Propaganda hizi za TBC ni za kipuuzi, za hovyo

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,384
TBC kwa sasa wanafanya propaganda za kipuuzi na za hovyo mno - sijui lengo lao ni lipi pale wanapoonesha vipande vya picha za vita na mauaji katika nchi mbalimbali hasa Rwanda katika taarifa yao ya habari.

Kwa udadisi tu nilitaka kuangalia taarifa yao ya habari usiku wa leo kuona watakavyoripoti mahubiri ya ibada za Krismas kwa siku ya leo...kilichooneshwa wala si mahubiri bali habari tu za kumsifia Magufuli, hakuna habari ya Askofu au Mchungaji yeyote kuwasemea wananchi wa kawaida, bali ni Magufuli...Magufuli...Magufuli tu mwanzo mwisho.

Kibaya zaidi pale ambapo Maaskofu walizungumzia umuhimu wa kulinda "AMANI", habari zinaripotiwa kwa namna ya kuwalaumu wananchi na kuwataka eti waige mfano wa Rais Magufuli kutunza "AMANI"...sasa unajiuliza Magufuli kafanya kipi kati ya hayo mawili - amesaidia kudumisha upendo miongoni mwa raia au amechochea na kukuza mafarakano na chuki miongoni mwa Watanzania?

Msisitizo mkubwa katika taarifa ya habari ya TBC ni wananchi kutii mamlaka iliyopo madarakani na kumtii Magufuli, sasa mimi najiuliza kwani kuna UASI hapa nchini? Kwani wananchi wana shida gani na Magufuli, si kila siku tunaambiwa anapendwa na hata wabunge na madiwani wamejiuzulu kwa sababu wanampenda?

Hizi propaganda ni za hovyo, za kipuuzi!
 
Anzisha yako!
 
Pale hakuna wanahabari na TBCCM kuitwa "chombo cha habari" ni sawa na kuvitusi vyombo vya habari, ashukuliwe mungu nchi iliruhusu vyombo vya habari binafsi kitambo, ingekua ni maamuzi ya sizonje basi wote tungelazimishwa kutizama uharo wa TBCCM
 
Back
Top Bottom