Programu ya Kuboresha Utumishi wa Umma

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
WanaJambo wenzangu... Leo naona Michuzi ameshatupostia hotuba ya Mhe Rais JK leo katika uzinduzi wa awamu ya pili ya rejeo hapo juu inapatikana at:
http://issamichuzi.blogspot.com/2008/01/jk-leo.html

Nimeisoma na kuielewa ipasavyo lakini my concerns are:
1. Mhe anasema CSRP phase I imepelekea kuwepo na serikali ndogo yenye ufanisi mkubwa - Hili mimi nalipinga moja kwa moja sababu katika maisha yangu serikali ya awamu ya 4 ina Baraza kubwa kuliko zote

2. Gharama ndogo za uendeshaji wa serikali - Hapa itakuwa ngumu sana kukubali ukizingatia manunuzi ya magari (VX,GX etc), safari za JK na viongozi nje na ndani ya nchi (frequency and size of delegations)

3. Ajira hew serikalini - Hili bado ni shida sana haswa vijijini na kwenye halmashauri ndogo... Pia nakubali kufuta ajira hewa lakini kuruhusu kuwepo kwa Vihiyo, na bias in recruitment (ndugu, jamaa na marafiki) havijaguswa wala kuongelewa!!

4. Maslahi kwa watumishi yame/yanaendelea kuboreshwa - Hili sina la kusema zaidi ya kutoa ushauri uende kuangalia hali ya walimu, waganga, mabwana shamba sio mijini/majijini bali vijijini na kwingineko kisha u-make conclusion on that!!

5. Swala la teknolojia na uzinduzi wa jengo - Hapa wala sisemi, manake tunashikia kununua na kuweka kopyuta lakini serikali yenyewe imeupa mgongo swala la "Fibre-optical backbone" liende kwa manyani.... Kuelezea hili ni kwamba TANESCO na wawekezaji wengine kila mtu anakimbilia njia yake na hakuna combined effort. So hili ni kujaza maji kwenye gunia kwa kujaribu weka vijikompyuta lakini hatuangalii mbele!!!

My take, hii ni nyingine katika vile vijisifa vya majukwaani lakini in real life ni gumzo la alinacha!!!
 
Hivi Kikwete anahisi watz wote ni wajinga au? Seriously there are things Mr.Presidaa anaongea unahisi either wamemnukuu vibaya au?Au hajui ni watu wa aina gani anaongea nao?!!.

Yaaani serikali hii yenye mawaziri timu sita za soccer anasema ni ndogo? Ukubwa huu anasema umeleta gharama ndogo za uendeshaji?-What a contradiction from Mr.President jamani!!!?
 
Tatizo lipo bado kwenye Kongamano warsha workshops na seminars. ukijumlisha na VX na GX basi kaazi kweli kweli kwenye utekelezaji!
 
Ttizo kubwa na mkuu wetu huwa hotuba zange mara nyingi hazikwantify anachokizungumza mambo mengi huwa yanakuwa generic with vague statements. Anywayz maybe hio ndio lugha ambayo watanzania walio wengi wanapenda kuisikia.

1. Alichotakiwa kusema hapo ni huo udogo wa serkali anamaanisha nini na analinganisha na nini au wapi?

2. The same na kwa gharama za uendeshaji anamaanisha nini na analinganisha na nini au wapi?
 
Back
Top Bottom