikiri nje ya mipaka ya maisha yako kabla hujakurupuka kutukana muanzisha mada.

  Kama shughuli zako ni ofisini-nyumbani-ofisini-nyumbani huwezi kupata picha ya watu wanafikiri nini. Sisi wengine shughuli zetu ni za kuhamahama leo hapa kesho pale, tunasikia mengi na tunakutana na watu tofauti. Amini nakuambia, wapo watu wengi ambao hata ukiwaambia nini, bado watakwambia 'CDM walisababisha kwa kutotii amri halali ya polisi'

  Juzi tu hapa nilikuwa Tabora, mfanyakazi wa ngazi ya kati ya ofisi ya bodi ya Tumbaku anajadili hoja hii hii na wenzake, pamoja na elimu yake ya wastani bado comment yake ilikuwa 'ah hawa CDM nao sasa wamezidi. Haiwezekani kila siku wao mizozo tu na polisi. Kama hao polisi wangekuwa wakorofi mbona wasiwapige CCM au wasiwapige watu wakiwa kanisani? lazima tu kuna kitu watakuwa wanafanya, tena nimesikia wanalipwa na nani sijui ulaya huko waanzishe fujo ili hao wazungu wauze silaha. Nyie tuendeleeni tu na ushabiki wa kijinga, maisha ya vita sisi hatujayazoea'

  Kama huyu aliyeko ofisini ana mawazo haya, umeshajiuliza wa shambani ana mawazo gani ikiwa habari anazitegemea kwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji?

  Msipende kupuuza jambo kabla ya kulitafakari. Tanzania haiishii saluni unakofanya kazi, kuna vijiji na mapori. Ikiwa shigela anayeishi mjini anaongea upuuzi ule, mama yake aliyemwacha kule kijijini atasema nini juu ya tukio kama hilo kama si kuishia kuilaumu CDM
   
 14. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri, haijalishi wangapi wanajua au laa, lakini hili tukio liwe chachu ya kuwafungua watu walio vijijini zaidi ambao mara nyingi hutumia redio Tanzania kupata habari za kitaifa kwakuwa redio hii ndio propaganda ya ccm.
   
 15. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  MTENGETI

  ww unazungumzia watu wenye Acess ya kusafiri,watu wenye kupita hata kwenye meza ya Magazeti....!!! Nazungumzia watu wa NAMTUMBO na Mbamba Bay,,,nk
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mkuu ww ni GT,kiukweli PROPAGANDA hii ya Magamba imefanikiwa sana....
   
 17. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hapa tulipofikia kama taifa, mwananchi yeyote mwenye akili timamu hawezi katu kutamka maneno kama hayo hapo juu ila awe ni mwongo, mnafiki au limbukeni. Hizi sifa zote tatu zinamfanya awe adui mkubwa wa Watanzania wote wanaolipenda kwa dhati taifa lao na wana nia njema ya kulikomboa taifa kutoka mikononi mwa walafi, wezi na wauaji waliojificha chini ya kivuli cha chama tawala, CCM. Huwezi kudai unalipenda taifa lako huku umesimama kando ukishuhudia linavyoteketezwa na genge la wahuni...genge hilo linaweza kuwa madarakani kisheria (sheria walizozitunga wao na kuzisimamia) lakini kamwe hakina uhalali kama vitendo vyake vinakinzana katiba ya nchi.

  theHAVARD_product, watu wa aina yako ni hatari kuliko hata hao polisi ambao, kama mazezeta, wanaamriwa kuwaua ndugu zao ambao ilitakiwa wawalinde kwani ndio waajiri wao wanaowalipa mishahara. Utakuwa punguani mkubwa kama unaamini kwamba siku zote uwongo utadumu, ni swali la muda tu na serikali yoyote ile inayotegemea uwongo ili iweze kubaki madarakani, haidumu, huo ndio ukweli. Yeyote yule, awe Kagasheki au Mwakyembe, anayeshirikishwa katika utendaji wa kila siku wa serikali hiyo, anabariki vitendo vyote vinavyofanyika ndani ya serikali, hawezi kukwepa lawama. Ni kama dereva anayeendesha gari huku amewapakia wezi, akakaa pembeni akishuhudia wanavyoiba, halafu anajitenga nao akidai kama dereva hajavunja sheria.

  theHAVARD_product, ningekuwa wewe nisingeendelea kutetea huu umbea uliouleta humu jamvini, kumbuka na sisi wengine tunawasikia wananchi wanasemaje. Je, baada ya propaganda za Mwigulu za kuwalaumu Chadema Igunga kwa kummwagia kada wa CCM tindikali na kumdhalilisha DC kwa kumvua hijabu, hali ilikuwaje baadaye huko Arumeru? Tofauti na maoni yako mimi nakuhakikishia kwamba hayo unayoyaongelea ndiyo yanazidi kuipandisha chati Chadema na ndio maana Kikwete yuko kimya hadi leo kuhusu kifo cha Mwangosi, wananchi wameamka hawataki tena kusikia matamko ya kipuuzi, wamechoka nayo. Ya Ulimboka bado yakaja ya Chona na hata vumbi haijatulia yamekuja ya Mwangosi...that is the way the cookie crumbles, na bado...eti una open mind, open mind my foot!
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Wewe huwajui wa TZ, analysis yako nadhani umeuifanya kwenye koo za viongozi wa CCM
   
 19. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kabisa jamaa ametoa ushauri mzuri Tz wajinga ni wengi haswa wale wenye mafungamano na magamba.
   
 20. S

  SUPERXAVERY Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na huo ndio ukweli ambao cdm mmekua mkiupotosha umma kwa kutumia media, kukashifu kila chombo cha habari chenye mtizamo tofauti nanyi, watanzania ukiacha washabiki wa cdm, ni waelewa and soon mtalitambua hilo.
   
Loading...