Proof: Binadamu alitengenezwa na Aliens

Safi sana mkuu...ila muache ahangaike nayo kwanza hiyo naamini ataanza kuona hisia tofauti na mazingira mengi atayaona kama sio rafiki tena but akizoea atajiona hero kinyama...ukweli ndo huo...kuna sehemu ataona kabisa illusion inabadilika na kuwa reality....
he will be able to view things in two planes of dimensions..

Ndo atajua kuwa mambo yote anayoyaona ni Ilusion 100% hakuna reality hapo na hapo ndo atajua kuwa kumbe kuna maisha nyuma ya pazia na faida yake ataijua pia...



Sent using Jamii Forums mobile app

 
Ndugu yangu kabla sijakupa list hii nakutahadharisha kuwa unaweza ukaharibu mfumo wako wa fikra juu ya wanadamu au Mungu utakapo soma chochote kati ya vitabu hivi, utaharibu mfumo wako wa maisha pamoja na Imani kwa ujumla.

1. The Secret Teachings of All Ages by Manly P. Hall.

2. The Secret Doctrine By Helena P. Blavatsky.

3. The secret wisdom by Annie Besant, Theosophical Society publishers.

4. Isis Unveiled " The Master Key to the Mysteries of Ancient and Morden Science and Technology, Volume 1&2

Nafkiri itakuchukua mwaka mzima kusoma hivi vitabu mpaka uvimalize.


Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekupata vema,, But, all in all I have to read them. Nimefanikiwa kuvipata vyote hapo. Kipi chafaa kuanza nacho?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao Aliens wanaidadi ya wanadamu ambao wanajishughulisha kutafuta hayo madini?

Maana ni asilimia ndogo tu inayojishughulisha na utafutaji wa hayo madin.

Hawaoni kama wao ndio waliowaumba binadamu wengi kwa kwa ajili ya kazi yao walipoteza muda wao?
Maana wengi wetu tuko bize na mapenziiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nimeisoma lakini bado sijaona hiyo "Proof" au "Evidence" kuwa tulitengenezwa na Aliens. Umeelezea tu DNA ilivyo na kuwa na non-functional genes sio ushahidi kuwa Aliens ndio wameetuumba. Kutojua non-coding genes zina kazi gani sio kwamba hazina kazi..ni kwamba bado wavumbuzi hawajajua kazi yake kwa sasa.

Na hiyo rhesus factor negative ndio Dah hamna hata uwiano na Aliens lututengeneza kwa taarifa uliyotoa.
Sasa na hizo Empire za Aliens walizopigana na kudondosha madini Duniani kuna proof gani kwenye hilo? Nani aliwaona wakipigana? alijuaje walipigana? kuna ushahidi gani kuwa hayo madini yalianguka?kwamba kumeonekana mashimo makubwa yenye madini Duniani? maana kama yalianguka kungekuwa na Impact kwenye tabia nchi ya maeneo husika kama ambavyo vimondo vinavyodondoka..

Enewei bado hapo hujaweka "Proof" kuwa tulitengenezwa na Aliens kama kichwa cha habari cha makala yako kinavyosema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom