Programming Language swahili version

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,409
9,183
Lugha inayotumika katika Programming languages zote ni kiingereza. Je zipo sababu za msingi ya kupendelea kiingereza kuliko lugha nyengine yeyote? Kwanini kusiwepo kwa mfano java swahili,chinese au arabic versions?

Nadhani ukibadilisha lugha itakuwa sio Java tena, maana keywords zitakuwa sio zenyewe.
Unaweza ukafanya kama academic exercise lakini sidhani kama kuna sababu ya msingi kufanya hivyo.

Nahisi pia itabidi to re engineer compiler kwa sababu compiler fuctions by recognizing keywords.

Yeah itabidi ubadilishe kote au uweke layer ya kutranslate back into English, kazi bure.
Sidhani kama lugha ya programming ni kikwazo kikubwa kwa Watanzania maana keywords zenyewe ziko 50 tu, labda documentation ya Kiswahili au material za Kiswahili zingesaidia zaidi.

Lugha inayotumika katika Programming languages zote ni kiingereza. Je zipo sababu za msingi ya kupendelea kiingereza kuliko lugha nyengine yeyote? Kwanini kusiwepo kwa mfano java swahili,chinese au arabic versions?
habari, naomba nilijibu swali hili kama ifuatavyo,
si kweli kwamba lugha zote za kuprogram zinatumia kiengerza kuprogramu, 1/3 kati ya zaidi ya lugha 2400+ za kuprogramu hazitumii kiengereza, na ongelea zaidi ya lugha 700+ ambazo hazitumii kiengereza katika kuprogramu, mfano wa lugha hizi ni QALB ambayo ni ya kiarabu, yorlang ambayo hutumia kiyoruba kuprogramu, chinese-python na nyingine nyingi mno.

fumbo limekuwa kama kuna lugha nyingi mno ambazo hazitumii kiengereza kuprogram kwa nini hazitumiki, sababu kuu ambayo yaweza kusababisha jambo hili ni kwamba, lugha hizi ni kawamba zimetengenezwa kwa lengo (domain specific language - DSL) au watu fulani (essoteric) tu.

Swali jingine ni kwamba je kuna lugha ya kuprogramu kutumia kiswahili, ndiyo ipo lugha ya kuprogram ya kiswahili (DSL - educational purposed language), lugha hii imetengenezwa na kampuni inayoitwa edtech and IT Solutions.

Lugha hii ya kuprogram kwa kiswahili inafahamika kwa jina la swap au swahili program language na unaweza kuipata kupitia

swahili programming language package - swapro
swahili programming language tutorial - Trusted to help and guide you get the best IT solutions
swahili programming language github - ibnsultan/swahili-programming-langauge

Asante;

Ukibadil LUGHA.. umebadir LUGHA ya KU program..

Means... Sisi Waswahili TUUNDE programming LANGUAGE yetu wenyew... Kitu ambacho ni Ndoto za Alinacha

Tuanze na kubuni programming language ya Afrika kabla kuwaza suala la lugha, ukweli Waafrika tuko nyuma sana kwenye kila kitu. Na sio sisi tu kwenye bara hili, ila mtu mweusi amechelewa sana hata kama ni mzawa wa huko Ulaya. Hebu fanya utafute top programmers in the world, hamna mweusi hata mmoja.
Ukweli mchungu ila ndivyo ulivyo, tuukubali ili tuanze kurekebisha.

Mimi mara nyingi huwa nachat na Wachina kwenye Skype, ambao wengi hawafahamu kingereza, akiandika Kichina nakifanyia copy pasting kwenye translator, kisha naandika Kingereza na kukibadilisha Kichina namtumia, haya masuala ya lugha bana......

WeChat ndo naona nzuri sana kuchat na wachina, Yaani yeye akiandika kichina chake kule na kukutumia ww automatically inakutranslatia kwa lugha ya English unaelewa, Na ww vilevile unamjibu kwa English ujumbe ukimfikia automatically kule kwa chini ake unamtranslatia kwa kichina chake! Skype hawana hii kitu? Au mpaka u copy & paste kwenye translator ya Google?

Kuna mtu alinishauri kuhusu WeChat ila nikasuasua maana kufanya installation ya apps zozote za Kichina huwa naogopa maana hawakawii kuiba personal data zako zote, ok poa nitajaribisha ila nafahamu huwa through reference, yaani lazima ualikwe na mtu anayeitumia.

Alafu ina maswala ya kuscan QR code unaposajili ko uwe na access ya simu 2 moja yenye account inayofanya kazi ili uscan hapo ndio wanaponiachaga hoi! Sema iko vizuri sana naona hata whatsapp huwa wanaiba sana features zake nyingi kutoka WeChat...

Back
Top Bottom