Program Note: Mada 5, Dakika 5, Siku 5 - Tutatoa Majibu!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,736
40,858
Kuanzia Jumatatu - In Sha Allah - nitaanza mfululizo wa siku tano wa kujibu hoja mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa dhidi ya mabadiliko ya kimfumo, kiutendaji na kimwelekeo wa sera ambayo yanafanyika chini ya Rais Magufuli. Nitajibu baadhi ya hoja za ndugu zetu ambao mabadiliko haya yamewaacha mbali kifikra na wanatatizika.

Baadhi ya maswali nitakayoyajibu na kuweza bila utata kubadili mawazo ya fikra za baadhi ya ndugu zetu hawa ni kama haya (hayako kwa mpangilio wa umuhimu au siku):

- Je Magufuli ni Dikteta? Je, anatumia madaraka yake vibaya?
- Je kutumbua watendaji ambao ni wabovu au wasioendana na kasi ya Rais ni uonevu?
- Je, Katiba Mpya ni tiba ya matatizo yetu yote ya kisiasa na kiutawala? Tuanzie kwenye Katiba ya Warioba?
- Ni kweli upinzani ulibadili 'gia' angani?
- Kwanini siamini CCM ilivyo sasa haiendani na kasi Magufuli? Inaweza kubadilika na ikibadilika maana yake nini - kwa wana CCM wenyewe na nje yake?
- Ni jaribio gani la kisiasa linapangwa dhidi ya Magufuli kuzuia asiendelee na kasi hii?
- Ili mtu apate uhalali wa kisiasa ni lazima awe mkosoaji?
- Mambo gani Magufuli akifanya yatazidi kumuongezea maadui lakini yatazidi kumthibitisha kama kiongozi wa zama hizi mpya?
- Na maswali mengine mengi ambayo yamejitokeza kwa miezi hii karibu saba tangu Rais Magufuli aingie madarakani?

Operesheni Zinduka Inaendelea... "hatutaki kuwaacha ndugu zetu nyuma..."

MMM
 
MMM,
Kuna mtu amekuomba au amekuagiza au amekutuma kua utoe majibu ya hayo uliyoyataja? je utayajibu ukiwa na fikra huru au ukada? na unaonaje na kudhani kua majibu yako ndo yatakua majibu sahihi?

Mzee wangu nchi haiendelei kwa style ya kusifia kila kitu, by the way maelezo yako ni fikra yako wala siyo ya waTanzania wote.
 
Tunaisubiri operesheni zinduka pamoja na kwamba kuna wengine wameamua kuvaa ujinga ili waweze kupinga kila kitu kinachofanywa na Rais Magufuli.

Yes, kuna mapungufu machache sana katika utendaji wa Rais Magufuli.
 
Je ni halali kumtumbua jipu mtu kwa kutumia press na kumrudisha kimyakimya bila press kwa mlango wa nyuma? je hilo lina tofauti gani na tawala zilizopita?
 
Tunaisubiri operesheni zinduka pamoja na kwamba kuna wengine wameamua kuvaa ujinga ili waweze kupinga kila kitu kinachofanywa na Rais Magufuli.

Yes, kuna mapungufu machache sana katika utendaji wa Rais Magufuli.

Wewe kuna siku ulishaona kosa angalau moja alilofanya Rais? unapowaita wengine wajinga kwa kutoona mazuri ya rais na wewe unavaa ujinga huohuo ya kutoona mabaya/makosa ya rais.
 
MsemajiUkweli;
Hayo wewe unayoyaona kuwa ni machache huenda ndio yaleMakubwa yanayoweza kuiangamiza nchi yetu. Usimhesabu kwa makosa mhesabu kwa aliyokubali kukosolewa. Usimchukulie ka yeye ndiye akili yoote ya hao zaidi ya milioni 50 anao waongoza.
 
Baadhi ya maswali nitakayoyajibu na kuweza bila utata kubadili mawazo ya fikra za baadhi ya ndugu zetu hawa ni kama haya (hayako kwa mpangilio wa umuhimu au siku): ...
MMM
Ongezea na hili:
- Je, ni utaratibu gani unaomruhusu JPM kuelekeza baadhi ya fedha za serikali kwenda kufanya kazi katika wizara au sekta fulani bila ya fedha hizo kuidhinishwa na bunge? Je, kwa utaratibu huo, kuna haja yoyote tena ya bunge kuendelea kuwa linakaa vikao vya kupitia na kupitisha/kuidhinisha bajeti ya serikali?
 
MMM,
Kuna mtu amekuomba au amekuagiza au amekutuma kua utoe majibu ya hayo uliyoyataja? je utayajibu ukiwa na fikra huru au ukada? na unaonaje na kudhani kua majibu yako ndo yatakua majibu sahihi?

Mzee wangu nchi haiendelei kwa style ya kusifia kila kitu, by the way maelezo yako ni fikra yako wala siyo ya waTanzania wote.
Punguza hofu unachoogopa nini!

Huu mchezo hauitaji hasira.
 
Wewe kuna siku ulishaona kosa angalau moja alilofanya Rais? unapowaita wengine wajinga kwa kutoona mazuri ya rais na wewe unavaa ujinga huohuo ya kutoona mabaya/makosa ya rais.
Yes, nilishaona kosa alilofanya Rais Magufuli.

Kwani vipi?
 
MMM,
Kuna mtu amekuomba au amekuagiza au amekutuma kua utoe majibu ya hayo uliyoyataja? je utayajibu ukiwa na fikra huru au ukada? na unaonaje na kudhani kua majibu yako ndo yatakua majibu sahihi?

Mzee wangu nchi haiendelei kwa style ya kusifia kila kitu, by the way maelezo yako ni fikra yako wala siyo ya waTanzania wote.
Subiri usome kwani wote wanaouliza wametumwa? Nitajibu kwa kadiri ya uelewa wangu wa mambo yanavyoendelea. Stay tuned
 
Siku hizi nikikuta bandiko la mwanakijiji nasoma tu sentesi mbili za mwanzo na mbili za mwisho kisha nakimbia. Ni tofauti na kipindi cha nyuma alipokuwa huru nilikuwa namsoma na hata kurudia tena na tena. Toka fikra zake ziende utumwani kusaka mlo wa siku dizaini ya kale kajamaa kalikotafutiwa u-DC amepoteza kabisa weledi wa uwakilishi huru.
 
Back
Top Bottom